Birth day yangu ni 09.12.2011 natimiza miaka 50 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Birth day yangu ni 09.12.2011 natimiza miaka 50

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mpui Lyazumbi, Dec 1, 2011.

 1. Mpui Lyazumbi

  Mpui Lyazumbi JF-Expert Member

  #1
  Dec 1, 2011
  Joined: Sep 1, 2010
  Messages: 1,853
  Likes Received: 146
  Trophy Points: 160
  Wakuu heshima mbele. Nimeanza mwezi wa kumi na mbili kwa faraja kuu. Kwamba ifikapo tarehe 09 natimiza umri wa miaka 50-sambamba na uhuru wa Tanganyika. Kwa kweli ni safari ndefu sana, na naomba nilete kwenu siku yangu muhimu kabisa. Na kwa kawaida yake, wanabodi mtazungumza mengi hasa yenye kunijenga mkizingatia kuwa miaka 50 si haba. Kuna wengi hawakuisogelea kiasi changu na kuna waliozidi hapa. Nasema binafsi nimekuwa na mafanikio kiasi katika MAISHA na mchango wangu umekuwa wa kuridhisha katika ujenzi wa TAIFA. Hata hivyo kasi ya kujiletea maendeleo kama taifa bado ni ndogo sana. Tufanye nini kwa ajili ya mafanikio ya kizazi kijacho?

  NAWASILISHA.
   
 2. Lasikoki

  Lasikoki JF-Expert Member

  #2
  Dec 1, 2011
  Joined: Jan 10, 2010
  Messages: 642
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  kwanza hongera, namshukuru Mungu kwa ajili yako

  Then, nina swali binafsi, je wewe binafsi unaweza kutupa muhutasari wa maisha yako ktk nyanja mbalimbali mathalan kiuchumi, kijamii, kielimu, kiimani, kisiasa n.k Je ni yepi umefanikiwa na yepi hukufanikiwa? Je nchi kama nchi na sera zake, uongozi wake vimechangia kiasi gani ktk mafanikio au failure zako as an individual? Tufanyeje, tuboreshe vipi?

  Nasema hivi coz wewe ni unit ya jamii na taifa. Mafanikio ya kila mmoja wetu ni mchango mkubwa tunapozungumzia maendeleo in totality kama nchi.

  Niko interested kupata muhutasi wa safari ya maisha yako towards maendeleo and self satisfaction.

  By the way if its becoming personal just leave it na pokea salam na hongera zangu kwako za kutimiza miaka 50 mnako 9 desemba
   
Loading...