dittu
Member
- Dec 2, 2016
- 75
- 53
Kuna siku nilikuwa nasafiri kutoka Dar kuelekea Dodoma tulipofika maeneo ya benzi akasimama jamaa mmoja, alivyosimaa mimi nikajua ni wale wale wa kuuza sabuni na vipidozi.
Alipoanza kuongea ndipo nikagundua jambo tofauti, alikuwa anazungumza kuhusu kutembelea vivutio vya utalii alizungumza mengi sana akiwahamasisha watu watembelee mbuga za Mikumi, Seluo na Udzugwa sababu kwa watu wanaokaa Moro na Dodoma ni rahisi kwako kuzifikia.
Baada ya kuzungumza akatoa nafasi ya maswali yanayohusiana na utalii tu, abiria tukaanza kuuliza na kujibiwa pia watu wakatoa changamoto jamaa akawa anazinoti na kusema kuwa atazifikisha sehemu husika na mwisho kabisa akagawa vipeperushi vyenye taarifa za utalii.
Mara nyingi tumekuwa tukiwalaumu sana bodi ya utalii kuwa hawatangazi, kwa hiki mnachokifanya tunawapongeza maana mtu akifanya vibaya tumkosoe, akifanya vizuri tumpongeze.
Endeleeni kuwa wabunifu maana isije kuwa nguvu ya soda baada ya muda muache.