Bubu Msemaovyo
JF-Expert Member
- May 9, 2007
- 3,877
- 2,888
Ukisoma taarifa hizi utadhani unaangalia filamu fulani ya kutisha, lakini ukizinduka na kuona kumbe huoni picha bali unasoma ndipo unapata mawazo mapya kwamba huenda uko sehemu nyingine na siyo hapa Tanzania tunapopaita "Kisiwa cha Amani" ili uweze kukubaliana nami soma hapa.
*Watoa masharti ya kupewa sh. milioni 10
*Baba mtu ajitosa msituni usiku kuwapelekea
Na Mwandishi Wetu
KUNDI la majambazi linalojiita Black Mafya, limemteka mtoto Fardosa Mohamed Othuman (2), mwenye asili ya kisomali mkazi wa Mtoni Saba Saba, Dar es Salaam.
Tukio la kutekwa kwa mtoto huyo ambalo lilitokea juzi saa 3 asubuhi karibu na baa ya Ikweta Grill.
Akizungumzia tukio hilo Dar es Salaam jana, mama mzazi wa mtoto huyo, Bibi Anab Ahmed, alidai kuwa mtoto wake alitekwa saa tatu asubuhi, huku watekaji wakiacha masharti makali kwa familia yake.
Alidai kuwa masharti yaliyoachwa na watekaji hao ni kwamba hawatakiwi kutoa taarifa sehemu yoyote wala kituo chochote cha Polisi na wakibainika kufanya hivyo, mtoto waliyemteka atauawa.
"Ni tukio la kusikitisha katika familia yetu, kwani baada ya mtoto kuchukuliwa na watu hao, wakatuachia masharti makali yakiwamo ya kututaka tufiche siri kwa kutosema kwa mtu yeyote kupitia barua ambayo walikuwa wameleta saa chache kabla ya kumteka mtoto wangu," alidai Bibi Ahmed.
Aliongeza kuwa masharti mengine yalikuwa ni kupewa sh. milioni 10 ili mtoto huyon aachwe akiwa salama.
Alidai siku ya tukio kabla ya mtoto wake kutekwa kuna mtu alipeleka barua nyumbani kwao akidai kuwa ni ya mumewe.
Wakati huo nyumbani kulikuwa na watoto huyo na wengine na wafanyakazi wa ndani wawili, hivyo walichukua ile barua na kuiweka ndani ili baba yao atakaporudi wampe.
Baada ya muda mfupi kupita, mtoto huyo ambaye alikuwa ndani ya eneo la uzio wa nyumba yao, aligundulika kutoweka.
"Muda wote mtoto alikuwa akicheza ndani na wala hakutoka nje ya lango la nyumba yetu, lakini cha kushangaza baada ya yule mtu kuleta barua, alipoondoka mtoto hatukumwona ndipo tulipomtafuta bila mafanikio.
"Hata hivyo, tuliamua kupiga simu kwa baba yake kumpa taarifa za kupotea kwa mtoto na kumweleza kuwa kabla ya mtoto kutekwa, kuna barua yako imeletwa na watu ambao ndio watakuwa wamemchukua," alidai Bibi Ahmed kwa masikitiko makubwa.
Baada ya taarifa hiyo, baba wa mtoto, aliwaruhusu waisome barua hiyo, kwani yeye hakuahidiana na mtu kupeleka barua nyumbani, na walipoisoma ile barua, ndipo ilipoonesha wazi kuwa mtoto ametekwa na majambazi hao.
Alidai kuwa ndani ya barua hiyo kulikuwa na vitisho kwa wazazi kwamba vizipotekelezwa mtoto wao atakuwa hatarini.
Aliendelea kudai kwamba ilipofika saa 7 mchana, watu hao walipiga simu kwa baba na kusisitiza kuwa watamwachia iwapo atatimiza masharti yao kabla ya saa 24 kupita.
"Ilituchukua muda kuamini kama mtoto wetu yuko hai au la kwa sababu kila tulipotafakari tulishindwa kuelewa, lakini tulichofanya ni kumwomba Mungu mtoto wetu tumkute salama," alidai Bibi Ahmed.
Aliongeza kuwa majambazi hao walitoa taarifa kwamba wangepiga simu tena saa 11 jioni kujua wapi wanaweza kukutana na baba wa mtoto, ili wapewe fedha walizohitaji ili wamwachie mtoto huyo.
Hata hivyo kuanzia saa 7.30 mchana simu waliyokuwa wakitumia majambazi hao ilizimwa na kuwashwa saa 12 jioni na kupiga simu kwa baba wa mtoto wakitaka wakutane maeneo ya Mbagala katika vichaka.
Alidai kuwa baba wa mtoto alikubali amri hiyo na kuchukua sh. milioni 3.5 baada ya kukosa sh.milioni 10 waliyokuwa wakiihitaji majambazi hao.
"Ukweli hatukuwa na kiasi hicho cha fedha, hivyo tulichukua sh. milioni 3.5 na baba wa mtoto kwenda walikopanga kukutana. Baada ya kufika ikiwa ni saa 3 usiku, alifuata maagizo ya kuweka fedha hizo chini.
"Walizichukua fedha hizo na kumwachia mtoto na kurudi naye wakafika nyumbani saa nne usiku wa kuamkia leo (jana)," alisisitiza Bibi Ahmed.
Alidai mtoto huyo alikuwa amechoka na aliporudi nyumbani na inawezekana ni kutokana na kukosa kula kwa muda wote aliokuwa mateka.
Alieleza kuwa walifuatilia Polisi Chang'ombe jana asubuhi, ili kujua kama majambazi waliokuwa wamemteka mtoto wao wanafahamika lakini wakaambiwa bado uchunguzi unaendelea ili kubaini wahusika.
Kwa upande mwingine, walisema ulinzi uliopo katika eneo hilo ni mdogo na hivyo ni vigumu wao kutambua nani adui na nani mwema.
"Tunaishi kwa hofu na mashaka makubwa hivi sasa, maana hatujui nini kitafuata baada ya tukio hili, ukiangalia na masharti tuliyokuwa tumepewa na watu hao," alisema dada wa mtoto aliyetekwa, Bi Saad Mohamed.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Temeke, Bw. Emmanuel Kandihabi alithibitisha kuwapo kwa tukio hilo, na kusema uchunguzi unaendelea ili kuwakamata waliohusika na utekaji huo.
Wakati huo huo, wakati waandishi wawili wa gazeti dada la Dar Leo, Bi Stella Aaron na mpiga picha Charles Lucas wakifuatilia tukio hilo nyumbani kwa mateka, waliwekwa chini ya ulinzi na polisi wa Chang'ombe wakidaiwa kuingia nyumbani kwa mtu bila idhini.
Kamanda Kandihabi alipouliuzwa kuhusiana na hatua hiyo, alisema alitoa amri ya kukamatwa kwa wanahabari hao ili kuwahoji na kujiridhisha kama hawakuwa wamevamia nyumba ya mtu baada ya baba wa mtoto kuwatilia shaka.
"Tumewakamata ili kuona kama hawa waandishi walivamia au la, kwani tukio lenyewe ni la ndani...lingekuwa la hadharani tusingehangaika nao, lakini mtu yuko ndani nyumbani kwake akifanya mambo yake, unaingiaje huku amefunga milango?," alihoji Kamanda huyo na kusema aliwasiliana na baba wa mtoto ambaye alionesha wasiwasi wa watu kuingia nyumbani hapo.
http://www.majira.co.tz/kurasa.php?soma=tanzania&habariNamba=7339