Body itching after bath

George Betram

JF-Expert Member
Oct 10, 2015
4,524
6,013
wana JF hili tatizo linanisumbua muda mrefu sasa...
yaan nikioga tu mwili wote unawasha,yaan hii hali huwa inachukua kati ya dakika 25-30 mpaka mwili utulie...
yaan hadi nachukia kuoga wanandugu...
lakini pia sometime hata nikitoka jasho nawashwa pia...
tena mara nyingine hata nikiloa na maji ya mvua mwili unawasha pia...
anayeufahamu huu ugonjwa na tiba yake anisaidie jamani...
NACHUKIA KUOGA
 
Pengine una allergy.

1. Kuna kemikali katika maji haipatani na ngozi yako.

2. Kuna kemikali akatika sabuni haipatani na ngozi yako.

3. Maji ni aina gani? Ya bomba? Ya kisima?
"Hard water" yanaweza kukuwasha Kama yana calcium nyingi.

4. Oga maji ya vugu vugu au baridi. Kuoga kwa muda mwingi na maji ya moto inaondoa kinga ya ngozi ya mafuta ya ngozi na kukupa uwasho.

5. Usibadilishe sabuni au shampoo Mara kwa mara.

6. Tumia sabuni yenye povu dogo kama za watoto wadogo. Sabuni nyingi zinatengenezwa na nazi. Nazi ina kemikali Sodium lauryl sulfate, inakupa uwasho.

7. Sabuni unayotumia kufua foronya na taulo haipatani na ngozi yako.

8. Tumia cream baada ya kuoga.

9. Onana na daktari wa ngozi ili upimwe kama una allergy na kitu au chakula.

10. Kuna ugonjwa wa ngozi unaitwa Aquagenic Pruritus. Ngozi haipendi maji. Ukioga tu, unawashwa. Wanaweza kukupima kama unao.

Daktari wa ngozi atakupa skin test kujua kama una allergy na kitu gani au wanaweza kuchunguza kwenye damu pia.

cholinergic urticaria ni ugonjwa unaotokana na allergy na jasho lako mwenyewe. Huu pia unaweza kupimwa na daktari wa ngozi.
 
Kaka hata mm nilishawahi kuwa na tatizo kama hilo.Kwa kweli mpaka leo duniani hakuna daktari anayejua tiba ya hilo tatizo sababu mm nilizunguka hospitali nyingi sana na kufanya vupimo vingi hakuna kilichoonekana tofauti.Nadhani mafaktari au fani ya utabibu hilo halimo kwenye sylabus zao.
cha kufanya unapooga usijifute na taulo kwa kujiburuza buruza ila jifute kama unajikanda kanda.Ukifanya hivyo hutawashwa kabisa.Mm hii solution nilipata kwenye blog moja hivi tena kwa shida mno.
Try that kisha unipe matokeo kwa kuni pm.
 
Nina tatizo hilo maisha yangu yote. Ila mimi nikioga mchana ndio nawashwa mwili mpaka nijifute nipake lotion na kuvaa nguo. Nikioga asubuhi au jioni baada ya mazoezi siwashwi hata nisipopaka lotion.
 
Hilo tatizo linakera, linaweza kugeuza mvivu wa kuoga.
Nilikua na hilo tatizo sijui liliishaje labda kwa sababu siku hizi kila siku natumia maji ya moto peke yake.
Hehehe! Yaani mtu ukitoka bafuni ni full kujikunakuna kila kona, pole sana, i understand your pain.
 
Pengine una allergy.

1. Kuna kemikali katika maji haipatani na ngozi yako.

2. Kuna kemikali akatika sabuni haipatani na ngozi yako.

3. Maji ni aina gani? Ya bomba? Ya kisima?
"Hard water" yanaweza kukuwasha Kama yana calcium nyingi.

4. Oga maji ya vugu vugu au baridi. Kuoga kwa muda mwingi na maji ya moto inaondoa kinga ya ngozi ya mafuta ya ngozi na kukupa uwasho.

5. Usibadilishe sabuni au shampoo Mara kwa mara.

6. Tumia sabuni yenye povu dogo kama za watoto wadogo. Sabuni nyingi zinatengenezwa na nazi. Nazi ina kemikali Sodium lauryl sulfate, inakupa uwasho.

7. Sabuni unayotumia kufua foronya na taulo haipatani na ngozi yako.

8. Tumia cream baada ya kuoga.

9. Onana na daktari wa ngozi ili upimwe kama una allergy na kitu au chakula.

10. Kuna ugonjwa wa ngozi unaitwa Aquagenic Pruritus. Ngozi haipendi maji. Ukioga tu, unawashwa. Wanaweza kukupima kama unao.

Daktari wa ngozi atakupa skin test kujua kama una allergy na kitu gani au wanaweza kuchunguza kwenye damu pia.

cholinergic urticaria ni ugonjwa unaotokana na allergy na jasho lako mwenyewe. Huu pia unaweza kupimwa na daktari wa ngozi.
You nailed it!!
 
Kama ushauri wa Tokyo hapo juu ukiufanyia kazi naamini utaleta mrejesho mzuri!!
Lakini pia jizoeshe kutembelea saluni za kike ambazo wanafanya massaji! Ukifika omba mdada mzuri akufanyie body scrub angalau mara moja kwa kila mwezi! kuna scrub nafanyiwaga ya chumvi nakuhakikishia itatoa wadudu wote wanao washa kwenye huo mwili!!
 
Mkuu Thegame.

Kusafisha ngozi ulivyoelezea ni muhimu sana kwa afya ya ngozi yako.

Ugonjwa wa ngozi mwingine kama
Atopic eczema hautibiki kwa sababu unatokana na vitu vingi katika hewa kama pollen, stress za maisha, vumbi, kemikali katika sabuni na maji.

Mara nyingi, unalazimika kutumia cream maisha yako yote kupunguza uwasho lakini siyo kutibu kabisa.
 
Mimi pia nina tatizo hilo yaani kila ulichokielezea ndicho kinachonitokea. Hali huwa mbaya sn hasa pale unapojifuta maji baada ya kuoga kwa taulo au kwa kusugua sn mwili. Nimezunguka sn lkn sijapata solution na mpk sasa tatizo hilo linanisumbu japo najitahidi sn kupambana nalo kwa kutojisugua sn hasa kwa wavu wakati naoga, kujifuta maji kwa kanga nyepesi baada ya kuoga na kujitahidi kusafisha bafu na chumba kabla ya kuoga maana kama kukiwa kuchafu hali huwa mbaya zaidi hasa kama kukiwa na kinyesi cha panya au mjusi.
 
Mimi pia nina tatizo km hilo lkn najitahidi kupunguza muwasho kwa kutojisugua sn wakati wa kuoga na kujifuta kwa kitambaa chepesi au kanga baada ya kuoga, pia kwa kusafisha bafu na chumba chako kabla ya kuoga maana muwasho huwa mkali zaidi endapo chumba au bafu lako litakuwa na uchafu hasa wa kinyesi cha panya na mijusi. Kwakweli tatizo hili ni gumu sn kulitatua maana nimezunguka hospital kibao lkn sijapata suluhisho!!! Nafikiri kunahitajika uchunguzi wa kina kwa wataalamu wetu kugundua chanzo cha cha ugonjwa huu maana unasumbua mno.
 
Jamani naomba kusisitiza,jaribu hii njia,Unapooga baada ya kumaliza kuoga usijifute na taulo au nguo kwa kujisugua au kubalazia.Jifute kama kwa kujigusagusa au kujikanda kanda.Kamwe usijisugue au kubalazia.Jaribu hiyo utaona matokeo.
 
Kaka hata mm nilishawahi kuwa na tatizo kama hilo.Kwa kweli mpaka leo duniani hakuna daktari anayejua tiba ya hilo tatizo sababu mm nilizunguka hospitali nyingi sana na kufanya vupimo vingi hakuna kilichoonekana tofauti.Nadhani mafaktari au fani ya utabibu hilo halimo kwenye sylabus zao.
cha kufanya unapooga usijifute na taulo kwa kujiburuza buruza ila jifute kama unajikanda kanda.Ukifanya hivyo hutawashwa kabisa.Mm hii solution nilipata kwenye blog moja hivi tena kwa shida mno.
Try that kisha unipe matokeo kwa kuni pm.
nitajaribu hii kaka..!
nitakupa mrejesho haraka iwezekanavyo...
ila hata tauro niliacha kutumia kwasababu nilikua nikitumia tauro yaani ndo kama nalizidisha tatizo..!
 
Hilo tatizo linakera, linaweza kugeuza mvivu wa kuoga.
Nilikua na hilo tatizo sijui liliishaje labda kwa sababu siku hizi kila siku natumia maji ya moto peke yake.
Hehehe! Yaani mtu ukitoka bafuni ni full kujikunakuna kila kona, pole sana, i understand your pain.
we acha mkuu...
ili tatizo linanifanya nichukie kuoga...
yaani ni shida mkuu..!
 
Kama ushauri wa Tokyo hapo juu ukiufanyia kazi naamini utaleta mrejesho mzuri!!
Lakini pia jizoeshe kutembelea saluni za kike ambazo wanafanya massaji! Ukifika omba mdada mzuri akufanyie body scrub angalau mara moja kwa kila mwezi! kuna scrub nafanyiwaga ya chumvi nakuhakikishia itatoa wadudu wote wanao washa kwenye huo mwili!!
ahahahahah...
sawa mkuu...
nitajaribu na hii njia pia..!
 
Mimi pia nina tatizo km hilo lkn najitahidi kupunguza muwasho kwa kutojisugua sn wakati wa kuoga na kujifuta kwa kitambaa chepesi au kanga baada ya kuoga, pia kwa kusafisha bafu na chumba chako kabla ya kuoga maana muwasho huwa mkali zaidi endapo chumba au bafu lako litakuwa na uchafu hasa wa kinyesi cha panya na mijusi. Kwakweli tatizo hili ni gumu sn kulitatua maana nimezunguka hospital kibao lkn sijapata suluhisho!!! Nafikiri kunahitajika uchunguzi wa kina kwa wataalamu wetu kugundua chanzo cha cha ugonjwa huu maana unasumbua mno.
ndugu yangu pia niligundua huu ugonjwa unazidi pale utakapokua kwenye eneo lenye vumbi..!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom