Mkuu unachokitafuta hauwezi kukipata kamwe.
Na kama watatokea programer wa kutengeneza hiyo software inayokidhi mahitaji yote itauzwa zadi ya usd 2000.
Cha msingi ainisha aina gani ya simu unazozilenga wewe na aina gani ya matatizo unayokumbana nayo ili uweze kusaidiwa.
Kuna box zinazodili na maswala ya network unlock, network repair na tasks ndogo ndogo.
Zipo zinazodili na cpu tu na siyo brand ya simu.
Zipo zinazodili na known brand pakee kama samsung, huawei, lg nk
Zipo kwa ajili ya chines phones nyingi hizi zinapiga hadi simu za batani.
Zipo za frp, zipo jtag, zipo za michoro ya saketi za simu nk.
Kama unataka zote sema kama unataka aina flani kulingana na simu unazokutana nazo sema ushauriwe hapa.