Boko, Dar: Ajali mbaya yatokea baada ya Lori kukosa breki na kuvamia waendesha bodaboda na kupelekea vifo na majeruhi

Mhandisi Mzalendo

JF-Expert Member
Aug 23, 2010
6,052
9,855
Ajali mbaya imetokea Boko baada ya lori kufeli break muda huu.Inasadikika watu kadhaa wamefariki, bodaboda 20 zimesagwa, magari 10 yamegongwa.

Barabara ya Boko imefungwa na wananchi.

=====

UPDATES;

Dar es Salaam. Watu wawili wamekufa na wengine saba kujeruhiwa katika ajali ya lori la mchanga iliyotokea eneo la Boko Magengeni jijini hapa, wakati gari hilo likitokea njia ya Bagamoyo kuelekea Tegeta.

Kamanda wa polisi Mkoa wa Kinondoni, Jumanne Muliro alithibitisha kutokea kwa ajali hiyo saa kumi jioni baada ya lori aina ya Scania lilipopoteza uelekeo na kuanza kugonga magari mengine kwa nyuma na mali za watu zilizokuwa pembezoni mwa barabara.

“Magari aina ya Scania wengi wamezoea kuyaita mende, ilikuwa imebeba mchanga baada ya kupoteza uelekeo iliyagonga magari madogo mawili na baadaye lilihama njia lilizigonga pikipiki 12 ambazo zilikuwa pembeni, lakini madereva wa bodaboda waliwahi kukimbia,” alisema Murilo.

Mkuu huyo wa polisi Kinondoni alisema: “Eneo lile lina watu wengi wanafanya biashara lakini uzuri madereva wa pikipiki waliiona ajali hiyo mapema, hivyo wakakimbia na kuzitelekeza pikipiki zao.”

Alisema wanaendelea na uchunguzi zaidi kuhusu tukio hilo, huku majeruhi wakiendelea na matibabu lakini mmoja hali yake hairidhishi, huku akiwataka madereva kuzingatia sheria za barabara na kuhakikisha wanafanya matengenezo ya magari yao mara kwa mara.

Murilo alisema dereva wa lori hilo alikimbia baada ya kutokea ajali hiyo na wanaendela kumtafuta huku akimtaka ajisalimishe.

Hata hivyo, magari yanayosomba mchanga na yanayobeba mkaa yamekuwa yakilalamikiwa ama kwa uendeshaji mbaya au ubovu.

Licha ya bodaboda kuegesha eneo la Boko Magengeni, wamachinga nao hupanga bidhaa zao hasa wakati wa jioni.

Chanzo: Mwananchi


1.jpeg
2.jpeg
3.jpg
4.jpg
 
Sasa wananchi wa boko mnafunga barabara wakati lori limefeli breki?!


Pole kwa wahanga wote wa ajali
 
Asante kwa taarifa. Pole wote mliofikwa na msiba. Tuzidi kupeana update
 
Back
Top Bottom