A BIG BOX OF NOTHING
Member
- Sep 9, 2014
- 16
- 3
Mambo vipi jamiiforum members.
Bila shaka nyote mpo pouwaa na wazima sanaa! Nina rafiki yangu ana umri kama miaka 47 hivi tupo naye ofisi moja ijumaa aliyopita alikuwa na kihoja cha mwaka.
Ni kwamba, yeye alifiwa na mkewe kama miaka mitatu iliyopita alikuwa mwanamke wa kihehe kutoka Iringa ila walibahatika kupata watoto wawili wote wa kiume wanasoma primary.
Sasa baada ya kuishi ki-bachelor kwa muda wote huo akaamua kutafuta na kumpata mwanamke mwingine mjane lakini ambaye tayari ana binti mmoja mwenye miaka takribani 23 anayeishi naye.
Sasa huyu rafiki anasema kadri siku zinavyozidi kwenda huyo binti wake wa kufikia anakuwa anabadilika tabia kwa kasi sana.
Mwanzoni alikuwa kila asubuhi lazima binti atoe shikamoo, ila kwa sasa hakuna tena.
Anaweza kumwambia za asubuhi au akaamua kukaa kimya kabisaaa. Wanaweza kuwa wapo kwenye dinning table wanakula, ila mama mwenye nyumba akiinuka kidogo kwenda jikoni kufuata kitu, binti anaweza nyanyua kijiko cha "baba yake" huyo na kuanza kumlisha.
Binti anaweza kuvaa khanga moja tu, kisha akakaa sebuleni anaangalia TV (mpira) na baba yake mama akiwa amelala, kitu ambacho mwanzoni hakuthubutu hata kumsogelea.
Jamaa akiwa ofisini meseji kila wakati za kumjulia eti anaendeleaje na kazi.
Imekuwa too much hata saa ya kulala meseji inakuja "eti baba lala salama"kweli jamani hali hii?
Cha ajabu na kusikitisha kuliko yote, binti sasa anamuuliza eti kwa nini asiwachukue waende weekend moja trip ya Bagamoyo kuliko kukaa tu home anaboreka sana.
Yote hayo ni sehemu ndogo ya mkanda mzima wa vituko vya huyo kwa jamaa.
Mimi binafsi nilichomshauri ni kwamba amvutie tu pumzi na azidi kumvumilia, ila akiona hali inazidi kuwa mbaya achukue MAAMUZI MAGUMU kama liwalo na liwe.
Wadau mnashauri vipi.