Bodi ya Mikopo Elimu ya Juu hamkujipanga?

hunchback

JF-Expert Member
Nov 10, 2014
658
289
Mmeanzisha mfumo mzuri sana wa wanufaika wa mikopo kuhakiki taarifa zao kwa njia ya mtandao.

Tatizo ni kuwa mtu ukitaka kuomba taarifa fupi ya malipo 'statement' haipatikani. Nilipoomba mara ya kwanza nilipata ujumbe nisubiri baada ya masaa 72, ikapita wiki. Nikajaribu kuomba tena sasa nimepewa namba ya foleni ambayo toka nimepata ni wiki sasa na foleni ya huduma haijasogea hata mtu mmoja.

Wazo ni zuri sana lakini utekelezaji naona uko duni, ni kama vile mmeweka mfumo ambao hauko tayari kutoa baadhi ya huduma.
 
Leo siku ya 4 hata Mimi naambiwa anahudumiwa mtu yuleyule mmoja na foleni haisogei, tafadhali toeni statement kwa njia ya mtandao, hilo sio suala geni sana kiufundi mabenki yanatoa hadi makampuni ya simu yanatoa
 
Hii bodi ifumuliwe upya wamefanya uhuni kwenye kuondoa penalty na value retention fee wanadai penalty na value retention fee vitaondolewa kwa wanufaika watakaomaliza mwaka huu tu na kuendelea na kumbuka ile sheria ili wagusa hata ambao walimaliza chuo kabla ya sheria kupitishwa sasa iweje value retention fee iondolewe kwa wanufaika wa mwaka huu tu,wapepingana na maelekezo ya Boss wao ambaye ni Waziri wa Elimu
 
Sheria ikiwa nzuri inaanza mwaka huo ila ikiwa mbaya inarudi nyuma.
Mkurugenzi jipu huyu
 
Sasa kama value retention fee itaanza kwa wanufaika wa mwaka huu watwambie ile sheria mbovu iliyopitishwa mwaka 2016 kwa nin imewagusa wanufaika wote hata ambao ilikuwa haiwahusu?tukisema hawafai kuendelea kuwepo ofsini tutawaonea?na ukiwaulza wanasema walipokea maelekezo hayo toka juu,
 
Yule Mkurugenzi wa bodi niliwahi kuhisi sio mtanzania ana mambo ya kijinga sana yule jamaa
 
Sasa kama value retention fee itaanza kwa wanufaika wa mwaka huu watwambie ile sheria mbovu iliyopitishwa mwaka 2016 kwa nin imewagusa wanufaika wote hata ambao ilikuwa haiwahusu?tukisema hawafai kuendelea kuwepo ofsini tutawaonea?na ukiwaulza wanasema walipokea maelekezo hayo toka juu,
kama ni kweli haya ni mambo ya ajabu sana ni kama hawataki kuitoa ila wanatafuta visingizio ilikuwa sheria ya hovyo sana ile sijui benki wangekuwa wanafanya hivi ingekuwaje
 
Ni kweli kabisa,ukiwaulza wanasema at wameelekezwa hivyo ,yaan wana jikanganya
 
Mwezi huu baada ya mapenati kufutwa watu wengi wamemaliza na kunauhitaji mkubwa wa statement physically pale ofisini kwao. Last week nilienda kuchukua barua ya kumaliza. Kuna foleni kubwa sana ya watu
 
Back
Top Bottom