Binti wa Miaka Mitano Anayekaribia Kufariki Kwa Kula Sana | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Binti wa Miaka Mitano Anayekaribia Kufariki Kwa Kula Sana

Discussion in 'Matangazo madogo' started by MziziMkavu, Aug 16, 2009.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Aug 16, 2009
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,615
  Trophy Points: 280
  Suman Khatun Saturday, August 15, 2009 11:06 AM
  Mtoto mmoja wa kike wa miaka mitano wa nchini India humaliza kilo 10 za mchele, kilo tano za viazi na lita sita za maziwa kila wiki asipopewa chakula hupiga kelele na hupiga watu mawe. Madaktari wanahofia kuwa mtoto huyo anaelekea kufariki. Shuka mwisho wa habari hii kwa Picha zake.
  Madaktari nchini India wanahofia kwamba Suman Khatun, binti wa miaka mitano anayesumbuliwa na matatizo ya homoni yanayomfanya awe ana kula sana kuliko kawaida anaelekea kufariki kutokana na kula kwake sana.

  Suman Khatun anakula sana kiasi cha kwamba familia yake ambayo haina uwezo hulazimika kumnunulia kilo 10 za mchele, kilo tano za viazi na lita sita za maziwa kwaajili ya matumizi yake ya kila wiki.

  Hata hivyo chakula hicho huwa hakimtoshi na mtoto huyo huomba chakula cha ziada kutoka kwa majirani zake.

  Suman ana uzito wa kilo 75 na urefu wa mita moja. Familia yake ni masikini sana kiasi cha kwamba haina hata pesa za kuwawezesha kusafiri hadi mji wa Calcutta kwaajili ya matibabu yake.

  "Sisi wenyewe na watoto wetu wawili hatuwezi kujitosheleza kwa chakula, tunaposhindwa kumpa chakula, Suman hulia na hupiga kelele na wakati mwingine hutupiga na mawe" alielezea kwa huzuni mama yake, Belly Bibi, 33.


  GONGA HAPA KWA PICHA ZA MTOTO HUYO> http://www.nifahamishe.com/photos_news.aspx?topic=166&&NewsId=718
   
 2. M

  MzalendoHalisi JF-Expert Member

  #2
  Aug 16, 2009
  Joined: Jun 24, 2007
  Messages: 3,869
  Likes Received: 116
  Trophy Points: 160
  Mtoto huyu ..yaani kazi sana! Kama hamu ya kula inaazimika..basi angeniazima hapo kiasi tu ..maana hamu ya kula sina! Ha ha ha!
   
Loading...