Bodi ya Sukari acheni sinema, wajibikeni sasa

Songambele

JF-Expert Member
Nov 20, 2007
4,695
2,553
Kama ilivyo desturi hatuwezi kukaa kimya kuacha sinema za karne iliyopita ziendelee tena kila uchaguzi unapokaribia.

Sukari adimu kwa maelezo Yao wenyewe uzalishaji ni mdogo kuliko mahitaji.

Hili sio jipya zipo hatua hata mwenda ZAKE alichukua kupambana na uhaba wa sukari.

Wafanyabiashara wadogo kama Ada wanatolewa kafara kuficha uzembe, urasimu na uhafidhina wa Bodi.

Leo hii wametoa maofisa kwenda kukamata walanguzi, lakini hawakuwa na maofisa kwenda kuhimiza kuongeza uzalishaji.

HATUA zilizochukuliwa miaka 8 iliyopita zilikuwa za kidikteta za zimepiga buyu kama mara zote wanasiasa wanavyotuingiza chaka.

Mlitoa amri Jeshi la Magereza washirikine na NSSF kuanzisha kiwanda mbigili Leo mnazo sababu lukuki za kuelezea kwa nini mmefeli na hamja acha kusingizia mabadiliko ya tabia nchi.

Hamkumbuki kabisa kama Hao mliowapa dhamana kwanza wanamikono michafu na hawana records za kufanya mradi wa namna hiyo ukafanikiwa na mlikuwa mnalazimisha serikali ifanye biashara.

Azam wao wameweza na Wana records za kufanya vyema katika bishara.

Bodi ya Sukari kwanza muwatake radhi watanzania kwa kushindwa kutimiza wajibu wenu na kukosa weledi wa kushindwa kuwashauri wanasiasa njia iliyo sahihi.

Sukari ni BIASHARA na iamuliwe kama BIASHARA hizi politike imetosha na haya mambo ya kuficha penseli na nyie Hao Hao mnatusaidia kutafuta yaacheni bhana.

Hebu kubalini kwamba wanasiasa na Bunge yapo ambayo hawana weledi nayo wawa achie wafanya BIASHARA washauri kuhusu biashara

Bodi jipimeni wenyewe na mjichukulie hatua nyie wenyewe mtakaona inafaa.

Waachieni wauza sukari au wapelekeeni sukari wauze bei mnayotaka nyie.

Waziri wa Kilimo aongeshe weledi hapa Sasa kwa ku engage wafanyabiashara sio Yale mambo ya BB, watu wafunge viwanda kila sehemu Mbeya, Rukwa, Kigoma, Iringa pamoja na mabonde yote waliyonayo wamezuiwa wasifunge viwanda Ili Mapapa yauze sukari Yao kutoka nchi Jirani na waliopo wasibughuziwe.
 
Back
Top Bottom