Bodaboda asababisha kifo cha mtoto barabara ya mwendokasi

Chachu Ombara

JF-Expert Member
Dec 11, 2012
6,042
10,787
Ajali hii imetokea eneo la Shekilango Jijini Dar es salaam baada ya bodaboda mzembe kutaka kupita gari lililokuwa njia ya kawaida lakini mpuuzi huyo wa bodaboda zoezi hilo lilimshinda na kuangusha pikipiki chini. Alikuwa amempakia mama na mwana ambapo mwana aliangukia njia ya mwendokasi na kugongwa na basi la mwendokasi lililokuwa kwenye njia yake.

Mpuuzi huyo wa bodaboda mimi binafsi namlaani, na apatwe na mabaya maisha yake yote.

Screenshot from 2016-05-19 18:00:26.png
 
Watu wote wanaothibitika kusababisha ajali katika barabara maalum za mabasi ya haraka wanapaswa kuozea jela...
 
Hawa wavuta bangi lazima wadhitiwe mapema. Wameambiwa hiyo njia siyo ya vyombo vingine vya moto zaidi ya ma bus husika lakini hawasikii.
 
Bado Watu Ni Wagumu
Katazo Limetolewa Ni Marufuku Kupita Njia Ya Hayo Mabasi Wao Hawasikii!!
 
Boda boda wengi ni wavuta bange..hawajui sheria za barabara...
Yaani hapo Shekilango ni majanga. Boda wanapitaga wrong mbele ya polisi na hawakamatwi. Mfano: Gari zinaoenda mjini hupita kushoto na yanayotoka kulia. Wao boda hupita kulia kwenda mjini. Tabia hii huhatarisha maisha ya watembea kwa miguu na vyombo vingine vya usafiri. Bodaboda wanajitanua service road za UDART japo zimechorwa baiskeli na watembea kwa miguu. Naomba waajiriwe Vijana wa kusimamia sheria barabarani wakae kila baada ya nusu kilometres ya barabara kuu. Mshahara wao utalipwa toka kwenye faini watakayolipishwa Wavunja sheria za barabara. Mbona huko USA Na Ulaya sheria za barabarani hufuatwa? Boda Na Bajaj ni kero ya mjini inayotakiwa kutatuliwa. Vyombo vya moto vifuaye sheria.
 
Ingekuwa amri yangu ningezifuta bodaboda na kutoa leseni upya kwa utaratibu mkali, mgumu na wenye masharti mazito. Pole kwa mama alaiyepotezewa uhai wa mtoto kwa mpuuzi aliyekuwa akiwahi 1000 bila kujali uhai wa abiria.
 
Alafu akina mama jamani nawasihi, ogopeni kidogo kupanda hizi bodaboda, km walikuwa wanapita morogoro road, walikuwa wanaenda wapi wasipande basi, au bajaji? Bodaboda panda ikupeleke vinjia ambavyo hamna mabasi, sioni sababu ya kupanda pikipiki tena na mtoto juu, mnapita barabara hatari km morogoro, kwani kutikana na wembamba wake, ishakuwa hatari na lazima upite kwa makini, yaani akina mama huwa wanajiachia sana wakiwa kwenye bodaboda, samahani lakini km nitaeleweka vibaya.
 
Alafu akina mama jamani nawasihi, ogopeni kidogo kupanda hizi bodaboda, km walikuwa wanapita morogoro road, walikuwa wanaenda wapi wasipande basi, au bajaji? Bodaboda panda ikupeleke vinjia ambavyo hamna mabasi, sioni sababu ya kupanda pikipiki tena na mtoto juu, mnapita barabara hatari km morogoro, kwani kutikana na wembamba wake, ishakuwa hatari na lazima upite kwa makini, yaani akina mama huwa wanajiachia sana wakiwa kwenye bodaboda, samahani lakini km nitaeleweka vibaya.
Hata wasichana, kuna visichana vinapenda sana boda boda na havivai hata helmet..
 
Dada zanguni acheni kupanda bodaboda tena mkiwa mmepanda na watoto!mbona daladala zipo?inakiwaje unapanda bodaboda ukiwa na mtoto mdogo!huku ni kuweka rehani maisha. Tena wengi wao huwa wame relux utafikiri wamepanda taxi. Anyway poleni wafiwa!
 
Ombi
Hata wasichana, kuna visichana vinapenda sana boda boda na havivai hata helmet..
Naomba Serikali itengeneze ajira za kusimamia sheria barabarani hasa za mjini kipekee Dar es salaam. Polisi hawatoshi kabisa, by the time anadeal Na mvunja sheria mmoja makosa hayohayo yanaendelea nyuma au mbele yake. Kuna Vijana wana nguvu hawana ajira wanaweza kufanya hii kazi. Sisi tunaopita Moro Road daily tunaona jinsi barabara zinavyotumika isivyo. Majiko ya kupika vitumbua na supu asubuhi watu wajipikia barabarani kwa raha zao na kusave hapo hapo. DART wanashindwa kufagia au kukwangua tope lililoganda kwenye paving blocks na lami ya njia za Huduma. Uchafu kila kona. Toeni ajira muone kama DART haijawa kama ya Developed Countries.
 
Back
Top Bottom