Blackberry yaboresha Mitandao ya Kijamii kwenye BB OS 10

Blackberry yaboresha Mitandao ya Kijamii kwenye BB OS 10

ManiTek TV

JF-Expert Member
Joined
Jun 3, 2011
Posts
410
Reaction score
159
[h=1]Blackberry Yaboresha App Za Mitandao ya Kijamii OS 10[/h]

​
Blackberry imeboresha app za Facebook na Twitter kwa simu zinazotumia Blackberry OS 10, watumiaji wa simu zenye OS hiyo wataweza kupakua bure uboreshwaji huo kwenye duka la app la OS hiyo yaani “Blackberry World”, uboreshwaji huu utawafanya watumiaji wa simu za Blackberry Z10 na Q10 kuweza kutumia apps hizo kwa ufanisi zaidi. Taarifa hizi zimetolewa kupitia blogi rasmi ya Blackberry


Uboreshwaji wa Facebook 10.0.1


Marafiki Walio Karibu: App ya Facebook iliyoboreshwa ambayo ni toleo la 10.0.1 itawapa watumiaji uwezo wa kuwagundua marafiki wanapotoa taarifa ya kuwasili (check in) mahala ambapo karibu na alipo mtumiaji.


​
Picha: Pia watumiaji wataweza kuziambatanisha (tag) picha zilizo kwenye Facebook kwa urahisi, kadhalika wataweza pia kupakua picha hizo na kuzihifadhi kwenye simu zao.


Matukio (Events): Facebook 10.0.1 imerahisisha sana kupanga na kuweka vizuri matukio yako. Imekuwa ni rahisi kutoa mwaliko kwa marafiki zako, pia katika ukuta wa tukio mtumiaji anaweza kuweka maoni, picha na kuwa-tag waalikwa.


Kubadilishana (share): Kubadilishana habari kumeboreshwa katika toleo hili la Facebook app. Mtumiaji anaweza kuhamisha taarifa kwa urahisi baina ya Facebook, Twitter, barua pepe, BBM, ujumbe mfupi na mawasiliano ya aina nyingine.


Twitter toleo la 10.0.2


​
Your Connect Tab: Twitter 10.0.2 inakuruhusu utazame matukio mbali mbali katika sehemu moja, pamoja na kufuatilia habari inayoitaka mwenyewe ambayo imetwaja. Huu ni moja kati ya ubora wa BB10 OS kwa ujumla, kwamba taarifa nyingi zanaweza kujumuishwa mahala pamoja kwa kutumia mtindo wa Blackberry hub. Hata hivyo uboreshwaji huu ni tofauti ha BB hub.


Maudhui ya Ziada: Kufuatia uboreshwaji huu sasa unaweza kuangalia picha, muhtasari wa makala na taarifa nyingine bila ya kutoka kwenye app ya twitter.


Mtazamo wa nyongeza: - Katika toleo hili la twitter utaweza kujua ni mara ngapi tweet imependwa (favoured) na watu mbali mbali.




Ikiwa unatumia simu yenye BB OS 10 basi pakua apps hizi kwenye kwenye viungo vifuatavyo:


Facebook 10.0.1


Twitter 10.0.2

Chanzo: gajetek habari
 
Sure Millah After 1 year Nitakuwa Nimejifunza Mengi Kupitia Wewe Nice Work
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom