Binti kajisogeza baada ya kuhisi harufu ya madafu

Mecury

Member
Jan 5, 2013
83
40
Wataalamu habari zenu,

Kwanza kabisa mimi ni mmoja wa wahitimu wa chuo kikuu flani cha afya hapa mchini, kwa wasiofahamu ni kuwa ukimaliza masomo ya shahada ya baadhi ya kozi za afya huwa wahitimu hutakiwa kwenda kufanya mafunzo kwa vitendo ambapo walau tunapata mpunga flani hv/mwezi ktk muda wa miezi 12.

Sasa tuje kwenye mada kuu, miaka kama miwili hivi niliwahi kuwa na mahusiano na binti mmoja hivi nilimpenda ma yeye akanipenda tatizo alikuwa ni mtu wa virungu sana japo sio vikubwa kihivyo so niliweza kumvumilia, sasa katika harakati za maisha alikuja akapata msala kazini kwake akatimuliwa. Muda ukapita kidogo akapata mishe nyingine katika wilaya jirani na tulipokuwa tunaishi sasa katika kwenda huko mawasiliano yaliharibika kwa kiasi kikubwa na kupelekea uhusiano kudorora kabisa, tukawa kama marafiki na sio kama wapenzi siwezi kumlaumu yeye kwani kwa kiasi kikubwa nilichangia kuharibika kwa mahusiano yetu kwani mimi ni MTU introverted sana.

Sasa ikawa tunawasiliana mara moja moja sana, akawa amerudi mjini mapema mwaka huu sasa, tukaendelea kuwasiliana lakini kama marafiki wa kawaida. Nikajikuta natamani turudi kama tulivyokuwa mwanzoni. Sasa nikamweleza binti, chakushangaza binti akawa anaringa sana mara atake zawadi na tena anapendekeza iwe ya aina gani na ya gharama kweli kweli ama akiwa na shida ndo aje getto afu hataki hata nimshike mkono.

Sasa maajabu mwezi wa nane kipindi nakaribia mitihani yangu ya mwisho kabisa chuoni. Sasa binti akaanza kujilegeza mwenyewe simu nyingiiii anakuja getto bila sababu zozote za msingi mara aseme anataka mtoto mara aseme anataka tuishi pamoja wakati mwanzoni alikuwa kuja getto mpaka zawadi afu anakaa umbali wa mita moja hataki kuguswa, sasa mimi huwa na mzungusha hv make kumla napenda lakini kumuoa sasa nashindwa kabisa kwani nimemuona kama kawa kama mbangaizaji hivi siku hizi.
 
Muoe tu si kakupenda,,,be Care ukikosea kujenga utabomoa utaanza upya lakin ukikosea kuoa utajuta...tafuta mke kwa kumshirikisha Mungu usidandidandie ovyo utakuja kujuta rafiki
 
Acha tamaa dogo hakika ukimtia mimba huyo bint utajutaaa maisha yako yoootee
Huyo amefuata pesa sasa anakulaghai uone unapendwa
Tulia muombe Mungu akupe mke acha tamaa
 
Mpaka umekuja kububujikwa huku niwazi kuwa unapenda huyo binti na hauna namna unaomba ushauri tu.

Fanya hivi muoe
 
Mtu mkimya, mwenye aibu na asiyependa maongezi au tunawaita anti social.

Mara nyingi watu kama hawa huwa MAJASUSI, watu wasiojulikana, watu wenye akili nyingi sana.
Ahaa sawa, nahisi ugonjwa huo unaninyemelea ni Ugonjwa Actually
 
Acha tamaa dogo hakika ukimtia mimba huyo bint utajutaaa maisha yako yoootee
Huyo amefuata pesa sasa anakulaghai uone unapendwa
Tulia muombe Mungu akupe mke acha tamaa
Kabisa asee make mwanzoni nilihisi sasa kama anataka kunibambikizia mimba make alikua akija analala kabisa afu natumia kinga huku yeye anakuwa ana raha kabisa. Sema natafuta njia ya kumuacha kistaarabu kabisa.
 
Wataalamu habari zenu,
Kwanza kabisa mimi ni mmoja wa wahitimu wa chuo kikuu flani cha afya hapa mchini, kwa wasiofahamu ni kuwa ukimaliza masomo ya shahada ya baadhi ya kozi za afya huwa wahitimu hutakiwa kwenda kufanya mafunzo kwa vitendo ambapo walau tunapata mpunga flani hv/mwezi ktk muda wa miezi 12.
Sasa tuje kwenye mada kuu, miaka kama miwili hivi niliwahi kuwa na mahusiano na binti mmoja hivi nilimpenda ma yeye akanipenda tatizo alikuwa ni mtu wa virungu sana japo sio vikubwa kihivyo so niliweza kumvumilia, sasa katika harakati za maisha alikuja akapata msala kazini kwake akatimuliwa. Muda ukapita kidogo akapata mishe nyingine katika wilaya jirani na tulipokuwa tunaishi sasa katika kwenda huko mawasiliano yaliharibika kwa kiasi kikubwa na kupelekea uhusiano kudorora kabisa, tukawa kama marafiki na sio kama wapenzi siwezi kumlaumu yeye kwani kwa kiasi kikubwa nilichangia kuharibika kwa mahusiano yetu kwani mimi ni MTU introverted sana.
Sasa ikawa tunawasiliana mara moja moja sana, akawa amerudi mjini mapema mwaka huu sasa, tukaendelea kuwasiliana lakini kama marafiki wa kawaida. Nikajikuta natamani turudi kama tulivyokuwa mwanzoni. Sasa nikamweleza binti, chakushangaza binti akawa anaringa sana mara atake zawadi na tena anapendekeza iwe ya aina gani na ya gharama kweli kweli ama akiwa na shida ndo aje getto afu hataki hata nimshike mkono.
Sasa maajabu mwezi wa nane kipindi nakaribia mitihani yangu ya mwisho kabisa chuoni. Sasa binti akaanza kujilegeza mwenyewe simu nyingiiii anakuja getto bila sababu zozote za msingi mara aseme anataka mtoto mara aseme anataka tuishi pamoja wakati mwanzoni alikuwa kuja getto mpaka zawadi afu anakaa umbali wa mita moja hataki kuguswa, sasa mimi huwa na mzungusha hv make kumla napenda lakini kumuoa sasa nashindwa kabisa kwani nimemuona kama kawa kama mbangaizaji hivi siku hizi.
Huyo si mwanamke wa kuoa my friend...hilo ni bomu
 
Muoe tu si kakupenda,,,be Care ukikosea kujenga utabomoa utaanza upya lakin ukikosea kuoa utajuta...tafuta mke kwa kumshirikisha Mungu usidandidandie ovyo utakuja kujuta rafiki
Ahsante kwa ushauri wako mzuri rafiki.
 
Huyo si mwanamke wa kuoa my friend...hilo ni bomu
Duh make amenibadirikia ghafla yani sasa hv anajifanya mwemaa yani nikimkanya kitu hata kabla sijamaliza anaomba msamaha haraka sana ila mi namcheki tu anavyoigiza.
 
Huyo kuwa rafiki naye kawaida au la.pasha kiporo tu.Ukioa umekwishwa.Kumbuka wagonjwa na taifa vinakuhitaji usikumbatie gaka hilo
 
Maamuzi yako kichwani mwako mkuu,ukiona utapata faida nyingi kuliko hasara oa,ila ukiona hasara ni nyingi kuliko faida piga chini.
 
Hata siku moja usirudiane na demu aliyekuacha kisa huna pesa.Kaenda kutafuta kakosa ndio maana kakurudia labla baada ya kuona umepata hvyo siku na mwenye pesa kukuzid atakusumbua na kukuacha
 
Back
Top Bottom