Binti Siso


Idd Ninga

Idd Ninga

JF-Expert Member
Joined
Nov 18, 2012
Messages
2,603
Likes
1,003
Points
280
Idd Ninga

Idd Ninga

JF-Expert Member
Joined Nov 18, 2012
2,603 1,003 280
?type=3BINTI SISO
1)Ukweli toka moyoni,kuvumilia siwezi
Ameingia rohoni,kanifanya kuwa chizi
Ila shida masikini,ngemfata mpaka Swazi
Huyu binti binti Siso,Kumwambia natamani.

2)Kumwambia natamani,nataka kumwambia wazi
Ningenda kwao nyumbani,sipendi penzi la wizi
Linitie matatani,kichwani nipigwe nazi
Huyu binti binti Siso,abaki kwetu nchini.

3)Abaki kwetu nchini,mwachini awe mwangazi
Aingie kwangu ndani,aniite laazizi
Anitie furahani,awe wangu mwangalizi
Huyu binti binti Siso,kumuoa natamani.

4)Kumuoa natamani,sghida mahari ni ghali
Eti ngombe themanini,tena wote mafahali
Nawaza nifanye nini,nataka ndoa halali
Huyu binti binti Siso,nimpe mahari gani

5)Nimpe mahari gani,nionekane jabali
Yeye ataka kidani,shida wazazi wakali
Bila ngombe themanini,ndoa niitupe mbali
Huyu binti binti Siso,nimtoroshe mjini.

6)Nimtoroshe mjini,nimpeleke kijiji
Mzuri toka kicwani,mimi kwake sina hali
Nilimuona ndotoni,haikuwa afadhali
Huyu binti binti Siso,lolote kwake sijali

SHAIRI=Binti Siso
MTUNZI=Idd Ninga wa Tengeru Arusha
+255624010160
iddyallyninga@gmail.com
 
Idd Ninga

Idd Ninga

JF-Expert Member
Joined
Nov 18, 2012
Messages
2,603
Likes
1,003
Points
280
Idd Ninga

Idd Ninga

JF-Expert Member
Joined Nov 18, 2012
2,603 1,003 280
Asante sana
 
BangiNyeusi

BangiNyeusi

JF-Expert Member
Joined
Jul 14, 2016
Messages
438
Likes
477
Points
80
Age
22
BangiNyeusi

BangiNyeusi

JF-Expert Member
Joined Jul 14, 2016
438 477 80
Ni zuri saana napenda mambo haya ushairi na riwaya, hongera iddy
 

Forum statistics

Threads 1,236,727
Members 475,218
Posts 29,267,442