Kazi za polisi wa barabarani ni pamoja ni kuzuia bodaboda wasipite njia ya mwendokasi hawakua na haja ya kumsubiri Rais aseme. Hakukuwa na upungufu wa sheria katika kuhakikisha kuwa bodaboda hawapi kwenye njia hizo.Uhakika ni kwamba bodaboda hatakiwi kupita njia ya mwendokasi.
Hakuwa na haja ya kumsikiliza Rais zaidi ya kufuata sheria.
Unaruhusiwa kukatisha upande wapili katika sehemu rasmi iliyowekwa kama vile kwenye zebra, ila unashuka na kukokota pikipikiyako ukisha vuka unapanda, safari inaendelea na hukamatwi.Polisi wameongezewa kula ukiingia hata kwa kukatisha itabidi uchague ung'olewe tairi au utoe buku 10
KweliUhakika ni kwamba bodaboda hatakiwi kupita njia ya mwendokasi.
Hakuwa na haja ya kumsikiliza Rais zaidi ya kufuata sheria.
Ili askari wa barabarani wazuie bodaboda wasiingie mwendokasi road inabidi wawe kama 10,000 kuanzia mbezi hadi kivukoni.Kazi za polisi wa barabarani ni pamoja ni kuzuia bodaboda wasipite njia ya mwendokasi hawakua na haja ya kumsubiri Rais aseme. Hakukuwa na upungufu wa sheria katika kuhakikisha kuwa bodaboda hawapi kwenye njia hizo.
Hasa kariakoo kama ndo njia yao vileHii sheria haifanyi kazi mbona boda zimejaa tu huku mwendokas!
isitoshe hili lilijulikana kabla hata njia zenyewe hazijazinduliwa. visingizio kwamba hawasikilizi au hawana redio/tv ni kiduchi sana. mbona mengine ya maandamano yanawafikia? wenzao waliogongwa kwa makosa ya kupitisha tukutuku zao hapo hawakupewa maonyo? yule abiria aliyeburutwa uvunguni mwa basi si aliponzwa na dereva asiyejua au aliyekaidi sheria? iweje leo tuendekeze na kulea makosa yatakayogharimu maisha ya wenzetu na vilema vya maisha ati ni kuogoapa sera ya 'wapiga kura' kwani wanaogongwa na kufa/kulemaa sio wapiga kura? tuweke itikadi kando tukemee na kupongeza inapobidi. mizaha na michezo michezo kwa uhai wa binadamu tuuepuke kabisa.Uhakika ni kwamba bodaboda hatakiwi kupita njia ya mwendokasi.
Hakuwa na haja ya kumsikiliza Rais zaidi ya kufuata sheria.
mwenye njaa tangu lini akatii sheria?, tuangalie na kulaumu kule tulipojikwaa sio tulikoangukia. Unapoongelea suala la bodaboda na machinga lazima uwe makini sana.Yani kuwatetea bodaboda unatakiwa labda ujitoe fahamu, maana siku zote hawa ni watu wa kuvunja sheria tu. Ni mara ngapi imetangazwa wasipite kwenye barabara ya mwendo kasi lakini wanapuuza tu! Hiyo kauli ya Mheshimiwa Rais alikuwa anatilia mkazo tu. Hao bodaboda hata wangewekewa matangazo kila kona bado hawawezi badilika. Hivyo inahitajika nguvu ya ziada kuwafanya wabadilike ili wafuate sheria.
We bwana sijui wataka nn.. Karne hii ya 21 mwaka wa 2017.. Kweli utasingizia hujapata taarifa.??Nijuavyo mimi bodaboda wengi hawana TV, ving'amuzi wala muda wa kuangalia TV au kusikiliza redio. Muda mwingi wanasikiliza muziki kwenye flash zao kwenye pikipiki ili kujaribu kuvutia wateja wapande bodaboda zao. Tangazo la rais kuhusu kung'oa matairi ya bodaboda zao huenda halikusikika kwao, hivyo sio vizuri watendaji kumchonganisha Rais na wananchi wake kwa kushindwa kutafsiri kauli zake.
Mimi nilidhani kuwa baada ya mh. Rais kutamka vile nyie watendaji mngejiongeza kwa kutoa elimu zaidi kwa waendesha bodaboda kuhusu utekelezaji wa kauli ya Rais na ubaya wa kupita kwenye barabara za UDART kabla ya kuanza kung'oa tairi za bodaboda fasta fasta huku mkipaza sauti kuwa mnatekeleza agizo la Rais.
Kusudio kuu la Rais pale halikuwa kung'oa tairi za bodaboda bali alitaka watendaji wakuu kuepusha ajali za barabarani kwa nguvu zote kwa mujibu wa sheria na kanuni zilizoko kwenye makablasha yetu. Kung'oa tairi la mkosaji ni kanuni au sheria namba gani ya usalama barabarani?
Ningekuwa mimi ndio mh. Magufuli ningewatumbua waliong'oa tairi za bodaboda za wapiga kura wake, maana wameshindwa kazi kwa kushindwa kujiongeza, kutafsiri na kuzuia ajali za barabarani kwa kutumia sheria na kanuni zilizopo za kuzuia makosa ya barabarani. over!