Blind date hii noma sana

Mimi nina experience tofauti aisee. Nilikutana na binti mmoja hapa hapa JF. Ni binti msomi na mwenye mtazamo mpana sana kuhusu maisha na masuala mbali mbali yanayohusiana nayo. Yaani mkikaa kuongea utafikiri unaongea na Socrates jinsi anavyopangilia hoja kulingana na mada. Mpaka leo nikiwa na jambo zito linalonitatiza ndiko ninakimbilia kuomba msaada wa kimawazo.

Physically pia binti yuko vizuri siwezi kulalamika na ni mtu wa gym sana - flexibility from yoga ile mbaya (if you know what I mean). Kwangu mimi sina cha kulalamika kwa kweli. Thanks JF!
 
Kama anaongea like Socrates huyu atakuwa yule binti anaetumia ID ya housegirl!
 

Hahahah pole
Beauty(of a woman)is inversely proportional to smartness
So vice versa is true
 

Kama malengo si mapenz nahisi yaweza kuwa ni sehemu nzuri sana ya kimuit Gt regardless jinsia, hongera sana, thanks kwa mrejesho
 
IDs noma mana ni vizuri kuzingatia privacy za watu kwani hata mawasiliano yalikuwa kwa PM tu
Kama unaona noma nini kimekutuma ulete huu uzi kuwaumbua watu acha mambo ya primary
 
Uko interested sana na mada za mlengo huu.
Mkuu nilichojifunza ni kwamba mtu unaweza kujifunza tabia za mtu na kumuelewa kwa undani kupitia JF bila hata ya kuonana au kukutana nae!!!...... Unaweza kujifunza na kuelewa tabia za mtu kama vile tabia za uchepukaji,umbea, kupenda mapenzi ya fedha,utapeli,mtu huwa anafanya nini huko PM,dharau, kujali wengine, umri wa mtu, shughuli ya mtu, jinsia,lengo la mtu JF na tabia nyingine za kibinadamu kwa kuangalia huwa anaadika thread za aina gani, huwa anachangiaje na nini kwenye thread za watu, huwa anareact vipi mtu akimuuzi, huwa anareact vipi akisifiwa,huwa anachangia katika mood gani, huwa anaamini nini kwenye maswala mbalimbali, msimamo wake ni upi kwenye mambo fulani fulani,huwa anapenda kuchangia thread za aina gani, huwa anapenda kuchangia thread za akina nani e.t.c!!
 
Jamani kwani blind date ndo nini?
 
Humu unakuta mtu anajitia kuwa active kumbe ni home mom ..anawatoto watatu na ndoa ..akija basi ujue mumewe kasafir
ukimpa keyboard sasaaa..si utajua totoooz nimepata..kwa mahaba kwa washa washa zoote anajua
akija ki date kaja na kitenge mixa kikoi..lol
 
Jamani kwani blind date ndo nini?
term za wazungu sana hizi..ni ki outing ambacho hujawahi kuonana na mtu ata mara moja, ndo first time yenu..unaweza kuta ni marafiki zenu wame wa set for a date, au mmekutana mtandaoni..ili mradi muwe hamjawahi kuonana na ni mara ya kwanza
 
term za wazungu sana hizi..ni ki outing ambacho hujawahi kuonana na mtu ata mara moja, ndo first time yenu..unaweza kuta ni marafiki zenu wame wa set for a date, au mmekutana mtandaoni..ili mradi muwe hamjawahi kuonana na ni mara ya kwanza
OK..ahsante mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…