Binti hamtaki Mama Mzazi

Binti hamtaki Mama Mzazi

pare girl

New Member
Joined
Jan 6, 2015
Posts
4
Reaction score
0
Habari zenu jamani,mimi ni Mgeni humu ,kuna jambo nataka niwashirikishe labda na nyie mtalichukuliaje?.kuna dada mmoja anaishi na Baba yake Mzazi na Mama wa Kambo,Maisha yake yote yalikuwa ya mateso kutoka kwa Mama wa Kambo,lakin ialivumilia akafika Chuo huyo Mama akafanya Fitina waKamfukuza wakamwambia aende kwa Mama yake Mzazi basi Likizo

ikiisha anawasiliana na Mama mzazi anamtafutia pa kukaa Dar es Salaam kwa sababu Mama yake yupo huko Vijijini basi Binti kapata Mchumba kawaambia Baba yake Mama wa Kambo kuskia Binti kanaolewa akamtafuta akamuomba Msamaha arudi Nyumbani.akarudi maandalizi yakaanza Kichern Party na Sendoff Mama Mzazi akakatiliwa asiende maan huyo Mama wa kambo alisema atafanya kitu mbaya Mama Mzazi akienda.

Binti akakubali Mama Mzazi asiende.na kuanzia hapo Binti akawa hataki mawasiliano na Mama mzazi hajibu sms wala kupokea cm.sasa harusi inakuja binti anasema kwenye harusi hatamtambulisha Mama Mzazi atamtambulisha huyu Mama wa kambo.kibaya anadiriki kusema Mama Mzazi kajitakia mwenyew asingemzaa nje ya ndoa,jamn hebu wamama ndo wanastahili adhabu hii?
je angeitoa je?
amesahau kwenye shida Mama Mzazi ndo alikuwa mkombozi wake.

Mama ake anaogopa kwenda kwenye harusi binti hamtaki mpaka kaanza kuumwa kwa sababu ya Mawazo?
hii si laana jamani,nawasilisha.
 
Huyo binti anatafuta laans, kama upo karibu na mama yake mzazi mshauri atulie ndoa ifungwe walw asihangaike nao hao mabaradhuri. Mungu huwa anatoa adhabu hapa hapa dunianj,
 
Oh my Kweli mwisho Wa dunia . Poor my mother, Mungu amtie nguvu na kumpa moyo Wa kusamehe. Thanks!
 
Mama wa waru ajitulize zake.

Binti dunia itamfunza tu

yaani anatia huruma,na hivi anavidonda va tumbo bac ndo vimezidi.binti akiambiwa anauliza sasa yeye afanyeje.mhuu hizi laan tunajitafutia wenyeww
 
yaani anatia huruma,na hivi anavidonda va tumbo bac ndo vimezidi.binti akiambiwa anauliza sasa yeye afanyeje.mhuu hizi laan tunajitafutia wenyeww

Aisee.....

Una uhakika hakuna kingine hapo katikati kati ya mama na mtoto? Mara nyingine ni vyema pia kusikia upande wa pili. Waeza kuta mama wa kambo amemfanyia makubwa sana huyo binti na yote mnayoambiwa ni fitna. Kumbuka, si mama wote wa kambo ni makatili.

Sikilizeni na upande wa pili..... Japo hiyo haihalalishi binti kumkana mama yake mzazi bali inaweza kuleta suluhisho.
 
Huyu binti naona anajichumia laana au Yule mama kwa kambo keshaenda ule upande wa pili kufanya mambo, who knows
 
aisee huyo mama wa kambo anaroho mbaya mpaka ndugu zake wa tumbo moja hawampendi na ndo wanamwambia mama ake mzazi asali sana.na mashemeji zake hawampendi .kiujumla huyo mama ndugu wa tumbo moja mpak mashemeji haziivi kwasababu ya roho mbaya.hata mama mzazi wa huyo mama zilikuwa haziivi maana anakataz wajukuu wasiende kumsalimia.
 
Huyu binti naona anajichumia laana au Yule mama kwa kambo keshaenda ule upande wa pili kufanya mambo, who knows

bwana wew umo mule mule,maan binti alikuwa hayupo hivo.na kabla ya hapo alikuwa anamwambia mama ake anavumilia tu shule iishe arudi kwa mama ake,sa hivi ndo labadilika hataki kumsikia mama ake
 
Huyo mama atulie tuli. huyo bidada yeye ni mwanamke, ajue yapo njiani yanakuja ataikumbuka hadi siku mama yake alipokuwa labour.
 
Habari zenu
jamani,mimi ni Mgeni humu ,kuna jambo nataka niwashirikishe labda na
nyie mtalichukuliaje?.kuna dada mmoja anaishi na Baba yake Mzazi na Mama
wa Kambo,Maisha yake yote yalikuwa ya mateso kutoka kwa Mama wa
Kambo,lakin ialivumilia akafika Chuo huyo Mama akafanya Fitina
waKamfukuza wakamwambia aende kwa Mama yake Mzazi basi Likizo

ikiisha anawasiliana na Mama mzazi anamtafutia pa kukaa Dar es Salaam
kwa sababu Mama yake yupo huko Vijijini basi Binti kapata Mchumba
kawaambia Baba yake Mama wa Kambo kuskia Binti kanaolewa akamtafuta
akamuomba Msamaha arudi Nyumbani.akarudi maandalizi yakaanza Kichern
Party na Sendoff Mama Mzazi akakatiliwa asiende maan huyo Mama wa kambo
alisema atafanya kitu mbaya Mama Mzazi akienda.

Binti akakubali Mama Mzazi asiende.na kuanzia hapo Binti akawa hataki
mawasiliano na Mama mzazi hajibu sms wala kupokea cm.sasa harusi inakuja
binti anasema kwenye harusi hatamtambulisha Mama Mzazi atamtambulisha
huyu Mama wa kambo.kibaya anadiriki kusema Mama Mzazi kajitakia mwenyew
asingemzaa nje ya ndoa,jamn hebu wamama ndo wanastahili adhabu hii?
je angeitoa je?
amesahau kwenye shida Mama Mzazi ndo alikuwa mkombozi wake.

Mama ake anaogopa kwenda kwenye harusi binti hamtaki mpaka kaanza kuumwa
kwa sababu ya Mawazo?
hii si laana jamani,nawasilisha.

maskini wengine tunaomba sku ya kuolewa mama mzazi awepo huyu haoi ilo? siku moja atatoa chozi kwa ilo. afu amtafte mtu ambae kafiwa na mama amweleze uchungu alonao. nan kama mama????
 
Kama haitakua ni story basi uyo mama nampa pole na binti+mama wa kambo+baba yake wote watapata wanachostahili hapa duniani

Sent from my BlackBerry 9320 using JamiiForums
 
Huyo binti ana hasira na mama yake kwasababu kama alipata manyanyaso kwa mama wa kambo yeye anaamini mama yake ndo aliyesababisha kwasababu ndo aliyemuacha aishi kwenye mazingira aloishi. Which is true. Badala ya huyo mama kulalamika atafute mwanya wa kuongea na binti yake amueleze sababu za yeye kumuacha kwa baba
yake pengine atamuelewa na kumuonea huruma.

Ye binti karudi kwa mama wa kambo kwasababu anajua pamoja na yote MAMA WA KAMBO NDO ALIYEMLEA na sio mama yake mzazi.
 
aisee huyo mama wa kambo anaroho mbaya mpaka ndugu zake wa tumbo moja hawampendi na ndo wanamwambia mama ake mzazi asali sana.na mashemeji zake hawampendi .kiujumla huyo mama ndugu wa tumbo moja mpak mashemeji haziivi kwasababu ya roho mbaya.hata mama mzazi wa huyo mama zilikuwa haziivi maana anakataz wajukuu wasiende kumsalimia.

Mlijuaje yote hayo?

Isije ikawa mtu mmoja mwenye chuki naye anamchafua tu.

Swali dogo: Huyo binti aliyefanyiwa ubaya na mama wa kambo... kiasi cha kumchongea mpaka akafukuzwa chuo.... ikatokea kwa jitihada za mama mzazi binti kasoma mpaka kamaliza chuo..... Inakujia akilini kweli binti wa umri huo na elimu hiyo asiujue ubaya wa mama yake wa kambo kiasi cha kumkumbatia na kumtosa mama yake aliyemsaidia wakati wa shida??

Kaswali kengine: Nini kimemfanya huyu mama ea kambo kujipendekeza kwa binti kwa kuwa kapata mchumba? Anaolewa na mtoto wa Rugemalira au Prof Tibaijuka?
 
Habari zenu jamani,mimi ni Mgeni humu ,kuna jambo nataka niwashirikishe labda na nyie mtalichukuliaje?.kuna dada mmoja anaishi na Baba yake Mzazi na Mama wa Kambo,Maisha yake yote yalikuwa ya mateso kutoka kwa Mama wa Kambo,lakin ialivumilia akafika Chuo huyo Mama akafanya Fitina waKamfukuza wakamwambia aende kwa Mama yake Mzazi basi Likizo

ikiisha anawasiliana na Mama mzazi anamtafutia pa kukaa Dar es Salaam kwa sababu Mama yake yupo huko Vijijini basi Binti kapata Mchumba kawaambia Baba yake Mama wa Kambo kuskia Binti kanaolewa akamtafuta akamuomba Msamaha arudi Nyumbani.akarudi maandalizi yakaanza Kichern Party na Sendoff Mama Mzazi akakatiliwa asiende maan huyo Mama wa kambo alisema atafanya kitu mbaya Mama Mzazi akienda.

Binti akakubali Mama Mzazi asiende.na kuanzia hapo Binti akawa hataki mawasiliano na Mama mzazi hajibu sms wala kupokea cm.sasa harusi inakuja binti anasema kwenye harusi hatamtambulisha Mama Mzazi atamtambulisha huyu Mama wa kambo.kibaya anadiriki kusema Mama Mzazi kajitakia mwenyew asingemzaa nje ya ndoa,jamn hebu wamama ndo wanastahili adhabu hii?
je angeitoa je?
amesahau kwenye shida Mama Mzazi ndo alikuwa mkombozi wake.

Mama ake anaogopa kwenda kwenye harusi binti hamtaki mpaka kaanza kuumwa kwa sababu ya Mawazo?
hii si laana jamani,nawasilisha.

Ningekuwa karibu ningemcharaza fimbo huyo binti. Mama aliyembeba tumboni miezi 9 leo hamthamini.

Huyo dada akijakupata mtoto naye akaitwa mama, ataelewa ukubwa wa kosa analolifanya sasa.
 
Huyo binti ana hasira na mama yake kwasababu kama alipata manyanyaso kwa mama wa kambo yeye anaamini mama yake ndo aliyesababisha kwasababu ndo aliyemuacha aishi kwenye mazingira aloishi. Which is true. Badala ya huyo mama kulalamika atafute mwanya wa kuongea na binti yake amueleze sababu za yeye kumuacha kwa baba
yake pengine atamuelewa na kumuonea huruma.

Ye binti karudi kwa mama wa kambo kwasababu anajua pamoja na yote MAMA WA KAMBO NDO ALIYEMLEA na sio mama yake mzazi.

Heri ya mwaka mpya mpenzi....

Mi siamini kama hii stori iko balanced. Kuna kitu kinafichwa hapa afu jumba bovu anarushiwa mama wa kambo. Hii dhana mama wa kambo si mama wanawake mnatakiwa muiangalie kwa upande wa pili..... mchawi wa mwanamke ni mwanamke.

Ukiangalia hii stori imeandikwa na ndugu wa upande wa mama mzazi.... soma katikati ya mstari utagundua mama anarudisha majeshi baada ya kuona binti kishaanza kupata maisha katika mwanga bora.
 
Back
Top Bottom