Bobali: Elimu isimamiwe na Wizara Moja

ACT Wazalendo

JF-Expert Member
May 5, 2014
617
1,541
ACT WAZALENDO ELIMU ISIMAMIWE NA WIZARA MOJA.

Waziri Kivuli wa Elimu, Sayansi na Teknolojia amesema Hamidu Bobali ameitaka Serikali kuhakikisha sekta ya Elimu inasimamiwa na Wizara moja ili kuondoa mgongano katika usimamizi, utekelezaji na uwajibikaji. Kwa sasa Sekta ya Elimu inasimamiwa na Wizara tatu Wizara ya TAMISEMI, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia na kwa sehemu ndogo Wizara ya Maendeleo ya jamiii, Jinsia na Makundi Maalumu.

Anasema katika utekelezaji wa sera ya elimu kumekuwa na muingiliano katika utawala wa elimu, ujenzi wa miundombinu na utoaji wa miongozo mbalimbali ya uendeshaji wa Elimu.

Bobali ameshauri Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia iachiwe majukumu yote yanayohusu masuala ya elimu kuanzia ngazi ya awali mpaka chuo kikuu ili kuwaibika ipasavyo kuanzia, utangaji wa sera, utekelezaji na usimamizi.

Waziri Kivuli wa Elimu, Sayansi na Teknolojia
Hamidu Bobali
 
ACT huwa wana hoja nzito sana tofauti kabisa na genge la Mbowe. Kweli hata mimi naona kama vile TAMISEMI kusimamia elimu huku wizara ya elimu ikiwepo haiko sawa.
 
Back
Top Bottom