Bodaboda vinara ongezeko mimba za utotoni

Bodaboda vinara ongezeko mimba za utotoni

FikraPevu

JF-Expert Member
Joined
Jan 2, 2010
Posts
304
Reaction score
236
Kwa mujibu wa tafiti zilizofanywa hivi karibuni, waendesha bodaboda wanachangia asilimia 13 ya mimba za utotoni nchini.

Matumizi ya bodaboda, ama pikipiki kwaajili ya biashara, yameongezeka sana nchini Tanzania hasa pale ambapo ni ngumu kupata usafiri mwingine. Umaarufu wake unasababishwa na upatikanaji mgumu wa usafiri pamoja na bei nafuu za pikipiki; na huwa zinaendeshwa na vijana wadogo waliotoka kumaliza tu elimu ya sekondari.

Kwa mujibu wa utafiti huo, wasichana wadogo, hasa wale wa vijijini, wako katika mazingira hatarishi zaidi kushawishika kingono kwasababu inawabidi kusafiri umbali mrefu kwenda shule. Gazeti la Financial Times linasema, baadhi ya wasichana huishi umbali wa hadi kilometa 15 kutoka shuleni, hivyo huwalazimu kupanda bodaboda badala za kutembea umbali huo.

Kwakuwa hawana fedha za kutosha kuwalipa waendesha bodaboda hao, huishia kulala nao kama njia ya malipo. Wanapopata ujauzito kwa jinsi hii, huishia kufukuzwa shuleni.

1_hfK1g5NFwkQzu0cc6UwCaw-1.jpeg




Swali hapa ni je, mimba ngapi za utotoni ambazo zinasababishwa na waendesha bodaboda nchini Tanzania?

PesaCheck imefanya uchunguzi na kubaini ya kwamba, madai ya kuwa waendesha bodaboda wanachangia ongezeko la mimba za utotoni Tanzania ni kweli kwa kiasi kikubwa kwa sababu zifuatazo:

Utafiti wa Taifa kuhusu Vichocheo na Madhara ya Ndoa za Utotoni nchini Tanzania, unafafanua kwamba wasichana kutoka kaya masikini ni kundi hatarishi kwasababu ya hali yao ya kiuchumi. Kukosa mahitaji yao ya msingi, kama kuweza kulipia usafiri, kunawafanya iwe rahisi kunyanyaswa kingono.

Ni ngumu kujua idadi kamili ya mimba zilizosababishwa na waendesha bodaboda. Lakini, kilicho bayana ni kwamba wasichana waishio vijijini nchini Tanzania ni kundi hatarishi la kunyanyaswa kingono na watu wanaohusika na usafiri sehemu mbalimbali nchini.

Zaidi, soma hapa => Waendesha bodaboda wanachangia asilimia 13 ya mimba za utotoni nchini | FikraPevu
 
Back
Top Bottom