Makulaga,
Hili la udini mimi nalisikia kwenu.
Sababu ni kuwa hamkupata kusomeshwa historia ya Waislam katika kupigania uhuru wa Tanganyika.
Mkiamini Nyerere ndiye aliyefanya yote mliyokuwa mnaelezwa.
Nilipokuja na historia yenyewe ya uhuru mmeumia sana lau kuwa niliyoandika hakuna anaeweza kupinga kuwa si kweli.
Lakini katika vyuo vikuu nilivyoaliokuwa ndani na nje ya mipaka ya Tanzania, na katika wasomi waliokifanyia book review kitabu changu hakuna aliyenishutumu kwa udini.
Wote wamechukulia kitabu hiki kama ''Corrective History,'' yaani historia iliyosahihisha historia iliyokuwapo na ikaaminika.
Unatumia kipimo gani kujua kuwa ''natisha'' au ''sitishi?''