Blackberry kusitisha utengenezaji wa simu

Blackberry kusitisha utengenezaji wa simu

Kurzweil

JF-Expert Member
Joined
May 25, 2011
Posts
6,623
Reaction score
8,427
Kampuni ya simu ya Blackberry itasitisha kutengeza simu aina ya smartphone baada ya miaka 14 katika bishara hiyo ,kampuni hiyo imetangaza.

Ikiwa wakati mmoja kiongozi katika soko la mauzo ya simu,kampuni hiyo imeshindwa katika kuhimili kasi ya mashindano na kampuni za kisasa za simu kama vile Aple na Samsung.

Mnamo mwezi Mei,afisa mkuu wa kampuni hiyo John Chen ,alisema kuwa atajua ifikiapo mwezi Septemba iwapo biashara yake ya simu itakuwa ikileta faida au la.

Blackberry sasa inasema kuwa itazitumia kampuni nyengine inazoshirikiana nazo kutengeza simu hiyo.Lakini kampuni hyo haijasema ni lini simu nyengine za Blackberry zitatolewa.

Bwana Chen amekuwa na hofu kuhusu hatma ya biashara ya simu,akisema angependelea kuifunga iwapo haitoi faida yoyote.

Chanzo: BBC

 
Hao walishajifia kitambo, hata wazee hawanunui simu zao
 
Nina ya kwangu Balckbery Passport ina miezi minne tu iwe haina kazi ,
Sijui kama kuna simu nitakuja kuipenda kama Blackberry
 
Back
Top Bottom