Bodaboda, Umachinga ni upotevu wa nguvu kazi na ipo siku tutajuta

MURUSI

JF-Expert Member
Jun 25, 2013
4,496
8,731
Kumuelewa Lema unahitaji kuwa na akili kubwa sana, Shida ya hii nchi swala kuambiana ukweli ni tatizo sana, Leo hii kuna uharibifu mkubwa mno wa Mazingira ila hakuna hata kiongozi mmoja ana dhubutu kuamka na kukemea zaidi ya kukemea kwa mafumbo, kisa asiwaudhi wapiga kura, ndio maana vyanzo vya maji vinavamiwa mapori yanavamiwa na hao jawaguswi kisa ni wapiga kura.

Nini sustainability ya Bodaboda kwa baadae? Unazani 10 years from now hali itakuwaje?

Niliona bandiko moja Serikali ya Nigeria ikijuta sana kuto kudhibiti Bodaboda mapema sana na kuingiza siasa kwenye uhalisia, ndio kisa wakipigwa marufuku kuingia katikayi ya majiji makubwa.

Leo hii miaka 20 ijayo unadhani kutakuwaje mjini? Gari zitatembea au zitapack na ziwaachie bodaboda ndio watembeee mjini?angalia tu tu swala la bajaji.

Vijana wanakimbia vijijini tena wanauza hadi mashamba na kuja mjini kununua pikipiki za kufanya Bodaboda hii ni akili? na hakuna udhibiti hadi sasa wa Bodaboda wanazidi kuongezeka na wanaachwa kwa sababu ni wapiga kura.

Nguvu kazi Vijijini kwa sasa haipo tena wamebakia wazeee tu vijana wako mjini wanaendesha bodaboda na sisi tunashangilia tunaona ni sahihi kabisa kisa hawa ni wapiga kura wetu.

Serikali inakwepa jukumu la kuboresha maisha ya raia wake na kuwapatia ajira na imejikita kuona bodaboda na umachinga ni ajira.

Ipo siku tutajuta na hii ishu ya Bodaboda na itakuwa too late sana.
 
Wapo wamachinga wanalaza hesabu ya kueleweka . Labda hao bodaboda, ndiyo kidogo nina wasiwasi.

Ingawa nao wana mchango mkubwa sana kwenye kurahisisha usafiri kutoka eneo moja, kwenda lingine.
 
Kumuelewa Lema unahitaji kuwa na akili kubwa sana, Shida ya hii nchi swala kuambiana ukweli ni tatizo sana, Leo hii kuna uharibifu mkubwa mno wa Mazingira...
Kutajuta kikundi cha watu au mtu?
 
Ndio maana kwa sasa uzalishaji ni mdogo sana ma mahitaji ni makubwa KULIKO uhalisia

Unga umepanda bei na mchele unapanda bei kipindi Cha mavumo wakati ilitakiwa kuwa vice versa.....

Vijana wote wapo mjini WANAPIGA boda boda hawazakishi tena

Vijana wengi ni watu WA kulenga hapo karume.

Kilo ya sembe ni 2,000 na Dona ni 1,800

Kwanza HAWA boda boda ni shida tupu hapa kariakoo usipokuwa makini unaweza kuja mjini mzima ,ila ukarudishwa nyumban kilema

Vijana wanaendesha hovyo boda boda Wala hawatii Sheria

Wanaharaka wakati wowote.

HAWA ni vijana hawana chakupoteza katika maisha Yao ,japo wachache wanajitambua

Kama hakuna sera ya kuzuia hizi pikipiki kuingia nchini sijui tutakuwa nchi ya kituko kiasi gani baada ya miaka kitatu.

Labda tujenge moi nyingine Kila wilaya hapa dar mana Ile ya muhimbili haitotosha.
 
Bodaboda wamefungua nchi, zamani hadi ufike kijijini unamaliza wiki, siku hizi ni siku moja tu.

Ilikuwa unapanda treni siku ya tatu ndo unafika mjini unalala stand unachukua basi kesho, ukifika center unalala kwa ndugu Ili kuandaa miguu, kesho kutwa alfajiri unaanza kukanyaga mwendo jioni mnalala kijiji cha jirani kesho yake mnakanyaga tena ndo mfike kwenu.

Siku hizi ni masaa tu,
 
Kilimo kikiboreshwa kutapunguza idadi ya machinga na bodaboda kuzagaa mijini
 
Kwanza HAWA boda boda ni shida tupu hapa kariakoo usipokuwa makini unaweza kuja mjini mzima ,ila ukarudishwa nyumban kilema

Vijana wanaendesha hovyo boda boda Wala hawatii Sheria
Sasa umkute amepakia mzigo wa vitambaa
Yaani ni kuzidi hata pickup halfu polisi jamii 😇😇😇 wanaona wanatupiwa buku mbili maisha yanaenda
 
Hakuna atakayejuta kama taifa ispokuwa mtu mmoja mmoja kwa kushindwa kukamilisha malengo binafsi.

Taifa haliwezi kuundwa na kundi moja. Matabaka ni viambajenzi vya taifa. Matabaka yapo kila taifa, si Tanzania, wala Afrika pekee. Huwezi kumaliza matabaka katika jamii.

Uwepo wa matabaki katika nyanja za kiuchumi, kijamii na kisiasa ni ishara kwamba taifa lipo hai na litaendelea kuwa hai.

Ni wasiofahamu ulazima wa matabaka katika maendeleo ya taifa ndio watakao lalamika juu ya uwepo wa Bodaboda, mamanitilie, michezo ya bahati naibu, wamachinga na vicoba katika jamii.

Hakuna jamii isiyokuwa na matabaka. Na kuna makundi mengine katika jamii ni lazima ya wepo. Yasipokuwepo tutayaunda kwa lengo ya kulinda mizania ya ustahamilivu wa jamii.
 
Kumuelewa Lema unahitaji kuwa na akili kubwa sana, Shida ya hii nchi swala kuambiana ukweli ni tatizo sana, Leo hii kuna uharibifu mkubwa mno wa Mazingira...
Mtu anapata elfu kumi kwa siku baada ya kukamilisha elfu ya tajiri. Anakula na kuvaa kwa hela hiyo na anaanzisha na kufuga familia.

Mwaka ukiisha, pikipiki inakuwa yake. Unataka kazi hiyo ipigwe marufuku ili iweje!? Barabara hazipo kwa ajili ya magari tu.

Ikiwa bodaboda hazihitajiki, zisingekuwa nyingi hivyo. Kazi yako siyo ya maana kwa wengine. Usidharau kazi za watu. Kama kulima, nenda wewe huko kijijini ukalime.
 
Kama una miguu yote miwili bodaboda ikuvagae upelekwe moi huko utatulie hata mwezi kwanza....

Labda utapata akili.
 
Kumuelewa Lema unahitaji kuwa na akili kubwa sana, Shida ya hii nchi swala kuambiana ukweli ni tatizo sana, Leo hii kuna uharibifu mkubwa mno wa Mazingira...
Kuna huyu bodaboda mluguru ametoa maelezo jinsi bodaboda inavyompa kipato!!👇👇

Screenshot_20230306-141800.png
 
Back
Top Bottom