Bird's eye: Nahofia kuna utumiaji mbaya wa fedha za serikali zinazotumika kununua wanachama wa vyama vya upinzani

Ki Mun

JF-Expert Member
Oct 6, 2014
3,443
4,384
Haya mambo akina Grace watayashangilia wakati huu lakini ipo siku ukweli utajulikana...

Kipindi hiki kuna miradi mingi mikubwa ya mabilioni ya shilingi inayotekelezwa kwa kauli tu za mtu mmoja na mimi nahofia hizo fedha zinazotolewa kutumika kwenye hiyo miradi ndo hizo hizo zinatumika kununua kwa bei yoyote viongozi na wanachama wa vyama vya upinzani. This is nothing short of money laundering...ipo siku mtajibu dadeki zenu - MAYANGA CONTRACTORS! IPO SIKU MTAJIBU!
 
BODI YA USAJILI WA MAKANDARASI YAZUNGUMZIA UTENDAJI KAZI WAKE
  • Vigezo vya wakandarasi
  • Tofauti ya mhandisi na makandarasi
  • Tofauti ya Bodi ya Uhandisi na Bodi ya usajili wa Makandarasi
  • mkandarasi kusajili kampuni, cheti cha FTC kinatosha kuanzisha kampuni ili mradi tu pia ndani ya kampuni kuwepo mtaalamu aliyesomea uhandisi ngazi ya shahada ya kwanza.
  • Lazima kampuni ya ukandarasi kuwa na vifaa bora na vya kutosha kufanya kazi iliyojisajili kufanya kama mitambo, magari na vifaa.
  • Upana wa mkandarasi unaishia wapi maana kuna wale wa civil, mechanical, building, electrical, makandarasi specialist kama wa ICT, taa za airport , security n.k
  • mfuko wa CAF (Contractors Assistance Fund) kuwasaidia makandarasi ''wazawa'' kupata guarantee na kuwapatia mafunzo kama usimamizi wa mikataba n.k ili kushindana na makampuni ya kigeni ktk soko la tasnia ya ujenzi.

Source: Maisha ni Nyumba
 
Daraja la Mbutu kule Igunga, Tabora ilibidi makampuni 10 ya wazawa wajiunge pamoja joint-venture ili kukabiliana na changamoto za mradi wa daraja la Mbutu lililogharimu Shillingi Bilioni 10 za Kitanzania.

Mradi wa kiwanja kipya cha kimataifa cha ndege unaoendelea huko magharibi ya Tanzania kimeshatengewa zaidi ya Shilingi bilioni 30 za kitanzania ni mkandarasi mmoja tu ndiyo jina lake linajitokeza kuwa na ''uwezo'' bila kuwa na haja ya kusaidiwa/kuungana joint-venture na makampuni mengine ya Kitanzania.

Ikumbukwe ''Mayanga Contractors'' alikuwa mmojawapo wa wakandarasi kumi waliobidi kushirikiana kwa joint-venture kujenga daraja la Mbutu, Igunga mkoani Tabora, Tanzania kwa vile makampuni yote hayakuwa na uwezo wa kufanya mradi huo ''mkubwa'' bila kuomba nguvu za wengine..

Picha: Daraja la Mbutu, huko Igunga Tabora ni mradi mkubwa wa kwanza nchini kujengwa na Makandarasi wazalendo 10 waliojiunga pamoja kukabiliana na changamoto za kifedha, kiufundi na ujuzi, ambapo umekamilika kwa wakati kama matakwa ya mkataba yalivyohitaji.
 
Huyu hatoshindwa kumpachika mtu wa kumlinda kama walivyoshindwa JK na Ben
 
Back
Top Bottom