GE2025 Bodaboda na Machinga waahidi kutokuwa chanzo cha kuvunja Amani

GE2025 Bodaboda na Machinga waahidi kutokuwa chanzo cha kuvunja Amani

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Wild Flower

JF-Expert Member
Joined
Jul 20, 2023
Posts
844
Reaction score
1,604

Makundi ya waendesha bodaboda na wamachinga yamezunguka katika mitaa kadhaa ya jiji la Dar es Salaam ikiwemo Posta, Kisutu, Kivukoni, Kariakoo, Karume, na Buguruni, yakihamasisha wananchi kulinda amani na kujitokeza kupiga kura siku ya tarehe 29 Oktoba. Akizungumza na waandishi wa habari, Kiongozi wa waendesha bodaboda Ilala, Abdul Kimaro, amewataka vijana wenzake kutokubali kurubuniwa kufanya vurugu na badala yake kutumia haki yao ya kidemokrasia kwa kupiga kura kwa amani.

Kwa upande wao, makundi ya bodaboda na wamachinga wameonesha kukubali elimu hiyo, huku baadhi yao wakiapa kujitokeza kupiga kura na kusisitiza kuwa hawatashiriki katika vurugu za aina yoyote. Viongozi wengine wa wamachinga na wajasiriamali wadogo (mama na baba lishe) na bodaboda nao wamejitokeza kuunga mkono kampeni hiyo ya amani, wakisisitiza kuwa uchaguzi ni fursa ya maendeleo na siyo sababu ya migogoro.
 
Hawana akili hao ma Afsa usafirishaji, na ma Afsa lishe.
😂😂😂😂😂😂
 
Haya mambo tunayachukulia jumla jumla kama watu wenye mtindio wa Ubongo....

  1. Moja bodaboda na machinga hawana sauti moja
  2. Mbili hakuna Mtanzania atakayekwambia yeye ni chanzo cha kuvunja amani wala hakuna mtu ambaye hapendi Amani...
Sasa definition ya kuvunja Amani ni ipi ? Sababu madai ya watu wengi ambao ni walipa Kodi kwangu mimi naona ni ya maana kabisa wala sio ya kuvunja Amani na kwa kutokuwapa watu haya nadhani Serikali ndio inataka kuwa chanzo cha kuvunja Amani:

 
Back
Top Bottom