Jilanga
JF-Expert Member
- Feb 13, 2011
- 255
- 40
Natanguliza heshima mbele JF! Kero yangu leo Board ya mikopo kwa wanafunzi wa Elimu ya juu (HESLB). Ukisoma Mission na Vision zake zimelenga kuwasaidia wananafunzi wa kitanzania wenye uhitaji!
Lakini ukweli ni kwamba hii board imekuwa ikifanya kazi kwa ubabaishaji mkubwa kiasi kwamba imeshindwa kuwasaidia wale wanaowataja kuwa wenye uhitaji. Mfano mwaka huu wametoa majina takribani 1800 ya wanafunzi ambao hawatopata mkopo kutokana na taarifa zao kutokuwepo OLAS. Kwa madai kuwa hawaja-update ama waliupdate wakati mtandao hauko sawa hivyo taarifa kutofika kama tujuavyo IT Tz bado shida! Japo kuna wanafunzi ambao hawakuupdate lakini cha ajabu kuna idadi kubwa waliupdate na kuprint updation zao lakini bado majina yanatoka kuwa hawakuupdate! mwezi August walibaini kuwa kuna wanafunzi wanaoendelea na masomo taarifa zao hazijawafikia kwenye mtandao wao wa OLAS, wakatoa fursa ya week mbili watu kujaza form OLAS kwa faini ya sh 30,000/= wakidhani kuwa wanafunzi walipuuza kuuqdate. Pasipo kutoa majina ya wanafunzi ambao taarifa zao hazipo OLAS. Siku chache baadae wakawataka radhi kwa matatizo yaliyoukumba mtandao wao!
Swali langu ni kwamba, kama kweli HESLB ipo pale kuwasaidia wanafunzi wenye uhitaji walishindwaje kutoa majina ya wanafunzi ambao taarifa zao hazipo OLAS?
Lakini pia Wakati wanafunzi wanajaza form za kuomba mkopo huwa wanajaza email na number za simu kwa ajili ya kuwapatia taarifa mbali mbali. Walishindwaje kuwatumia e-mails wanafunzi ambao taarifa zao hazikufika OLAS? Nawasilisha!