BISHOP KAKOBE::Tanganyika Huru Lazima Ipatikane

Mkuu najaribu kuimajini ndio unadrive au uko kwenye basi unakutana na hicho kibao,raha sana
Hili jina lina mvuto kuliko Tanzania.

Mungu ibariki Tanganyika,Mungu ibariki Afrika.
===>Liko sehemu moja mkoani tanga (ukitokea muheza kwenda Tanga liko hivyo hivyo)
 
Asante Mungu kwa kumfufua Lazaro wetu,yaani Tanganyika,waliyemzika kwa miaka 50,kwa visingizio vya kusema ananuka,pale ulipowambia watoe jiwe,jiwe limetoka,tumebaki kufungua sanda na leso tu,halaf awe hai kabsaa kwa uwezo wa Mungu.ameeeni!!
 
kwa nini hujamuulza kikwete ambaye alienda kuongea naye au alikalia kuchekacheka tu kama anavyofanya na/kwa akina makinda!

..........kakobe kapewa taarifa za tanganyika na Bwana, sasa vipi kuhusu ziwa Nyasa.....arahisishe hapo !
 
Kakobe ni jasiri haogopi mtu atakama anatishiwa kunyongwa leo, huyu ndiyo Mtumishi wa Mungu asiyechumia tumbo kama wengine masaka tonge
 
Na huyu mtumishi wa MUNGU Kakobe ni hazina ya taifa tuliyopewa na MUNGU.

Ni sawa kabisa. Nakubali ni Mtumishi wa Mungu. ila kumbuka wako watumishi wa Mungu wenye kuona serikari mbili ndo jawabu.

Ni vema hisia zako kama kiongozi wa dini ziwe zako na wala sio za kanisa. Una waumini wenye milengo ya kisiasa tofauti na wewe . Na hilo haliwafanyi wao kuwa wahaini. Misimamo hiyo ilitakiwa itolewe bungeni. Maana ndo mahali pake , sio kanisani.
 
Ni vyema ikaeleweka wazi kwamba mtumishi wa Mungu Askofu Zachary Kakobe, alieleza kuhusiana na kurudi kwa Tanganyika si kwa ushabiki wa kisiasa bali KIBIBLIA, na kimsingi alitoa angalizo hilo tangu mwanzo wa mahubiri kabisa. Kwa hiyo tujadili hili huku tukiwa na angalizo hilo. Ndio maana alizingatia sana kuthibitisha ayasemayo kwa kutumia biblia
 
Najua wazi kuwa wapo wachache wavivu wa kusoma, kusikiliza kwa makini na kufuatilia mambo. Hawa ndio wanaoleta fujo na kuzungumza hovyo hovyo tu kwasababu ya ujinga wao.
Hawa hufikia mahali hata kuwakashifu watumishi wa Mungu. Binafsi napenda kuwapa onyo kwamba waache hiyo tabia kwani haitawasaidia, bali ni kujitafutia laana tu zinazoweza kuepukika.
Ushauri wa bure tu kwa hao wasio na adabu
 
Asante Mungu kwa kumfufua Lazaro wetu,yaani Tanganyika,waliyemzika kwa miaka 50,kwa visingizio vya kusema ananuka,pale ulipowambia watoe jiwe,jiwe limetoka,tumebaki kufungua sanda na leso tu,halaf awe hai kabsaa kwa uwezo wa Mungu.ameeeni!!

Waafrica tunakuwa wa ajabu. Tunawezaje kuthamini mipaka aliochora Mjerumani na kutugawa. Na kubeza juhudi za waasisi wazalendo wa kiafirika waliojaribu kuunganisha tena jamii zetu baada ya kumwondoa mkoloni.

Kama tunaidai Tanganyika yetu. Tukiipata Tanganyika, Siku Moja tutaidai Kilimanjaro yetu au Mwanza. Tutadai hati au sahihi za kuunganishwa maeneo yetu na Tanganyika. Tutadai uhalali wa mkutano na mipaka iliyowekwa Berlin.
 
Dini na siasa ni vitu viwili tafauti,ushauru wangu Askofu angalia neno la bwana acha siasa kwa wanasiasa
Bonge la ushauri ila haya wameyataka wenye serikali yao maana juzi kati kuna viongozi wa dini wametoa msimamo wa serikali mbili wamepongezwa na kuwa reference kwa wenye huo msimamo, leo ameibuka kiongozi mwingine na mtazamo wa serikali tatu ataonekana kituko simply because yupo against the system. Ipo siku ataibuka kiongozi mwingine wa dini na kusema muungano ufe.

Viongozi wa dini wana ushawishi sana kama serikali ingekuwa inajua isiwe na bias kwenye hili
 
Siku hizi hamuwatoi watu kwenye hoja, mambo ya zamani eti siasa na dini ni vitu viwili tofauti? Siasa ni maisha sio taaluma, kama asiposema kakobe mtu mwingine atasema, asiposema mtu yeyote jiwe litasema.
Angesema anataka serikali mbili hapo nadhani wangeona poa kabisa
 
Amesema Tanganyika huru lazima ipatikane ni
suala la muda tu
Nchi yetu imekuwa katika laana kwa muda mrefu
kwa sababu tumeshindwa kuilinda mipaka yetu
Moto wa kudai Tanganyika umewaka na hamna
mtu awezaye kuuzima. Awaonya watawala kusoma
alama za nyakati na amewataka kuiepusha nchi
kuingia katika machafuko kwa kuridhia Serikali ya
Tanganyika.
Pia amesema Nyerere sio Mungu naye ana
mapungufu yake wanaomuabudu wanakosea.
Kosa alilolifanya Nyerere ni kuruhusu kuunda
serikali hewa ya Tanzania bara ambayo kimsingi
haipo ukiliganisha na Zanzibar.
Amewaonya viongozi wanaopinga kurejeshwa
kwa Tanganyika kuwa wataitumbukiza nchi katika
machafuko.
...Hizo zilikuwa salamu za Pasaka alizozitoa leo
katika kanisa la FGBF Dar es salaam.

Acheni siasa Makanisani nyiee aaah!! Hembu kuweni na adabu kwny nyumba za Ibada...
 
na itaptikana tu...
Au ingekuwa ni serikali moja tu,kama wanataka muungano uendelee.isiwepo serikali ya zanzibar,iwe nchi moja tu.JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA,alafu iwe ya majimbo,Ambapo na zanzibar kutakuwa na majimbo nako.si ni muungano.mkiungana si mnakuwa kitu kimoja sio kama ilivyo sasa.kinyume na hapo lazima TANGANYIKA YETU TUIPATE,MBONA WAO WANA ZANZIBAR YAO!!
 
Back
Top Bottom