CHANGAMOTO ZA HII TAALUMA KWA SASA!
1.Makapuni ya vifaa tiba nchini!
Makampuni kama Anudha,Crown,pyramid,KASMEDICS,Bio-care,Pasific,Roche,e.t.c Hawa ndio wadau wa kuu wa vifaa tiba wanasupply vifaa ,wanafanya Installation na wanataka na kutengeneza vifaa iwe ni kazi yao ili biashara iendelee!Makapuni haya hayako tayari kumtrain Wala kutoa spare kwa Bio-Technician wa Hospitali husika! Kwa sababu hiyo vifaa Bio-Techinician anaonekana useless.Mwanzo Walikuwa wanahitajika sana Sasa baada ya wakuu wa Hospitali na vituo vya afya kuwa hitaji na serikali ikawapa ajira na baadaye wakaonekana hakuna lolote na hivyo gharama na hasara ina baki kuwa paleplale.
2.Uwezo wa ufundi mdogo,/Lack of enough skills from the training centre
3.Kutokuwepo kwa maduka ya electronics yenye spare za vifaa vya tiba!Kifaa kikiharibika kinahitajika spare ambayo huwezi kuipata kirahisi hapa Tanzania
4.Uongozi wa mbovu na dhaifu
5.Training zinazo tolewa hasa na nchi ya Korea kupewa wasio na sifa hasa mafundi walio soma veta na waliosoma Telecomunicaton na Electrical
Si Utani babu nimekukubali
Wewe ni Mtaaluma hasa kwenye uchambuzi huu,
Huwa nafikiria sana changamoto ya hali ya Maintenace ya hivi vifaa kwenye nchi za Africa hasa upatikanaji wa vifaa (spare parts) najua kuna wajanja kama hao uliowataja kutaka kuhodhi kazi za maintenace kwenye mahospitali ya Tz.
Nchi za nje, eg. UK kuna sheria kutoka Goverment agency i.e. MHRA, kwamba makapuni ya vifaa hivi ni lazima yatoe mafunzo ya ufundi kwenye vifaa vyao wanavyouza NHS, hakuna janja ya nyani kusema vikiharibika sisi wenyewe tutakuchaji kutenegeneza.
Kuhusu kozi huku wanataka degree yoyote ya engineering kwenye soko la ajira kupata kazi za Biomedical Engineering
Sababu zote ni principle zile zile in engineering, sababu University huku zinafundisha Multi discipline engineering courses kama BSc/BEng Electromechanical, Mechatronics, General Engineering kwa huku hizi ni nzuri kwa ajira sababu makampuni yoyote yanataka ujue zote Electrical, Electronics, Mechanical na Design engineering.
Wengi waliosomea Biomedical Engineering degree huku wanajikita kwenye makampuni ya research and development kugundua technology mpya ya vifaa ya matibabu
Mimi nilitoka na BSc/BEng Electromechanical Engineering, niko NHS, huku huwa kuna makampuni ya charity yananunua vifaa vilivyopita muda, kwa UK medical equipment mwisho miaka kumi kutumika kisheria, hizi kampuni huwa wanasema tuwape na spareparts zake kama zipo sababu hivi vifaa vikitolewa msaada Africa si muda wakirudi kuangalia progress wanakuta vimeswekwa store vimeharibika na hakuna namna ya kupata spareparts.