Je, ni sahihi kwa baba wa kambo na baba mzazi (biological father) kwa pamoja kuhudhuria katika sherehe ya harusi ya binti yao? Ni busara ipi itumike?

Infantry Soldier

JF-Expert Member
Feb 18, 2012
15,893
16,317
Habari za wakati huu kaka na dada zangu wote wa humu jamiiforums.

Ndugu zangu watanzania;

Je, ni sahihi kwa baba wa kambo na baba mzazi (biological father) kwa pamoja kuhudhuria katika sherehe ya harusi ya binti yao? Ni busara ipi itumike?

HIKI KISA NI KIREFU SANA ILA NINAOMBA KUANDIKA KWA UFUPI
==========
Kuna siku moja nilihudhuria katika mazishi ya binti mmoja wa miaka kama 21 alikuwa ni mwanafunzi wa chuo cha CBE. Huyu binti baba yake mzazi ni kutoka katika kabila la Wahehe ila mama yake ni mkurya. Huyu mama alizaa tu na Muhehe ila hakuolewa naye bali akaja kuolewa na Mkurya mwezie.

Huyu mama hakuwahi kumwambia baba mzazi (Mhehe) kuhusiana na mila za watu wa mkoa wa Mara kuwa kama mwanamke akizaa bila kuolewa, ikija ikatokea akaolewa basi yule aliyelipa mahari anamchukua mpaka na mtoto anakuwa wa ukoo wake. Siku ya mazishi baba yake mzazi alikuwepo ila baba yake wa kambo (Mkurya) hakuwepo kwa maana alikuwa Ulaya kwa masomo.

Baba yake mzazi ndio ikabidi aende kuweka shahada katika kaburi ingawa msalaha ulikuwa unasoma jina la yule baba wa kambo. Baba mzazi alikasirika sana siku hiyo kwa maana alitaka jina la katika msalaba lisomeke la ukoo wake.

(mfano; ELIZABETH MARWA BADALA YA ELIZABETH MSIGWA) kwa maana kwa mila za watu wa mkoa wa Mara, kama ambavyo nimeeleza hapo juu ni kwamba kama mwanamke akizaa bila kuolewa, ikija ikatokea akaolewa basi yule aliyelipa mahari anamchukua mpaka na mtoto anakuwa wa ukoo wake.

Nimejaribu kuvuta picha vp endapo kama huyu binti asingekufa mapema hivi? Vp kama angefanikiwa kufika umri wa kuolewa miaka labda 26 ingekuwaje katika siku ya sherehe?

Je, ni sahihi kwa baba wa kambo na baba mzazi (biological father) kwa pamoja kuhudhuria katika sherehe ya harusi ya binti yao? Ni busara ipi itumike? Ukifika muda wa bibi harushi kutambulisha wazazi wake atamtambulisha nani kama baba?

USISAHAU: ENDELEA KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USICHAFUE TASWIRA NJEMA YA TAIFA LAKO. USTAWI WA NCHI YETU UNAANZA NA WEWE. TIMIZA WAJIBU WAKO IPASAVYO.
 
Naomba urudie kuandika kwa ufasaha maana ukweli sijakuelewa, kuna sehemu unasema baba wa kambo alishakufa ila baba mzazi ndio yupo hapo nimeshidwa kuelewa samahani lakini
 
Sidhani kama kuna tatizo hapo.......ila huyo aliemwaga mbegu.......ikaota....alitunza kilichoota??,,, kama aliicha atunzie....hana haja ya kulalama.....

Hapo kwenye harusi......kuna mahali ifike ukubali matokeo....kumbukeni ni harusi ya mtoto...ni siku yake ya furaha......mukunyweee weeeee....maharusi wakitoka......mzichape kavu kavu....mshindi ndie anaepaswa kuwa BABA.....
 
Baada ya miaka 5 migongano ya namna hii itakuwa mingi sana maana vijana wa sasa wanazalisha na kuacha.

Kikwetu kama umezaa na mwanamke kisha mkaachana ili ummiliki mtoto inabidi ulipe faini. Ukishailipa basiii mtoto anakuwa wako.

Ila kwenye suala la sherehe mnatakiwa mtumie busara ya kibinaadam. Mzazi mwenzio kama ameolewa na wewe umeoa sio mbaya nyote mkihudhuria na kupeana sapoti kisha baada ya hapo kila mtu ashike njia yake.
Unforgetable
 
Baada ya miaka 5 migongano ya namna hii itakuwa mingi sana maana vijana wa sasa wanazalisha na kuacha.

Kikwetu kama umezaa na mwanamke kisha mkaachana ili ummiliki mtoto inabidi ulipe faini. Ukishailipa basiii mtoto anakuwa wako.
Hii Kilimanjaro nini mkuu?...
 
Hii Kilimanjaro nini mkuu?...
Kanda ya kati mkuu, yani huwezi kumzalisha binti kisha ukabeba mtoto, never.

Tena unatafuta wazee unaenda kunegotiate na upande wa mwanamke kabisa, mnayaweka sawa kisha unakuwa mzazi halali wa mwanao.

Wanafanya ivo ili pia kujenga undugu maana huyo mtoto anakuwa ni wa pande zote hivyo lazima wajenge connection.
Unforgetable
 
Naomba urudie kuandika kwa ufasaha maana ukweli sijakuelewa, kuna sehemu unasema baba wa kambo alishakufa ila baba mzazi ndio yupo hapo nimeshidwa kuelewa samahani lakini
Ulikuwa unasoma au unarukaruka tu kasema baba wa kambo alikuwa ulaya kimasomo sasa hii ya kufa umeitoa wapi kijana.
 
Back
Top Bottom