Bob Chacha Wangwe: Tunaenda wapi kutoka kwa ma-DED?

Bob Chacha Wangwe: Tunaenda wapi kutoka kwa ma-DED?

comte

JF-Expert Member
Joined
Dec 11, 2011
Posts
9,014
Reaction score
6,834
Leo asubuhi Bob Chacha WANGE ameshiriki kipindi cha gumzo cha BBC. sehemu ya mazungumzo yao:-
Mtangazaji:- mtazamo wenu hamuwataki MADED wasimamie uchaguzi; je ni nani wawekwe badala yao na itumike njia ipi kuwapata?
Wangwe:- sisi lengo letu ni kupata katiba mpya.... mtandazaji anamkatiza
Mtangazaji:- Swali langu nataka utusaidie namna ya kuwapata watu wa kufanya kazi ambayo kwa sasa wanaifanya MADED
Wangwe: Tunao ushaidi na tumeutoa mahakama MADED ni makada wa CCM

Nani anaweza kumsaidia Wangwe kujibu swali hili
 
Wawe waajiriwa wa NEC kwa specific time, mfano miezi 6 au mwaka ambapo kazi itatangazwa na sifa za mwombaji kuonyeshwa kwenye tangazo. Sifa za mwombaji among others lazima zizingatie katiba. Kabla ya kuajiriwa, majina yatangazwe gazetini ili kama mtu ana zuio la haki kwa mwajiriwa anayekusudiwa, mtu huyo aweze kueleza na hasa kama mtu anayetakiwa kuajiriwa ni kada wa chama fulani.
 
1. Njia ya kuwapata ni kwamba watu wenye sifa waombe hizo nafasi kwenye Tume ya Uchaguzi, mchakato uwe wazi.

2. Makada watawekewa mapingamizi na watapigwa chini endapo itathibika kwamba aliyeomba ni kada wa chama fulani. Awe CHADEMA, CCM, ACT atapigwa chini kama itathibitika ni kada.

3. Majina yaliyopita yatawekwa wazi na watakuwa wasimamizi katika ngazi ya jimbo ambao nao watatumia mtindo huo huo kuwapata wasimamizi kwenye ngazi za Kata, kisha ngazi ya kituo.
 
Nyokeni nao mbele Kwa mbele hao makada ndio tegemeo lao kwenye uchakachuzi
 
1. Njia ya kuwapata ni kwamba watu wenye sifa waombe hizo nafasi kwenye Tume ya Uchaguzi, mchakato uwe wazi.

2. Makada watawekewa mapingamizi na watapigwa chini endapo itathibika kwamba aliyeomba ni kada wa chama fulani. Awe CHADEMA, CCM, ACT atapigwa chini kama itathibitika ni kada.

3. Majina yaliyopita yatawekwa wazi na watakuwa wasimamizi katika ngazi ya jimbo ambao nao watatumia mtindo huo huo kuwapata wasimamizi kwenye ngazi za Kata, kisha ngazi ya kituo.

Kuwapata makada wa chama raisi sana kuwaexpose Kwa jamii jamii itakwambia huyu ni kada huyu si kada
 
Majina yawekwe wazi ili wananchi mwenyewe wawaone na kubaini makada na kuwatoa. Kwa hili tutawapata viongozi wa kweli na hii blah blah ya kutinga bungeni kuomba omba taarifa na miongozo itakoma. Wabunge watawajibika kwa wananchi wao na siyo kuitetea serikali
 
Wawe waajiriwa wa NEC kwa specific time, mfano miezi 6 au mwaka ambapo kazi itatangazwa na sifa za mwombaji kuonyeshwa kwenye tangazo. Sifa za mwombaji among others lazima zizingatie katiba. Kabla ya kuajiriwa, majina yatangazwe gazetini ili kama mtu ana zuio la haki kwa mwajiriwa anayekusudiwa, mtu huyo aweze kueleza na hasa kama mtu anayetakiwa kuajiriwa ni kada wa chama fulani.
Miezi sita au mwaka naona c sawa kwani wanaweza kuhongwa. Na yeye hawezi kukosa chochote kwani anajua kuwa hata akivurunda anaondoka
 
Miezi sita au mwaka naona c sawa kwani wanaweza kuhongwa. Na yeye hawezi kukosa chochote kwani anajua kuwa hata akivurunda anaondoka
Sina hakika kama NEC inaweza kuajiri wafanyakazi permanent kwa nchi nzima. Ma-DED wasingekuwa makada walikuwa wanasaidia kubana matumizi as walihitaji posho tu wakati wa uchaguzi na si mishahara kutoka NEC.
 
Leo asubuhi Bob Chacha WANGE ameshiriki kipindi cha gumzo cha BBC. sehemu ya mazungumzo yao:-
Mtangazaji:- mtazamo wenu hamuwataki MADED wasimamie uchaguzi; je ni nani wawekwe badala yao na itumike njia ipi kuwapata?
Wangwe:- sisi lengo letu ni kupata katiba mpya.... mtandazaji anamkatiza
Mtangazaji:- Swali langu nataka utusaidie namna ya kuwapata watu wa kufanya kazi ambayo kwa sasa wanaifanya MADED
Wangwe: Tunao ushaidi na tumeutoa mahakama MADED ni makada wa CCM

Nani anaweza kumsaidia Wangwe kujibu swali hili
Kwani nchi zingine zinazofanya chaguzi zisizoegemea chama fulani wanafanya Je ?!. Tena hizo nchi zime advance compare to us. eg Japan, S. Africa , Norweiy, S. Korea, France, Nigeria nk nk . Kwanini sisi tung'ang'anie kwenye chaguzi zenye hila ?!

Tatizo ni kukosa NIA NJEMA ya wanaoongoza serikali, kwa kujitazama wao na si kutazama taifa siku zijazo . Tukiongozwa na nia njema tutakuwa kioo barani Africa .

Kwingine nafasi hizi huwa wazi kwa wananchi wenye uwezo kuomba nafasi hizi. Si kuwapa watu wanaobanwa na sehemu ya wagombea. Na hii si kwa wakurugenzi tu, bali hata ngazi ya juu kuanzia na mwenyekiti na mkurugenzi wa NEC ngazi ya taifa. Ni watu wanaobanwa na mteuzi kumfanyia favour, kama si yeye basi chama chake.
 
Mkurugenzi wa NEC mwenyewe. Hapa tumekata matawi tu,steam na mizizi bado
nawadharau sana ccm tangu wajaze makada wao kwenye bunge la katiba hakika nawadharau sana! walianzisha mchakato mrefu namna ile kumbe hawakuwa wanamanisha?
 
sasa kwa mtazamo wangu hakuna watu wengine wenye kufaa na kutosheleza hilo hitaji
"longi mapexa, unawezaje kumjua mtu ambaye hana uelekeo kisiasa? Hii ndiyo changamoto. Wenye akili fupi wameenda mahakamani wakaomba wakapata walichoomba- ila nchi zima tumebaki na swali tunawapataje mbadala wao- yaani watu wasio wanasiasa wasimamie uchaguzi wa wanasiasa
 
Back
Top Bottom