Joel kaigarula
Member
- Jun 3, 2014
- 28
- 16
On a serious note, habari ni kuwa kampuni ya Google imeamua kufunga blog zote zenye picha za ngono kutoka kwenye platform yake ya blogger. Kwa lugha rahisi kwa faida ya wasiofahamu, platform ya blogger ni ile yenye anuani inayoishia ".blogspot.com". kila blog inayoishia na maneno hayo iko kwenye platform ya blogger.
Vile vile platform hii ya blogger inaruhusu matumizi ya anuani kamili (custom domain name), hivyo ziko blogs zinazotumia platform ya blogger, ambazo zina majina yasiyo na ".blogspot.com". Mfano mzuri ni blog hii unayosoma, anuani yetu rasmi ni www.bofyatz.com, lakini kimsingi iko juu ya bofyatz.blogspot.com, au mfano mwingine ni www.williammalecela.com ambayo actually ni williammalecela.blogspot.com. Hizi zote zinatumia mfumo wa blogger unaomilikiwa na Google.
Kupitia taarifa yake kwa umma, kuanzia tarehe 23 mwezi machi mwaka huu, hakuna blog yoyote kwenye platform ya blogger itakayoruhusiwa kupost picha au video za ngono.
Hii ni kwa blog zote bila kujali zinatumia ".blogspot.com" au custom domain name kama .com, na kadhalika. Hivi sasa blog za aina hiyo huweza kuingilika baada ya mtembeleaji kukubali onyo kuwa blog hiyo ina maudhui tata, kama inavyoonyeshwa pichani hapo chini.
Kutokana na mabadiliko haya ya kisera, blog zenye onyo kama la hapo juu, zitageuzwa kuwa private. Mtu pekee atakayeweza kuingia ni mwenye blog mwenyewe pamoja na watu wasiozidi mia moja ambao mwenye blog amewapa ruhusa (kwa maana ya username na password).
Kwa nchi ambazo zinaruhusu mambo ya pornography hili sio tatizo kubwa sana kwani waliokuwa na blogs hizi wanatarajiwa kukusanya content zao (archive) na kuhamisha blogs zao kwenye server binafsi, na kuendelea na blogs zao kama kawaida.
Lakini waendeshaji wa blogs za ngono kwenye nchi zisizoruhusu pornography kama Tanzania, huu unaweza kuwa ni mwisho. Platform ya blogger ilikuwa na kivutio cha usiri, hasa kwa wale waliokuwa wanatumia anuani ya "blogspot.com".
Hakukuwa na njia yoyote ya kumjua mhusika mwenye blog (actually zipo lakini mlolongo ni mrefu sana labda ushirikishe FBI hivi). Hawa hawataweza kuhamia kwenye server binafsi ndani au nje ya nchi, kwani hilo litahusisha malipo na malipo yatasababisha kumbukumbu za kibenki.
Hivyo kama blog ikifuatiliwa, itajulikana imekuwa hosted na kampuni gani, kampuni ile ikifuatwa na vyombo vya sheria itataja nani alisajili mtandao husika. Hii ndio maana blog kama hiyo yenye bango mwanzo wa habari, inatumia ".blogspot.com" badala ya custom domain.
Hii ni kwa sababu kama ingetumia .com au .net, vyombo vya sheria vingeweza kufuatilia kampuni iliyosajili jina hilo na kumjua aliyelipia ni nani.
Matumizi ya blogspot.com hayahitaji malipo kokote kule, hivyo hata ukienda kwa kampuni ya google, hawataweza kukupa jina la mmiliki, labda watakupa IP addresses ambazo mmiliki anatumia, ambazo hata hivyo zinaweza kuwa ni addresses feki kupitia huduma kama TOR na kadhalika. Mmiliki anaweza kuwa Tanzania lakini IP adress yake ikasomeka yuko japan!
Hatua hii ya Google haitaathiri kimapato waandishi wa blog za aina hii huku kwetu Tanzania. Hii ni kwa sababu Tanzania hairuhusu haya mambo ya picha za ngono, na hivyo blog zote zinazohusu hayo mambo sio blog za kibiashara kwa maana kuwa haziingizi kipato. Hivyo kuondoka mtandaoni hakutawaathiri bloggers wake kimapato kwa sababu ilikuwa ni hobby tu.
Watakaofaidika kiasi fulani ni watu ambao picha zao chafu zilivuja kwenye blogs za huduma ya blogger. Hawa watakuwa na ahueni kiasi fulani kwa sababu blog nyingi za kitanzania zinatumia huduma ya blogger na hivyo kwa hatua hii, picha hizi zitakuwa zimefikia mwisho au kupungua kwa kiasi kikubwa mtandaoni.
Hata hivyo, inatarajiwa kuwa waendeshaji wa blog za ngono kwa nchi kama Tanzania watahamia kwenye platforms mbalimbali mahsusi kwa ajili ya content za ngono na kufungua akaunti huko.
Hivyo archive zao bado zitakuwapo tu mtandaoni, ingawa akaunti hizi sio blogs, bado picha na video zitakuwapo pale pale. Hivyo njia pekee ya kuepuka aibu ya mtu kujikuta wazi mtandaoni ni kutokupiga picha hizi kabisa.
source:bofyatz.com