MUBENDE
JF-Expert Member
- Nov 11, 2022
- 705
- 1,200
Haya mambo yasikie tu yasikutokee ktk familia yako, yanaumiza sana kwakweli na sema hivyo kutokana na uzoefu wangu na ninachokipitia. Tumshukuru na kumtumainia Mungu hawa watoto wa miaka hii ni hatari sana ktk kuyanakili ya ulimwengu kuliko kusikiliza wazazi.Mwanafunzi wa kidato cha tatu wilayani Arumeru mkoani Arusha mwenye umri wa miaka 15 ambaye alitoroka nyumbani kwao kwa zaidi ya siku 30, amerejea akiwa na ujauzito na kudai amefukuzwa na fundi Gereji aliyekuwa anaishi naye Kinyumba mkoani Kilimanjaro.
Mwanafunzi huyo aliyetoroka na baadae kutuma ujumbe kwa njia ya simu, ukisema asitafutwe yupo sehemu salama na anatafuta maisha, amedai ametimuliwa baada ya fundi huyo kuona taarifa GADI TV ikisema kuwa anatafutwa.
Familia imesema inaendelea kumuhoji mwanafunzi huyo na baadae hatua nyingine zitafuata.