asiyetabirika
Member
- Oct 14, 2019
- 46
- 55
Kwa niaba ya wananchi wanyonge na wenye kipato cha chini naomba nitokwe na maoni yangu juu ya mchakato uliopo bodi ya mikopo tokea hatua ya kuomba mkopo hadi kuja kupata matokeo kuwa umepata mkopo au haujapata.
Hadi sasa imekuwa ni muda mrefu sana unaotumiwa na bodi ya mikopo hadi kuja kutoa matokeo yaani hadi siku za kufunguliwa kwa vyuo zinakaribia majibu ya mikopo bado hayajatoka ikizingatiwa wao ndio huanza mapema kupokea maombi ukilinganisha na TCU, hii hali ya kuchelewa kwa majibu ya mikopo yanaweza athiri sana familia za watoto wa wanyonge/ masikini hasa endapo itatokea mtoto atakosa mkopo kwani kitendo cha majibu ya mikopo kutoka karibu na tarehe za kufungua vyuo kutasababisha muda wa maandalizi kuwa mchache hasa kwa wale ambao wanauwezo wa kuchangisha kidogokidogo kutoka kwa ndugu/jamaa ama kukopa kwa lengo la kuja kurudisha baada ya kupata mkopo. Lakini pia hii adha inaweza ikaleta athali hata kwa wale watakaolipiwa asilimia chache kwenye tuition fee (ada) kwani muda wa kutafuta pesa ya kujazia unaweza ukawa ni changamoto kwao.
Ombi langu nikuona nafasi ya teknolojia ikionekana hasa kwenye kuokoa muda, kwani kwa sasa tumeona maombi yanatumwa kwa mtandao tofauti na miaka yetu huko nyuma ya analojia, natumaini maoni yangu yatawafikia walengwa na yatazingatiwa kwa maslahi mapana ya jamii za wanyonge.