Binti mchepuko zingatia

miss chagga

JF-Expert Member
Jun 7, 2013
57,821
48,976
Habari zenu wana MMU mimi mzima wa afya .
Kuna kisa nimeshirikishwa kupitia njia nyingine za mawasiliano ambapo akanieleza kisa kina msibu sasa hivi yeye na mchepuko wake naweza sema ex mchepuko baada ya kuamua kurudi katika njia kuu… mwanaume yupo humu kwa heshima yako mkuu sitakutaja… binti nimeshaongea nae kaanza kuelewa .

Kisa chenyewe ni hiki jamaa alikuwa na mchepuko wake japo ana familia yake na anaipenda pia ila kuna kutoelewana kulitokea ndani ya nyumba akaamua kuchepuka kutuliza mawazo, japo aliongeza gharama zilikuwa kubwa ha hahaha a nacheka ningemtimua mie sitaki kuwa na mwanaume mchepuko huna hela..

Sasa akaamua kumwambia binti wakati wa sikukuu naomba tuachane endelea na maisha yako mi narudi kwenye familia yangu wacha weeee binti hakuamini sababu alikuwa kasha jimilikisha akijua she different from that wife of him…

Sasa binti kamwambia jamaa anataka kujiua na ameshajaribu once kujiua ndiyo nikaletewa nikamchamba etii oooh nimemwacha boyfriend wangu kisa huyu hahahaha mume wa mtu ni wa mtu tafuta wako …. Kutokana na haya naomba niwafundishe binti ambaye ni mchepuko weka akilini yafuatayo yatakusaidia kama yanavyonisaidia mimi :-

Mume mtu ni wa mtu hawezi kuwa wako hata awe kaburini tafuta wako ..
Usiache boyfriend wako kisa mume wa mtu ha hahaha we ni sawa na bambucha kwa bata tu lakini lazima atarudi kwa mkewe one day sasa wewe leta dharau kwa vipesa vidogo ujione special ha hahaha we jijue utatemwa mda wowote. HESHIMU BOYFRIEND WAKO NA UMRI HAUSIMAMI NA WAZURI WANAZALIWA KILA SIKU.

Usimpende mume wa mtu kwa moyo wako wote sababu we hakupendi zaidi anakudanganya anakupenda ili akukule tu na akisha choka hicho kidude ujue unatemwa…KUWA EXPENSIVE USIKUBALI KULIKA KILA SEHEMU

Usitembee na mwanaume wa mtu anayemdharau mke wake ukadhani we ni special its just a matter of time ipo siku na wewe atakudharau tu..KARMA IS A BITCH

Usimzalie mume wa mtu kwa kigezo cha kuwa ili awe na wewe ha haha mimba ikifikisha miezi mitano ni kichefu chefu kwake ankutafutia mchepuko mnakuwa watatu Timu inazidi kuongezeka kuwa makini…..BINTI MIAKA HAISIMAMI UKISHAZAA MAJUKUMU HAYO HUWEZI TENA KULA NAYE BATA KILA BAR ATAKUAMBIA LEA MTOTO SASA HAPO ANATAFUTWA KIBINTI KIDOGO ZAIDI YAKO..

Mwanaume ambaye anakutunza wewe familia yake haijali ndugu machozi ya mkewe hayaendi bure kuwa hata mnafki sisitiza atunze familia yake ….

Waaume jitahidi kuwa wazi hata kwa vitendo kuwa familia yako ni muhimu kuliko yeye si anakupigia simu sa nane usiku upo tayari utoroke kitandani kwa wife ukaongee naye huko huo ni ufala …ACHENI KUTUKUZA MBUNYE.

Chepuka usiumize familia yako kama huna pesa za kutosha acha kuchepuka.
KUCHEPUKA SIYO SULUU YA MATATIZO NDANI YA NYUMBA ZAIDI UNAONGEZA SOLVE HALAFU CHEPUKA KWA UTASHI WAKO TU…….

Niwatakie kila la kheri mjirekebishe .
 
Haya mambo ingekuwa tunatumia akili hakuna ambae angelia

tatizo akili huwa haitumiki hapa

ni asuala ya mioyo na macho..
na wote tunajua macho hudanganya na mioyo ina ukichaa
nakubaliana na wewe the boss kwa binti watumie akili la sivyo watapoteza muda mwingi wengine kuishia kuwa masingle parents
 
Uzinzi ni matumizi ya demokrasia katika mapenzi, uzinzi unaanzia kichwani, kisha moyoni kabla hamjavuana pichu kitandani. Lakini wengi wanaishiaga kumlaumu shetani.
hakuna shetani hapo sababu ni jambo unapanga unanafasi kubwa sana ya kupangua sema ndiyo hivyo tena
 
Hivi unakubalije kuwa mchepuko...tena wa mume wa mtu...mh watu wana mioyooyani tupeane zamuu
 
Sikiliza nikuambie wewe Data. Mume Wa mtu kumpenda ni hatari...

Miss usipomtaja jina humu hatojirekebisha... So tutalajie msiba mwingine wa mwana JF
 
uyo dada kutaka kujiua sbbu ya mume wa mtu amekutana na dushe ya dhahabu au, Mungu anisamehe siwezi jiua sbbu ya mwanaume kama mapenzi yameisha acha maisha mengine yaendelee kuna maisha mengine bada ya mapenzi.
usipime kirahisi mapenzi ngoja uachike na uone nitakavyo kuwa nakuletea mapozi na dushe langu...
 
uyo dada kutaka kujiua sbbu ya mume wa mtu amekutana na dushe ya dhahabu au, Mungu anisamehe siwezi jiua sbbu ya mwanaume kama mapenzi yameisha acha maisha mengine yaendelee kuna maisha mengine bada ya mapenzi.
ha haha una wanawake wamejichoka kikweli hivi nikae na mume wa mtu mpaka mapenzi yanakuwa jua kali navumilia nini labda? mapenzi mapya yakiisha babu kula kona niache
 
Hivi mtu unajijua ni mchepuko unaanzaje kuzaa na mume wa mtu ili tu umvute awe karibu?

Unanikumbusha kisa kimoja, kuna mchepuko ulizaa na huyo kaka baadae mkewe akajua, mke akaleta sana vurugu akitaka asamehe basi mume awaandike mali zote watoto. Mwanaume akakubali,baada ya miezi 6 yule kaka alifariki kwa ajali ya kutatanisha. Yule mchepuko kabaki tu anaangaika na mtoto maana hakua na kazi, na huyu mama mpaka leo analea watoto wake na hataki hata kumsikia yule binti

Wanaume tulieni na wake zenu haijalishi mnapitia mapito gani kwenye ndoa yenu...tafuta jinsi ya kutatua hizo changamoto na sio kuongeza matatizo.
 
Miss chaga umenichekesha hapo ulipo Sema.. Ni ufala kutoka room kwenda nje kisa tu Unaogopa.. Huo ni ufala kweli.. Nime fikiria nimeona ni ufala kweli.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom