Bodi ya michezo ya kubahatisha Tanzania mjitathimini, watu wanadanganywa kuwa kamali ni chanzo cha ajira na mtaji na nyinyi mpo kimya tu

Wazolee

JF-Expert Member
Sep 1, 2018
2,868
3,340
Sikuhizi Kila station ya radio utakayosikiliza imejaa matangazo ya kamali na kibaya zaidi katika matangazo yao wanashawishi watu kuwa watafute mitaji Kwa njia ya kucheza kamali na nyinyi Bodi ya michexo ya kubahatisha mnasikia ila hamuwakatazi

Pale uwanja wa maonyesho mmewaka kabisa tangazo lenu linasema

BAHATI NA SIBU SIO CHANZO CHA AJIRA WALA MTAJI ILA NI MCHEZO WA KIJISTAREHESHA KAMA MICHEZO MINGINE

Sasa mbona hamulisimamii hili mnaacha watu wanaibiwa tu Kwa kudanganywa kuwa ni chanzo Cha ajira na mtaji?
 
Yule kiongozi wa bahati nasibu kwa vile yeye ana kampuni ya kamari ndio chanzo cha kutamalaki kwa vipindi vya kamari maredioni na tv. Hana ujanja tena wa kuzuwia kwa vile naye anayo kampuni kubwa ya kamari
 
Back
Top Bottom