Board ya mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu yakosa ufanisi na uwajibikaji.

Jilanga

JF-Expert Member
Feb 13, 2011
255
40
Natanguliza heshima mbele JF! Kero yangu leo Board ya mikopo kwa wanafunzi wa Elimu ya juu (HESLB). Ukisoma Mission na Vision zake zimelenga kuwasaidia wananafunzi wa kitanzania wenye uhitaji!
Lakini ukweli ni kwamba hii board imekuwa ikifanya kazi kwa ubabaishaji mkubwa kiasi kwamba imeshindwa kuwasaidia wale wanaowataja kuwa wenye uhitaji. Mfano mwaka huu wametoa majina takribani 1800 ya wanafunzi ambao hawatopata mkopo kutokana na taarifa zao kutokuwepo OLAS. Kwa madai kuwa hawaja-update ama waliupdate wakati mtandao hauko sawa hivyo taarifa kutofika kama tujuavyo IT Tz bado shida! Japo kuna wanafunzi ambao hawakuupdate lakini cha ajabu kuna idadi kubwa waliupdate na kuprint updation zao lakini bado majina yanatoka kuwa hawakuupdate! mwezi August walibaini kuwa kuna wanafunzi wanaoendelea na masomo taarifa zao hazijawafikia kwenye mtandao wao wa OLAS, wakatoa fursa ya week mbili watu kujaza form OLAS kwa faini ya sh 30,000/= wakidhani kuwa wanafunzi walipuuza kuuqdate. Pasipo kutoa majina ya wanafunzi ambao taarifa zao hazipo OLAS. Siku chache baadae wakawataka radhi kwa matatizo yaliyoukumba mtandao wao!
Swali langu ni kwamba, kama kweli HESLB ipo pale kuwasaidia wanafunzi wenye uhitaji walishindwaje kutoa majina ya wanafunzi ambao taarifa zao hazipo OLAS?
Lakini pia Wakati wanafunzi wanajaza form za kuomba mkopo huwa wanajaza email na number za simu kwa ajili ya kuwapatia taarifa mbali mbali. Walishindwaje kuwatumia e-mails wanafunzi ambao taarifa zao hazikufika OLAS? Nawasilisha!
 
Hawa jamaa mfumo wa kuomba mkopo Online ni kama umewashinda. Kuna mapungufu mengi tumeyaona. (1)Wameshindwa kuweka majina ya wanafunzi wote walioomba mkopo kupitia OLAS baada ya tarehe ya kuomba mkopo kufika mwisho. (2)Mfumo waliotumia kutoa majina ya waliopata mkopo ni kama hawakuwa na uhakika. Inasikitisha sana na hawa ndiyo chanzo cha Umalaya vyuoni.
 
Serikali dhaifu. Hivi wanafunzi wanaosoma Urusi waliokosa hela ya kujikimu, nakukimbilia kwa barozi' hatima yao imefikia wapi?
 
hawa jamaa hivi kweli wameenda shule? je elimu yao inatija gani kwa jamii? kuna baadhi ya wasomi hapa nchini ni wanafiki
 
Bodi ya mikopo imejaa watendaji dhaifu sana,hata wale ambao hawana matatizo yoyote wapo UDSM,SAUT,UDOM,RUCO,TEKU na Ardhi lakini hawajapata hela za kujikimu bila sababu za msingi.Kuna wanafunzi walikuwa field hawakupewa hela mpaka sasa na hakuna maelezo yoyote ya msingi.Mwaka jana serikali dhaifu ya ccm ilitangaza kuunda upya HESLB lakini hakuna jipya lolote kiutendaji.Tunakoelekea wanafunzi watakuja kujitoa mhanga hapo msasani ili wafe pamoja na watendaji wa bodi.Hakuna haja ya kusitisha mikopo kwa wanafunzi 1800 eti taarifa zao hazipo OLAS.Hivi vijana hao wakirudi mtaani kwa kushindwa kuendelea na masomo kutokana na umasikini,serikali itafaidika nini?
 
Jaman kabla hamjawalaumu hawa jamaa mmewasiliana na hao wanafunzi ambao hawaku update mikopo yao? kwann hawaku update coz kitu sheria hukata huku na huku usipoomba huwezi pewa.Mi nilisaau ku update mpaka nikatoa ile faini ya 30000 sa kama m2 hata hiyo chance hakuiona shauri yake,mi siwalaumu bodi wanafuata sheria
 
Ebu tupe darasa zaidi una update vipi hizo taarifa zako OLAS wakati ni mwanachuo mpya?
Jaman kabla hamjawalaumu hawa jamaa mmewasiliana na hao wanafunzi ambao hawaku update mikopo yao? kwann hawaku update coz kitu sheria hukata huku na huku usipoomba huwezi pewa.Mi nilisaau ku update mpaka nikatoa ile faini ya 30000 sa kama m2 hata hiyo chance hakuiona shauri yake,mi siwalaumu bodi wanafuata sheria
 
makber ukisema asiyeupdate shauriyake unakuwa umekosea saana sana maana ujui wat hapened !.kweli ni kosa kupuuzia mambo lakn kumwambia m2 aahirishe mwaka kisa updation ni UONEVU ,mitandao yaweza kuwa ilikua inazngua HESLB wanafahamu kabisa ,wanathink using stomarch not brain !
 
Achwni kuwasingizia they just doing a great job

Wala usijaribu kuwatetea Hawa Watu,nimegraduate five years back now Nakatwa mikopo mwaka wa4 sasa have requested for my outstanding balances kwa maandishi kutoa kwa mwajiri wangu sijapata jibu mpaka Leo,surprisingly juzi Kati wakapandisha asilimia ya makato to 8percent your gross salary bila consent yetu,kulipa deni ni lazima Lakini makubaliano lazima yawepo Kati ya Mdaiwa na mdeni......this is insane
 
Soma swali langu kwanza mkuu!
makber ukisema asiyeupdate shauriyake unakuwa umekosea saana sana maana ujui wat hapened !.kweli ni kosa kupuuzia mambo lakn kumwambia m2 aahirishe mwaka kisa updation ni uonevu ,mitandao yaweza kuwa ilikua inazngua heslb wanafahamu kabisa ,wanathink using stomarch not brain !
 
Mbona wanafunzi wa kitanzania wanaosoma china wamesahauliwa hivi?jmani bodi ya mikopo ya elimu ya juu.tupeni fedha zetu vinginevyo muahe kukata mishahara yetu,winter imeanza maeneo mbalimbali ya china hata kununua nguo za baridi hatuwezi watu wa bodi badilika
 
huu ni use**** sasa kama data zake hazipo OLAS mbona mwaka wa kwanza kaja mmempa mwaka wa pili mmempa sasa kaja na anavithibitisho yeye ni mwanafunzi tatizo lipo wapi si wampe tu
 
Mi nikuwa pale bodi na jamaa yangu ambae haja update,wakamwambia 'Mkataba wa mkopo ni kwa ajili ya mwaka mmoja mmoja,so dent anatakiwa kila yr aoneshe kuwa antaka kuendelea kukopeshwa kwa ku update.So ili kuweza kuaproximate dent wangapi wameomba mkopo lazima kuwe na mwisho wa kuomba,na huo mwisho ukipita dent ambae haja update means hataki kulopeshwa. Kwa hili mi naona wako sahihi coz walitoa siku nyingi 16 Apr adi 30 jn +2wks lkn watu hawakuomba,ambao hawakuomba hawako makini na elimu yao.
 
hilo la mwaka wa pili na watatu lazma uaupdate taarifa coz huo ndo utaratibu but kiukweli wanazingua juct imagine kuna first year until zis time hawajapata mkopo so wat du u think abt dat ilhali waliomba na wakaambiwa wamepata bt still now danadana 2. stupid
 
Technology haijawasaidia! Na upuuzi wa TCU. Mi nafikiri TCU wangehamia TIRDO
 
Natanguliza heshima mbele JF! Kero yangu leo Board ya mikopo kwa wanafunzi wa Elimu ya juu (HESLB). Ukisoma Mission na Vision zake zimelenga kuwasaidia wananafunzi wa kitanzania wenye uhitaji!
Lakini ukweli ni kwamba hii board imekuwa ikifanya kazi kwa ubabaishaji mkubwa kiasi kwamba imeshindwa kuwasaidia wale wanaowataja kuwa wenye uhitaji. Mfano mwaka huu wametoa majina takribani 1800 ya wanafunzi ambao hawatopata mkopo kutokana na taarifa zao kutokuwepo OLAS. Kwa madai kuwa hawaja-update ama waliupdate wakati mtandao hauko sawa hivyo taarifa kutofika kama tujuavyo IT Tz bado shida! Japo kuna wanafunzi ambao hawakuupdate lakini cha ajabu kuna idadi kubwa waliupdate na kuprint updation zao lakini bado majina yanatoka kuwa hawakuupdate! mwezi August walibaini kuwa kuna wanafunzi wanaoendelea na masomo taarifa zao hazijawafikia kwenye mtandao wao wa OLAS, wakatoa fursa ya week mbili watu kujaza form OLAS kwa faini ya sh 30,000/= wakidhani kuwa wanafunzi walipuuza kuuqdate. Pasipo kutoa majina ya wanafunzi ambao taarifa zao hazipo OLAS. Siku chache baadae wakawataka radhi kwa matatizo yaliyoukumba mtandao wao!
Swali langu ni kwamba, kama kweli HESLB ipo pale kuwasaidia wanafunzi wenye uhitaji walishindwaje kutoa majina ya wanafunzi ambao taarifa zao hazipo OLAS?
Lakini pia Wakati wanafunzi wanajaza form za kuomba mkopo huwa wanajaza email na number za simu kwa ajili ya kuwapatia taarifa mbali mbali. Walishindwaje kuwatumia e-mails wanafunzi ambao taarifa zao hazikufika OLAS? Nawasilisha!

hawa jamaa washenzi sana mtu yuko nyumbani badala ya kumpa taarifa kua mkopo wake hautaendelea wanapiga kimya mtu anafika chuo paying slip zinakuja kutoka bodi dept. nzima wanafunzi hawana tena mkopo na walijaza form za kuendelea kupata mkopo mtu ananzaje kumjulisha mzazi ndo tunaonana matapeli wa wajue bodi ni moja ya sehemu inayotengeneza vijana kua chadema
 
Back
Top Bottom