Bodi ya mikopo pokeeni maoni yangu

asiyetabirika

Member
Oct 14, 2019
46
125
Kwa niaba ya wananchi wanyonge na wenye kipato cha chini naomba nitokwe na maoni yangu juu ya mchakato uliopo bodi ya mikopo tokea hatua ya kuomba mkopo hadi kuja kupata matokeo kuwa umepata mkopo au haujapata.

Hadi sasa imekuwa ni muda mrefu sana unaotumiwa na bodi ya mikopo hadi kuja kutoa matokeo yaani hadi siku za kufunguliwa kwa vyuo zinakaribia majibu ya mikopo bado hayajatoka ikizingatiwa wao ndio huanza mapema kupokea maombi ukilinganisha na TCU, hii hali ya kuchelewa kwa majibu ya mikopo yanaweza athiri sana familia za watoto wa wanyonge/ masikini hasa endapo itatokea mtoto atakosa mkopo kwani kitendo cha majibu ya mikopo kutoka karibu na tarehe za kufungua vyuo kutasababisha muda wa maandalizi kuwa mchache hasa kwa wale ambao wanauwezo wa kuchangisha kidogokidogo kutoka kwa ndugu/jamaa ama kukopa kwa lengo la kuja kurudisha baada ya kupata mkopo. Lakini pia hii adha inaweza ikaleta athali hata kwa wale watakaolipiwa asilimia chache kwenye tuition fee (ada) kwani muda wa kutafuta pesa ya kujazia unaweza ukawa ni changamoto kwao.

Ombi langu nikuona nafasi ya teknolojia ikionekana hasa kwenye kuokoa muda, kwani kwa sasa tumeona maombi yanatumwa kwa mtandao tofauti na miaka yetu huko nyuma ya analojia, natumaini maoni yangu yatawafikia walengwa na yatazingatiwa kwa maslahi mapana ya jamii za wanyonge.
 
MZEE RAZA

JF-Expert Member
Feb 19, 2015
2,645
2,000

Majina ya waliopangiwa mikopo awamu ya kwanza ( wale ambao maombi yao hayana makosa) yatatoka kesho kutwa oktoba 17.

Kwa hiyo usihofu,
 
Rayzuh

Member
Sep 15, 2019
13
45
Hii ndo Tz

kokosai

Member
Dec 25, 2018
37
95
Hata kama watatoa kesho kutwa lkn wamechelewesha sana, hiyo itkw batch1 na zngn sujui itkw lini na vyuo ndy vinakaribia kufungua!!!!
 
kokosai

Member
Dec 25, 2018
37
95
Hata kama watatoa kesho kutwa lkn wamechelewesha sana, hiyo itkw batch1 na zngn sujui itkw lini? na vyuo ndy vinakaribia kufungua!!!!
 
BSL

Member
Dec 15, 2018
78
125
Uko sahihi ndy yangu kwani kwa dunia ya leo mambo yanatakiwa yaende nataka na kwa uwazi .unakuta familia inategemea mkopo afu anakuja kuambiwa kuwa kijana wao hatapata mkopo zikiwa zimebaki wiki 2 au 1 sasa fikilia familia hiyo inatakiwa itafute labda laki 9 ndani ya wiki 2 kama si kuwatesa ni nn? Bodi wabadilike tu toeni taarifa mapema ili familia masikini wauze ata shamba mapema ili kijana wao aende chuo
 
asiyetabirika

Member
Oct 14, 2019
46
125
sifa mojawapo ya kupata mkopo nilazima uwe umepata na chuo, so hawawezi kutoa mapema wakati zoezi la kuomba vyuo bado lilikuwa linaendeleaa..
Je Unajua matokeo ya vyuo yametoka lini? Tokea TCU watoe matokeo ya waliopata vyuo hadi sasa ni muda gani umepita?

Katika hili bodi hawawatendei haki watoto wa masikini watakaokosa mikopo na wasijue pakuanzia ilihali wangetoa mapema watoto wa wenye vipato vyachini wangejipanga mapema namna ya kukabiliana na changamoto ya kifedha.
 
KTN

JF-Expert Member
Jul 24, 2016
367
1,000
kuna wanafunzi wamechaguliwa fourth round, kuna wanafunzi walikuwa na supp diploma nao walipewa fursa hio ya kuomba chuo fourth round, kuna wanafunzi walikosea kujaza taarifa zao na wakapewa fursa ya kurakebisha form zao ili nao waingizwe kwenye mfumo waweze kupangiwa mikopo na haya yote yamefanyika october..kwenye hili fungu pia kuna wanafunzi wenye vigezo na ambao hawana vigezo vya kupata mikopo..sasa bodi ingetoa mapema huoni kama kuna wanafunzi humu wasingetendewa haki...

unasemahivyo kwakuwa haupo kwenye hili fungu la hawa wanafunzi, tukiwa tunafanya mambo tujitahid kuangalia na upande wa pili, tusijiangalie sisi wenyewe tu kwakua mambo yetu yameenyooka..

au mlitaka wasitoe fursa kwa wengine kuomba vyuo fourth round , au mlitaka wasitoe fursa kwa wengine kusahihisha makosa yao katika form zao ilimradi watoe majina yenu ya ambao mmepata mkopo ...

NB
Bodi wanaumiza akili sana angalau kila mwenye uhitaji apate mkopo, wenye uhitaji ni wengi sana na kumtimidhia haja kila mmoja ningumu sana hivyo basi ikitokea umepata chochote ni jambo la kumshukuru munguu.
 
BSL

Member
Dec 15, 2018
78
125
Unajitahidi sana kujenga hoja yako ili uwaaminishe wengine kuwa wako sahihi, lakini ebu fikilia tu kidogo Leo ni trashed 17,majina hayajatoka kwa kigezo cha kusubilia wengine kufNy malekebisho ni jambo uzuri sana maana kila mtanzania anao haki ,lakini kumbuka vyuo vinaanza kupokea wanachuo kuanza tarehe 26 Oct je zimebaki siku ngapi hapo ? At uje uambiwe dada yako kakosa mkopo hivyo inatakiwa kumtafutia million moja ili aweze kuripoti je kwa muda chance huo utafanikiwa kuipata kama wewe ni mtanzania Halisi mwenye kipato cha Chini ,Hapana watu wanashauri kuwa angalau kuwepo na utaratibu wa muda ili ata kama i natokea kijana kakosa basi uwepo muda wa ndugu jamaa kujichanga ,
 
Majina batch one wanatoa leo, kuhusu utaratibu wa kutoa majina mapema ni mzuri ila uta depend na mombi ya chuo yataanza kufanyika lini..

kuhusu swala la ada hakuna chuo kinalazimisha mtu kulipa ada yote ya mwaka mara moja..
ada inaweza lipwa kwa awamu mbili yaan semester ya kwanza na semester ya pili..

so unaweza lipa nusu semester ya kwanza na nusu semester ya pili na kama mtu uwezo ni mdogo hata hio nusu unaweza ilipa kwa mafungu mafungu..

wachache sana watapewa 100% mkopo na wengine watapewa asilimia kadhaa na wengine watapewa pesa ya matumizi tu.. kama unafahamu hili unaweza kujiandaa kwa kidogo ulichonacho kujazilia pale bodi ya mikopo haitakupatia.

Hii system ya kulipa ada kwa mafungu kila baada ya week kadhaa mm ndio niliitumia mpaka nikamaliza chuo..sikua na uwezo wa kulipa hata hio nusu kwa mara moja na ndio mana nilijiandaa kwa kile kidogo nilichonacho kujazilia pale bodi ya mikopo ilipokuwa haijanipatia.
 
Capslock

JF-Expert Member
May 1, 2016
1,069
2,000
Umeelewa vizuri alichoongea mtoa mada?
anachojaribu kushauri ni kwamba bodi ya mikopo iwe inatoa majibu mapema kabla tarehe za kufungua vyuo hazijakaribia ili mtu ajue kama amepata au amekosa.
Majina ya waliopangiwa mikopo awamu ya kwanza ( wale ambao maombi yao hayana makosa) yatatoka kesho kutwa oktoba 17.

Kwa hiyo usihofu,
 
MZEE RAZA

JF-Expert Member
Feb 19, 2015
2,645
2,000
Umeelewa vizuri alichoongea mtoa mada?
anachojaribu kushauri ni kwamba bodi ya mikopo iwe inatoa majibu mapema kabla tarehe za kufungua vyuo hazijakaribia ili mtu ajue kama amepata au amekosa.
Sasa kama majina yametoka tarehe 17 Oktoba na vyuo vinafunguliwa Novemba 4, bado siyo mapema hiyo? watoto wenyewe wengi wao wametuma maombi yenye mapungufu, kila siku wanaongezewa muda wafanye marekebisho lakini mpaka leo hii wapo baadhi bado hawajakamilisha kufanya marekebisho kwenye maombi yao ya mikopo. Hili nalo ni la kuwalaumu HESLB?
 
Oct 15, 2019
9
20
Nani alaumiwe?

Mkuu naona hujaelewa hoja husika, hata hao watoto wangekosea mara ngapi tunajua bodi wanafanya kazi kwa deadline.. Shida ni uharaka wa kutoa majibu ili aliyepata ajue na asiyepata ajijue ili ajipangaje.

Kumbuka sasa hivi michakato inaendeshwa kidigitali tunahitaji kuona nafasi ya teknolojia katika kuharakisha michakato, rejea TCU muda wanaotumia na NECTA kutoa matokeo ya std.7 . Kumbuka bodi huwa wakianza mapema zaidi....
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom