Body Guard wa Kifipa

komedi

JF-Expert Member
Mar 6, 2011
204
17
Wakati marais mbalimbali wakiwa kwenye kikao huko Geneva nchini Uswisi kulitokea majigambo ya walinzi wa marais kati ya wale wa nchi zilizoendelea na wa nchi zetu hizi.....

Mlinzi wa Rais wa china alinyoosha mkono wake akagusa miwani yake na kuurudisha, ghafla gari lililombeba Rais wake likatokea na Rais wa China akashuka. Yule mlinzi akajisikia fahari sana kwa wenzake.

Kuona hivyo mlinzi wa Rais wa marekani akaamua kuonyesha kuwa wao ni namba moja akakohoa kidogo na mara hiyo gari la Rais wa marekani likatokea na Rais wa marekani akashuka. Yule mlinzi akajisikia fahari mno kwa teknolojia yao ya mawasiliano.

Walinzi wa Afrika wakajisikia vibaya sana mbele ya wenzao.

Ghafla mlinzi wa Rais wa Tanzania ambaye ni kijana wa kifipa akapigiwa simu na walinzi wengine na kumuuliza kama Rais anaweza kuletwa mahala hapo.
Huku walinzi wa kizungu wakiwa wanacheka sana kuona teknolojia inayotumika ilivyo ya kizamani, Mlinzi wa kifipa akajibu '' subiri kwanza nataka nitoe somo hapa''

Akatulia kimya huku marais wakiwa eneo la wazi nje wakisalimiana na wajumbe wa mkutano, ghafla akaingiza mkono mfukoni akatoa hirizi na kuitupa chini kisha akaiokota na kutoa mwamvuli na kujikinga. Ghafla ikaanguka mvua kubwa sana na kuwalowesha marais wote waliokuwepo. Baada ya dakika moja mvua ikakatika kabisa.

Akapiga simu na kuwaambia wenzake ''sasa Rais anaweza kuja''

Wale walinzi wa marekani wakabaki wanakodoa macho huku wakiuliza.

''what kind of intercom is that?''
 
he he heeeeeehh!!! Nimeipenda hii, njooni huku ili mshuhudie hayo aliyosema Komedi!!!
 
Hivi waafrika ndiyo tuko nyuma kwa kila kitu? mmh ni utani ila unaudhi ktk certain degree

Unakumbuka fimbo ya Musa kuwa nyoka na mchezo mzima ulioendelea pale kama wewe ni mtu wa dini? Jiulize maendeleo ya dunia hii maana yake ni nini? Kwamba wanadamu wameendelea leo kuliko alivyokuwa ameendelea Mungu siku za kina Musa?

No I mean don't worry mkuu, hizi jokes nyingine kuzielewa...you need to be a genius!!!!
 
Back
Top Bottom