Bodaboda yazua balaa kwa wapendanao!

Bodaboda yazua balaa kwa wapendanao!

Herbalist Dr MziziMkavu

Platinum Member
Joined
Feb 3, 2009
Posts
43,114
Reaction score
34,955
attachment.php



Stori: Dustan Shekidele, Morogoro

MIAKA ya nyuma watu walishuhudia akina mama wakipigana vijembe kwa maneno yaliyokuwa kwenye khanga lakini sasa hali hiyo imejitokeza kwa wanaume ambao hutumia pikipiki kuwafumbia maneno ya mafumbo watu waliokorofishana nao kwa kuyaandika katika mipira ya ‘madigadi’.

<center style="margin: 0px; padding: 0px; border: 0px; outline: 0px; vertical-align: baseline; background-color: transparent;"></center>
attachment.php




Gazeti hili hivi karibuni likiwa kwenye duka la kuuza pikipiki lililopo Mtaa wa Mindu barabara ya kueleka Faya Manispaa ya Morogoro, lilishuhudia pikipiki nyingi zikiwa zimeandikwa ujumbe tofauti.

Kijana mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Sule Manga akiwa juu ya pikipiki yake iliyoandikwa maneno yanayosomeka: “Usijisifu una mimba, msifu aliyekutia mimba hiyo” alipoulizwa sababu ya kuandika hivyo alifunguka:
“Pikipiki hii nimeinunua hivi karibuni na hili pepe nililichora tangu jana nikiwa na sababu maalumu, nilikuwa na demu wangu ambaye nilimtia mimba, juzikati kaniaga anakwenda kwao Tanga, chaajabu aliporudi amekata mawasiliano na mimi huku akijisifu kwa watu kwamba ana mimba bila kunisifu mimi niliyempa mimba hiyo,” alisema Manga na kuongeza:
“Nikimpigia simu hapokei, hivyo kuanzia juzi niliamua kuachana naye kwa sasa naelekea nyumbani kwao na pikipiki hii, nikifika naipaki jirani na nyumba yao kwa lengo la kutaka yeye na familia yake akiwemo mama yake mzazi wasome meseji hii…nasikia kambambikia mtu mwingine mimba yangu,” alisema.
Hata hivyo, hakuwa tayari kumtaja mwanamke huyo anayedai kuwa na mimba yake. Pikipiki nyingi mjini hapa zimeandikwa maneno ya mafumbo kama yanayoandikwa kwenye khanga.

MABODABODA KAZI YAKE KUBWA KUWATUKANA WAKE ZA WATU AHHH KASHESHE KWELI
 

Attachments

  • bodaboda.jpg
    bodaboda.jpg
    59.1 KB · Views: 760
  • pikipiki001.jpg
    pikipiki001.jpg
    92.4 KB · Views: 672
bodaman hiyo mimba ana uhakika gani kama ni yake? Aache kujifagilia huenda huyo demu yuko sahihi ndio maana anampiga chenga.
 
bodaman hiyo mimba ana uhakika gani kama ni yake? Aache kujifagilia huenda huyo demu yuko sahihi ndio maana anampiga chenga.

Sifa kwa aliyetia hiyo mimba kama ni yeye au sio yeye bali sifa ziende kwa mwenye mchango wa gene.
 
Tangazo la biashara tu hilo...kwa ujumbe huo lazima atakua maarufu kijiweni na kujizolea wateja zaidi...
 
bodaman hiyo mimba ana uhakika gani kama ni yake? Aache kujifagilia huenda huyo demu yuko sahihi ndio maana anampiga chenga.

Whatever, aliyetia mimba ni wa kifisiwa, be it mwenye mpenzi ama mwizi wa penzi!
 
Haisaidii sana haswa kwa mwanaume,imezoleka vijembe ni vya wanawake japo si vizuri,wananawake wakipeana vijembe jamii inawachukulia poa,ila kwa mwanaume inatia aibu.
 
Unasifiwa vipi....hongera kwa kutia mimba? :nono: :nono:
 
Kuna wakaka wataanza kuvalishwa mitandio na vitenge siku si nyingi......
 
Back
Top Bottom