Bodi ya michezo ya bahati nasibu Inashughulikiaje Vijana wanaopata Uraibu?

Bodi ya michezo ya bahati nasibu Inashughulikiaje Vijana wanaopata Uraibu?

Mstahiki Mea

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2018
Posts
5,581
Reaction score
10,110
Tasnia ya michezo ya bahati nasibu imekuwa ikikuwa kwa kasi, japo hatujafikia zilipo nchi kama kenya , Uganda, south africa, Ghana na , nigeria lakini sio haba, tumekusanya zaidi ya bilion 200 kwenye mapato TRA , pamoja na faida hiyo sio ajabu kuna mahali imeacha kilio na majuto , pamoja na uraibu, je wahusika wanashughulikiaje jambo hili? Kampeni za beti kwa kiasi zinazotolewa na kampuni husika zinatosha? Je kampuni zote zinazingatia kampeni hiyo?

Je, wana dhibiti matangazo ya kiasi?
Matangazo ya igaming yapo kila mahali karibu katika kila website unayoijua , influencer radio na televisheni kote wanatangaza bila kuhamasisha Tahadhari,, na vyombo hivyo nina uhakika vinatumika na watu wote hata wale wenye umri wa miaka 18,, Je hakuna umuhimu wa kudhibiti matangazo?

Maoni yangu nini kifanyike
1. Kwanza kusiwe na uhamasishaji wa moja kwa moja kwenye matangazo

2. Kila tangazo la igaming lazima liambatane na tahadhari

3. Waangalie kama kuna uwezekano wa matangazo ya betting kurushwa muda fulani mfano usiku sana 18+

4. Kuwe na Chombo maalumu cha kushughulika na watu waliopata matatizo ya uraibu na wanashindwa kuacha.

5. Website zinazohusu vijana kama website za vyuo kuwa na kipengele cha kupata msaada kuhusu uraibu wa kamari

6. Kila kampuni ilazimishwe kuhamasisha kubeti kwa kiasi
7. Matangazo yanayomlenga mtu moja kwa moja kama kupitia Sms za simu ya dhibitiwe au ya tumwe kwa watu wenye umri wa zaidi ya miaka 18 na waliokubali kupokea matangazo ya namna hiyo.

Asanteni. Safe betting ni ile iliyodhibitiwa

Pia soma:Ushauri kwa Bahati Nasibu ya Taifa ili Kuboresha Sekta ya Betting Ili Hela Zibaki Tanzania
 
Back
Top Bottom