BM Bus rekebisheni utoaji huduma wenu

BM Bus rekebisheni utoaji huduma wenu

mmteule

JF-Expert Member
Joined
Oct 3, 2011
Posts
6,035
Reaction score
15,071
Wadau Salaaam.

Baada ya Sifa kedekede humu jamvini kuhusu huduma za Mabasi ya BM nikiwa katika harakati zangu Jijini Dodoma nikajisemea ngoja nikamate BM BUS nishuke zangu Morogoro.

Huku na kule nikafika Ofisin kwao Pale Dodoma. Ofisi iko Kituo cha Mafuta, Kwanza Hakuna Viti vya Wateja kukaa kusubiri bus.

Lakini nikajisemea ngoja nifike Msalani kupata huduma.

Hakika Hawa BM BUS ni ama Menejimenti haijitambui au Mmiliki hana Exposure na Elimu ya Biashara ya kutosha.

Vyoo ni kama Jalala, nimefedheheka sana nguvu tunayotumia kupiga Promo za Utalii na madude kama ROYAL TOUR Halafu wenyewe walioshika Sekta Binafsi ndio hawa akina BM BUS.

Vyoo utadhan umeingia Jehanamu? Hakuna makopo ya kunawia, Tiles zina ukungu wa miaka kibao, Ndoo za Kunawia ni Madumu ya Oil yamekatwa just imagine LATRA mmeidhinisha hizi stendi Bubu pasipo kuweka Standards mwishowe tunazoa magonjwa.

Mamlaka zetu amkeni hii haikubaliki hata kidogo.
Picha zinajieleza
 

Attachments

  • 20220626_141632.jpg
    20220626_141632.jpg
    298.4 KB · Views: 18
  • 20220626_141646.jpg
    20220626_141646.jpg
    284.5 KB · Views: 17
  • 20220626_141959.jpg
    20220626_141959.jpg
    319.1 KB · Views: 22
  • 20220626_141553.jpg
    20220626_141553.jpg
    282.7 KB · Views: 18
  • 20220626_141558.jpg
    20220626_141558.jpg
    311.8 KB · Views: 20
  • 20220626_141624.jpg
    20220626_141624.jpg
    170.1 KB · Views: 23
  • 20220626_141548.jpg
    20220626_141548.jpg
    280.7 KB · Views: 19
Mkuu we sema tu kuwa ulishikwa na uharo wa ghafla tu, hayo mengine ni ajali kazini.

But on the real, watoa huduma wa Tanzania wana la kujifunza. Kuna msemo kuwa 'retail is detail. Sasa mtu unaweza kwenda sehemu huyo anaekupokea ni kama kalizimishwa kukuhudumia. Mazingira ya ofisi kama soko.

Kwa pesa wanayopata hao watu wamabasi hawashindwi kuweka ofisi zao kati mamdhari nzuri lakini mtu anaangalia faida tu.
 
Mkuu heri ungekuwa Mharisho maaana ukikuta hali kama hiyo lazima upone ghafla. Actual Call yangu ilipotea ghafla kulingana na Mazingira niliyokuta nikajisemea Hiiiiiii
Tatizo elimu duni sana ya uendeshaji biashara. Mmiliki akiona wateja wanakuja anaamini kila kitu kipo sawa.
 
mpwayungu anaaandamwa sana humu jamvini sahivi, ila kwa menejimenti ile LATRA waweke ukaguzi wa hizi stendi uchwara uchwara
Mpwayungu ni muhuni Sana
Mzee wa fix
Story za uongo
Sasa watu wamemchoka na uongo wake
Zaman kuna jamaa alikua anaitwa STUNTER alikua kama huyo boya saivi amepotea kimya kimya

Watu wasiojulikana
 
Tatizo elimu duni sana ya uendeshaji biashara. Mmiliki akiona wateja wanakuja anaamini kila kitu kipo sawa.
Uko Sahihi Mkuu hatutaki Kutanguliza Ubobezi mbele bali kazi tunawapa Vimada wetu na Wajomba zetu kisa ni Wanandugu matokeo yake ndio huu uhalo kwenye Uendeshaji.

Imagine Nauli ya Dom Dar yeye anachaji Tshs. 30,000/= kubwa kuliko Shabiby lkn Ofisi zao ndio ujinga ujinga wa hivyo.

Na mtu yeyote mwelevu utagundua kupitia miundombinu yake ya Usafi
 
Hivyo vyoo hatari sana,poor management
Nimeshangaa sana kukuta hali hiyo na Sifa ambazo zimekuwa zikimwagiwa hao BM kuuumbe ni Useless kabisa.
Mbaya basi lilibeba Abiria wengine takribani watatu ambao kwa Muonekano wanaweza kuwa wa Bara Ulaya au America, kama waliingia huko msalani sjui wameondoka na picha gani??? Poooor LATRA
 
Hivyo vyoo vinatumika na wapangaji wote wa hilo jengo pamoja na bar ya rainbow
Yaani ni vurugu tupu
Napajua hapo uholela umezidi
Hebu nendeni tena, mbona Ile sehemu inavyoo vizuri na visafi, na Wateja wa rainbow walivitumia kwa muda mfupi wakati wanafanyia ukarabati kwao.

Tatizo la vyoo vya pale ni vyakulipiana haijalishi ni MTEJA WA BM au laa.
 
Kwa iringa, ushindani wa vyoo vya PETROL STATION uko kwa Asas na Tawaqal, ni balaa, vyoo visafi sana huduma 24hrs Yani wako vizuri sanaa.
 
Hebu nendeni tena, mbona Ile sehemu inavyoo vizuri na visafi, na Wateja wa rainbow walivitumia kwa muda mfupi wakati wanafanyia ukarabati kwao.

Tatizo la vyoo vya pale ni vyakulipiana haijalishi ni MTEJA WA BM au laa.
Labda unasema Pahala pengine Mkuu au unaongelea historia ya vyoo hivyo vikiwa na wiki moja toka kujengwa kwake. Ukienda pale kwa sasa usithubutu!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom