Bob Marley ni mmoja ya wasanii mashuhuri duniani waliopata kuwa na watoto wengi

USSR

JF-Expert Member
Jul 15, 2015
9,896
22,666
Gwiji wa reggae duniani hayati Robert Nesta Marley (Bob) ni moja kati ya wasanii mashuhuri duniani waliopata kuwa na watoto wengi waliowazaa na wanawake tofauti-tofauti.

Katika maisha yake Bob alijaaliwa kuwa na familia ya watoto 11 aliowazaa na wanawake 7 tofauti huku wawili kati ya hao akiwa amewaasili (adoption) na mkewe Bi Rita Marley.

Pamoja na watoto hao, Bob anaelezwa pia kuwa na watoto wengine wawili ambao kwa sababu zisizowekwa wazi, wameshindwa kuingizwa rasmi kama sehemu ya familia.

Moja kati ya vitu vinavyosisimua sana ni namna Bob alivyowazaa watoto hao kwa kuwapishanisha umri kidogo sana, huku sehemu kubwa ya wanae wakirithi kipaji chake cha muziki.

Ifuatayo ni orodha ya watoto hao:

1. ZIGGY MARLEY.
Mzaliwa wa October 17, 1968 kutoka kwenye tumbo la mkewe Bi Rita Marley.

2. STEPHEN MARLEY
Mzaliwa wa April 20, 1972 kutoka kwenye tumbo la mkewe Bi Rita Marley.

3. ROHAN MARLEY
Mzaliwa wa May 19, 1972 kutoka kwenye tumbo la Bi Janet Hunt.

4. ROBERT MARLEY
Mzaliwa wa May 16, 1972 kutoka kwenye tumbo la Bi Pat Williams.

5. JULIAN MARLEY
Mzaliwa wa June 04, 1975 kutoka kwenye tumbo la Bi Lucy Pounder.

6. KY-MANI MARLEY
Mzaliwa wa February 26, 1976 kutoka kwenye tumbo la bingwa wa zamani wa Table Tennis, Bi Anita Belnavis.

7. DAMIAN MARLEY
Mzaliwa wa July 21, 1978 kutoka kwenye tumbo la Miss World 1976, Bi Cindy Breakspeare.

8. KAREN MARLEY
Mzaliwa wa February 26, 1973 kutoka kwenye tumbo la Bi Janet Bowan.

9. CEDELLA MARLEY
Mzaliwa wa August 23, 1967 kutoka kwenye tumbo la mkewe, Bi Rita Marley.

10. SHARON MARLEY
Mzaliwa wa November 23, 1964 ambaye Mke wa Bob, Bi Rita Marley alimuasili.

11. STEPHANIE MARLEY
Mzaliwa wa August 17, 1974 ambaye Bob na Mkewe Rita walimuasili.

12. IMANI CAROLE MARLEY
Mzaliwa wa May 22, 1963 kutoka kwenye tumbo la Bi Cheryl Murray ambaye hakuingizwa kwenye familia.

13. MAKEDA MARLEY
Mzaliwa wa May 30, 1981 (siku 19 baada ya Bob kufariki) kutoka katika tumbo la Bi Yvette Crichton ambaye naye hakuingizwa kwenye familia.

Pamoja na Bob kuwa na makundi matatu ya watoto katika familia yake: Watoto wa Mkewe/Watoto wa Nje ya Ndoa/ Watoto wa kuasiliwa (adoptions)/ bado familia hiyo inaishi kwa upendo mkubwa kiasi ambacho unaweza kuhisi wote wamelala kwenye tumbo moja.

Chuma kimekufa na miaka 36 tu. Kwa jinsi mtiririko ulivyokuwa unaenda, sijui kingefika miaka 50 ingekuwaje.!

#Balozi......

USSR
 
Yaan sipendi kufyatua fyatua tu hovyo lakini kuzuia uzazi napo ni kazi ngumu mno na mbususu kuzichakaza nyama nyama napenda mno, sjui nifanyeje

Kuna wakati natamani hata kufunga mirija ya manii
 
Niliona documentary moja inaelezea kwamba huyu mkewe kapitia kwenye maumivu sana, maana wanasema ilifikia kipindi mjoba alifungulia mbwa kabisa. Yaani mkewe kalala chumba hiki yeye huku chumba cha pili anakatika.
 
Ningependa financially huyu jamaa alikufa akiwa yuko vizuri au umaarufu tu wa jina ila mfukoni hakuna kitu maana kuna documentary niliangalia inaonesha makazi aliyokuwa akiishi ni ki culture zaidi ila kama vile pako duni sana
 
Franco Luambo naye kaacha watoto 17 aliozaa na wanawake tofauti tofauti.

Ila jamaa hakutoka na watoto pekee, ilibidi achomoke na ngwengwe ambayo ilimpeleka kaburini.
 
Back
Top Bottom