Boko Haram wauteka mji muhimu Nigeria

Boko Haram wauteka mji muhimu Nigeria

Kichwa Ndio Mtu

JF-Expert Member
Joined
Jan 17, 2014
Posts
3,079
Reaction score
1,719

140901201019_nigerian_army_512x288_reuters.jpg

Wanajeshi wa serikali ya Nigeria.


Kundi la Boko haram limefanya mashambulizi katika mji wa Bama na kusababisha mauaji ya watu wengi huku wengine wakitoroka.

Wanamgambo hao waliuteka mji wa Bama,ambao ni wa pili kwa ukubwa katika jimbo la Borno siku ya Jumatatu baada ya jaribio la awali la kutaka kuuteka mji huo kuzimwa na vikosi vya serikali.

Akizungumza na BBC ,wakaazi wamethibitisha kuwa mji huo umetekwa na kundi hilo na kwamba maelfu ya watu sasa wameachwa bila makao.

Mamlaka ya Nigeria bado haijatoa tamko lolote kuhusu shambulizi hilo.
Taarifa zinasema kuwa watu wengi wametoroka wakiwemo wanajeshi.


140826102145_boko_haram_fighters_512x288_afp.jpg

Zana za kivita zinazotumiwa na wapiganaji wa Boko Haram



Hapo awali jeshi la Nigeria lilitoa ripoti kuonyesha kuwa mpaka sasa limewaua wapiganaji 70 wa Boko Haram ,kutokana na mapigano kati ya kikundi hicho na wanajeshi Kaskazini -Mashariki mwa mji wa Bama.

Boko Haram walifika mapema asubuhi katika mji huo kwa magari ya kivita.Taarifa kutoka katika mji huo zinaeleza kwamba mashambulizi yalianzishwa na vikosi vya jeshi la Nigeria.

Msemaji wa kundi hilo la Boko Haram ameelezea hali ya mji huo kwa sasa kuwa wakaazi wa mji wa Bama wamekimbilia katika mji mwingine wa Borno na Maiduguri .

Nalo shirika la Amnesty International limetoa takwimu kuwa raia wapatao milioni nne wamekufa mwaka huu katika mgogoro huo kati ya Boko Haram na vikosi vya ulinzi vya Nigeria.




Chanzo
: BBC

http://www.bbc.co.uk/swahili/habari/2014/09/140901_nigeria_boko.shtml

Amnesty international imetoa takwimu kua mgogoro wa boko haramu huko Nigeria umepelekea vifo vya watu milioni 4 mwaka huu pekee.(miezi 8 tu). Ina maana kufikia mwezi 12 watafikia mil 5.

Kwa mwendo huu miaka 10 ijayo mgogoro wa boko haram utakua umepelekea vifo vya watu mi 50.

Swali langu:
Je nani anafadhili boko haramu? Binafsi nadhani kuna mkono wa wakubwa hapa.
 
watu milioni nne?. hiyo na genocide na genocide lazima UN wangeingilia. hebu nenda kavarify habari yako. unataka kusema kila mwezi walua watu 500,000. kila siku wwatu 16,000!.
 
watu milioni nne?. hiyo na genocide na genocide lazima UN wangeingilia. hebu nenda kavarify habari yako. unataka kusema kila mwezi walua watu 500,000. kila siku wwatu 16,000!.

Soma chanzo nilichoweka,sijajitungia. Nenda kwenye chanzo utaipata hiyo idadi.
 
Hiyo idadi ni kubwa mno ,pia kumbuka hawa wanaojiita sijui Boko Haram na pia isis na alqaeda wote hawa sio waislam kwa jinsi wanavyoendesha siasa zao,uislam kama ukiujua na kuusoma vizuri haufundishi waislam kwenda kuuwa binadamu bila sababu zozote zile,ukiangalia wengi wa wapiganaji wao wanatokea nchi za westerncountries,kama vile Canada Us,na england pamoja na nchi za europe,tatizo kubwa hapa mimi naona ni uchumi ndio chimbuko la haya yote tunayoyaona,hawa watu wa isis wanatumia hali mbaya za vijana wa west ku brain wash vijana kuwa siku moja watakuwa na nchi yao wenyewe na hali zao zitakuwa ni nzuri,vijana wengi wameingia katika huo utopia na kufikiria ipo siku watatoka kimaisha na watakuwa na nchi yao ambayo control ya uchumi itakuwa chini yao,hiyo ni ndoto ambayo haiwezekani kuwa reality.

Kwa upande mwingine hawa westerns nao ni watu wa kulaumiwa sana,unakuta hawa vijana wote wanaoingia katika makundi ka haya chimbuko lao ni watu wanaotoka katika marjinalized groups,watoto hawapatiwi ajira wanabaguliwa ndani ya society zao,hawana kundi wanalofikiria wanatoka na ni rahisi sana kwa vijana wadogo kama hawa kurubuniwa na ni rahisi wakaingia ndani ya traps ka hizi.

Uislam haufundishi haya yote tunayoyaona ndani ya national tvs,yaani mtu anafikia kumchinja mtu mbele ya dunia nzima bila kuogopa sijui hiyo authority wametoa wapi,na tatizo letu sisi waislam wengi au viongozi wetu wamekaa kimya bila kuyanyooshea vidole mabaya wanayoionyesha dunia.imeandikwa kuwa mungu wetu ni mungu wa compassionate sijui hivi vikundi hiyo compassionate mbona vinashindwa kuionyesha.

Siasa chafu ka hizo ni lazima zisikubaliwe kuingia nchini kwetu na huu umaskini tuliokuwa nao watu wengi wakisomeshwa nao wanaweza wakaingiwa na tamaa ka za watoto wa kiwestern,yaani kwenda kupigania dini na mali.Hii ni aibu kwa uislam na ni hatari kwa nchi zetu za kimaskini.
 
waswahilli wa bbcc swahili wameanza uswahili.
kutoka wikipedia.
Boko Haram (Western education is forbidden), Jama'atu Ahlis Sunna Lidda'Awati Wal-Jihad, is a militant Islamist movement based in northeast . The group has received training and funds from Al-Qaeda in the Islamic Maghreb, and was designated by the US as a terrorist organisation in November 2013. Membership has been estimated to number between a few hundred and a few thousand.

Boko Haram killed more than 5,000 civilians between July 2009 and June 2014, including at least 2,000 in the first half of 2014, in attacks occuring mainly in northeast, north-central and central states.[SUP][4][/SUP][SUP][5][/SUP][SUP][6][/SUP] Corruption in the security services and human rights abuses committed by them have hampered efforts to counter the unrest.[SUP][7][/SUP][SUP][8][/SUP] 650,000 people fled the conflict zone by August 2014, an increase of 200,000 since May.[SUP][9][/SUP]
 
watu milioni nne?. hiyo na genocide na genocide lazima UN wangeingilia. hebu nenda kavarify habari yako. unataka kusema kila mwezi walua watu 500,000. kila siku wwatu 16,000!.

Mkuu upo sahihi, hata mimi jana kuna uzi ulikuwa na habari kama hii eti watu milioni 4!!!!wameuawa toka january-hadi august???hata kama unakimbilia kutaja source changanya na za kwako kwanza!!!
 
Back
Top Bottom