JPN
Senior Member
- Jul 28, 2013
- 119
- 42
Anazungumzia juu ya kwanini anaenda kwenye Mialiko ya Kiserekali.. Ameaanza kuzungumza kwamba kanisa Hili LA FGBF siyo la Chama cha CHADEMA wala CCM wala chama chochote kingine.... Ndiyo anaendelea kuzungumza
juu ya kwanini anaenda kwenye Mialiko... Na kanisa Hili siyo CHADEMA wala CCM wala chama chochote kile....
======
"Sijawahi kuwa mwanachama wa chama cha Chadema wala CCM, na sina kadi ya vyama hivyo"-Kakobe
"Sijawahi kuwasiliana na kiongozi yoyote wa Chadema wala kuonana nao ana kwa ana, wala hawajawahi kuja ofisini kwangu, halijawahi kutokea"-Kakobe
"Niliwahi kuitikia mwaliko wa chama cha Chadema mara moja tu miaka michache iliyopita kwenye mkutano uliofanyika eneo la Mlimani City na nilienda kama baba anayeweza kualikwa na watoto"-Kakobe
"Wakati wa vuguvugu la katiba, niliwahi kwenda kwenye mkutano wa Chadema uliokuwa unafanyika katika viwanja vya Jangwani, na nikizungumza na Mbunge John Mnyika kwenye simu kuhusu mkutano huo, na nilikwenda"-Kakobe
"Hata Rais Magufuli akiniteua Leo siwezi kukubali, nitamueleza Nina kazi maalum ya kumtumikia Mungu, siwezi kuwa mbunge alafu nikakaa bungeni miezi mitatu niache kumtumia Mungu"-Kakobe
"Siwezi kuwa Mbunge wala Waziri, na hata siku ikitokea nimeteuliwa na Rais, nitasema asante lakini sitakubali"-Kakobe
"Waumini wangu si mnajua nina pesa, si mnnafahamu nilisema mimi ni tajiri kuliko serikali, si TRA wanajua walikuta fedha nzuri tu Benki, si walikuta akiba nzuri katika akaunti ya kanisa, utaninunua kwa bei gani? Sina bei mimi"-Kakobe
"Wanaosema mbona Askofu Kakobe anatuacha Chadema, " Niliwaacha wapi? Lini niliwahi kuwa na nyie? "-Kakobe
Habari zaidi...
Askofu Mkuu wa Kanisa la Full Gospel Bible (FGBF), Zachary Kakobe amewataka viongozi wa Chadema waliotukana viongozi wa dini watubu hadharani, wasipofanya hivyo, chama chao kitatumbukia kwenye shimo refu zaidi, hawataweza kuinuka tena.
Kiongozi huyo wa FGBF ametoa kauli hiyo leo Jumapili Januari 27, 2019 jijini Dar es Salaam wakati wa ibada kufuatia siku za hivi karibuni kuonekana mara kadhaa kwenye hafla za Rais John Magufuli na kupewa nafasi ya kuomba.
Pia, amesema yeye na kanisa hilo si wanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo( Chadema). Hata hivyo, amesema aliwahi kuhudhuria mkutano mmoja tu wa Chadema uliofanyika Mlimani City na kwamba katika mkutano huo alihudhuria si kama mwanachama bali kama baba ambaye anaweza kualikwa na watoto wengi.
"Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, sijawahi kuwa na mazungumzo naye; iwe kanisani au nyumbani au mahali popote. Hata katika mkutano ule nilipokelewa na viongozi wengine kabisa," amesema Askofu Kakobe. Amesema hajawahi kuonana wala kuzungumza kwa simu na mbunge wa jimbo la Ubungo (Chadema), Saed Kubenea ambaye anaongoza eneo ambalo kanisa lake lipo.
"Kama hamjui, nimehudhuria mikutano mingi zaidi ya CCM kuliko Chadema. Nakumbuka wakati mmoja niliwahi kuhudhuria mkutano wa wazee kumuaga Rais Benjamin Mkapa, nilialikwa na Yusuph Makamba. Wakati ule nilihudhuria mikutano mingi kwa sababu Makamba ni rafiki yangu sana," amesema.
Askofu Kakobe amesema kuhudhuria kwake mikutano ya Rais Magufuli kumeibua mitazamo tofauti, wengine wakisema ameahidiwa ubunge na wengine wakisema amenunuliwa. Hata hivyo, amekanusha madai hayo.
"Wanasema 'sasa inakuwaje umeanza kuandamana na Rais Magufuli, umeahidiwa ubunge? Nianze kukaa bungeni miezi mitatu, nani atafanya kazi hii. Hata nikiteuliwa, nitasema asante, nimeitwa kwa kazi moja tu."
"Wengine wanasema labda amenunuliwa, mimi? Si mnaelewa nina hela? Si wanafahamu nilisema nina hela kuliko Serikali? Si wanafahamu TRA walikuta fedha nzuri tu kwenye akaunti ya kanisa? Sasa unaninunua kwa bei gani, sina bei," amesema Askofu Kakobe huku waumini wake wakimshangilia.
CHANZO: Gazeti la Mwananchi.
Sent using Jamii Forums mobile app