Bodi ya MCC yainyima Tanzania fedha za msaada

Povu linakutoka tuuuuuu aliyeshinda atangaze,kuna haja gani ya kuwa na external observer?Aliyeshinda atangazwe tuuu
 
Kama unazungumzia Tanganyika mkuu uko sawa, lakini kama unaongelea Tanzania, jua kwamba hakuna tanzania bila zanzibar, zanzibar ni sehemu ya Tz na kule uchaguzi haukuwa huru na wa haki, so automaticaly Tz nzima inaathirika ambayo ni zanzibar na Tanganyika. Kama utaendelea kubisha basi wewe utakuwa Mulugo yule wa Tanzania ni muunganiko wa tanganyika na visiwa vya zimbambwe.
 

....sikiliza wewe kiraka; kwanza wewe na serikali yako ni omba omba hilo ulielewe,kama mna jeuri ya kimasikini kuanzia leo kataeni hiyo misaada yao.Kama bado mnataka misaada yao,simple, timizeni masharti yao!
 
Tuiombee nchi yetu turudishiwe pesa za wakwepa kodi. Tukipata hizo tutakuwa hatuhitaji pesa ya mtu au nchi yeyote. Tumuombee Rais wetu Dr. Makufuli asilegeze kamba azidi kutumbua majipu ambayo yamejificha.
 
Unajua ccm siyo kwamba hawaujui ukweli wa mambo ulivyo, wanayjya sana tu ila ni kale kauroho ka madaraka na kule kusema kwamba itakuaje huku ikiwa ccm na kule cuf??? ila wasisahau yale ndo yalikua matokeo ya kupiga kura, la sivyo waneachana na mambo ya kura na kuendelea kumweka Dr, madarakani. kama walitumia demokrsaia ya kweli, basi wana jukumu la kuachia nchi ili mambo mengine yaendelee na kuepusha mambo ya Fitna, WASIONAE wapinzani wamekaa kimya wakawaona mafara!!!!! tunaona kinachoendela kule Burundi na hatutaki kitokee na hapa kwetu, Kweli busara ya baba Lowassa ni zaidi ya serikali nyiiingi sana za Africa, Mungu amweke zaidi na zaidi huyu mzee wetu. Ila kwa Zanzibar??? Huu ni mwiba tayari
 
kumbe we hujui marekani inalengo TZ kuchafuke

Tz ndo nchi inaibania marekani kufanya yake ukanda huu
 
Hivi hili suali la Tanzania kukubali kukosa misaada kwa sababu ya Zanzibar ni uzembe au ni ujinga?
 

Ndugu huna taarifa au huna maarifa?

Wewe unataka kutuaminisha kuwa US hawaujui Muungano huu wa Tanganyika na Zanzibar?

Tafuta uzi humu JF utajionea vipi US walihusika kwa 110% kutuundia huu Muungano wa kiinimacho.

Ukishindwa kujipatia taarifa hizo, rudi tukusaidie kukuwekea viungo(links) ujiridhishe. US wanaujua na kuuelewa Muungano huu kuliko sisi wadanganyika.
Pia US wanajua kuwa CUF imekuwa inashinda uchaguzi huko Zanzibar tokea 1995. Ni sasa tu ndio wameamua kuwa yametosha.

Sio US tu hata EU nao watakunjua makucha yao karibuni.

Si jambo jema kwa CCM kubaka demokrasia kwa visingizio hivi:
Hili la kushinikizana si haki.Na wamarekani na jumuiya ya kimataifa ni vizuri wakawajua CUF vizuri kama hawawajui shauri yao.

Kwa nini CCM inaitisha uchaguzi mkuu kama haitaki kuachia madaraka inaposhindwa?

Kama wapiga kura, wananchi wamekichagua CUF huko Zanzibar kuongoza serikali kwa nini wachache waibuke na visingizio vya kijinga. Tanzania si mali ya CCM wala Zanzibar si mali ya CCM. Wenye mali ni watanzania na wazanzibari na maamuzi yao kupitia kisanduku cha kura ni lazima yaheshimiwe.

Msitake kuharibu amani na utulivu wa nchi hii.
 
Soko kubwa la dhahabu liko wapi????!!!!

I BELIEVE LIKO EUROPE, NA PROCESSOR WAKUBWA WA RAW MATERIALS ZETU MAJORITY NI EUROPE PIA AMERICA, TATIZO TUNAKUWA MASHABIKI TU BILA KUYAELEWA MAMBO, NCHI HII BADO INASUMBUKA NA KIPINDUPINDU 53 Yrs AFTER UHURU UKU WENGINE WANADAI TUJITEGEMEE, TUSISAHAU RUSIA KASALIMU AMRI KWA AMERICA, NADHANI UWE TUNASOMA PIA KUSIKILIZA VYOMBO VYA HABARI VIZURI... SISI KUJITEGEMEA KINADHARIA SAWA ILA KWA VITENDO BADO SANA.
KICHEKESHO.
 
Tuiombee nchi yetu turudishiwe pesa za wakwepa kodi. Tukipata hizo tutakuwa hatuhitaji pesa ya mtu au nchi yeyote. Tumuombee Rais wetu Dr. Makufuli asilegeze kamba azidi kutumbua majipu ambayo yamejificha.

Nafikiri ni vizuri pia kuondoa misamaha yote ya kodi toka kwa wawekezaji wa kutoka nchi za nje sababu sehemu ya faida wanazopata kwa uwekezaji wao Tanzania ndizo huzitumia kutupa misaada.Ajabu sisi tunapowapa nafasi ya uwekezaji nchini kwetu huwa hatuwapi masharti ya kisiasa lakini wao wakishavuna pesa kutoa msaada kidogo toka faida wanayopata wanatupa masharti kibao ya kisiasa.

Bill Gates anauza makomputa na masoftware kibao Tanzania.Anatengeneza pesa nyingi mno na makampuni mengi ya marekani yamewekeza Tanzania bila kupewa masharti ya Kisiasa na watanzania.

Wema wetu ndio wanatulipa kwa kutuingilia mambo ya siasa.

Wawekezaji hawana huruma kwetu naomba serikali iliyopo tufanye biashara nao tu.Wakitaka vitalu vya gesi au madini au ardhi kwanza walipe pesa za kununua na kufidia halafu watoe hisa kwa wenye wenye maeneo zisizopungua 40% wakikataa watuachia vitalu,madini na ardhi yetu.Tuanze kuwa wakali na sisi na kile tulichonacho kama wao wanavyokuwa wakali kwetu kwa vile walivyonavyo.
 
Kumbe ni swala la kiimani....basi sawa....

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…