Binti alyemuua mamake kwa kumlazimisha kuolewa na asiyempenda, Mahakama yamhukumu miaka minne

Chachu Ombara

JF-Expert Member
Dec 11, 2012
6,042
10,787
Mahakama kuu kanda ya Dodoma imemhukumu Kashinje Nkanda mkazi wa kijiji cha Ujungu wilaya ya Iramba mkoa wa Singida adhabu ya kutumikia jela miaka minne baada ya kukiri kosa la kumuua mama yake mzazi, Ngembe Salum bila ya kukusudia.

Mshitakiwa Kashinje inadaiwa kutenda kosa hilo kutokana na kuchoshwa na tabia ya mama yake kumlazimisha aolewe na mwanaume ambaye alikuwa hampendi.

Pia Kashinje alipandisha jazba zaidi baada ya mama yake Gembe kumkataza kuuza ng’ombe ili apate fedha za kugharamia huduma kwa mganga wa jadi.

Awali mwendesha mashitaka na mwanasheria wa serikali mwandamizi, Seif Ahmed,alidai mbele ya Jaji Awadh Mohammed,kuwa mnamo Aprili, 27 mwaka 2011 muda usiojulikana huko katika kijiji cha Ujungu, Kashinje alimwua mama yake Gembe bila kukusudia.

Seif alisema kuwa mshitakiwa ambaye walikuwa wakiishi wawili tu yeye na mama yake,alimwua mama yake na kisha kuuficha mwili kwenye magunia ya mpunga.

“Baada ya kuuficha mwili huo wa mama yake,mshitakiwa alifunga mlango kwa nje na kufuli na kutokomea kusikojulikana,” alisema mwanasheria huyo wa serikali mwandamizi.

Alisema siku tatu baadae baada kutokea kwa mauaji hayo, majirani walipata hofu na mshituko kutokana na nyumba hiyo kufungwa kwa muda wa siku tatu mfululizo na wakazi wa nyumba hiyo kutokuonekana.

Seif alisema kutokana na mshituko huo majirani hao walitoa taarifa kituo cha Polisi na baada ya kufunguliwa kwa mlango,harufu kali ilitokea sehemu ambako magunia ya mpunga yalikohifadhiwa na walipokagua,ndipo walipouona mwili wa mama Gembe.

Mwendesha mashitaka huyo alisema kwa vile mwili huo haukuwa na majeraha yoyote moja kwa moja majirani walimhisi Kashinje ndiye amemuawa mama yake.Msako mkali ulifanyika na kufanikisha kwa mtuhumiwa Kashinje kukamatwa.Hata hivyo,taarifa ya daktari imeonyesha kifo cha Gembe kimetokana na kukosa hewa.

Kabla ya hukumu kutolewa, Seif alisema pamoja na mshitakiwa kukiri kosa kitendo alichokifanya mshitakiwa cha kumuawa mama yake,kwa utamaduni wa kiafrika na hasa Tanzania,hakikubaliki na wala hakipaswi kuonewa huruma.

“Kwa hali hiyo Mheshaimiwa Jaji naiomba mahakama yako tukufu impe mshitakiwa Kashinje adhabu stahiki ambayo licha ya kuwa funzo kwake mshitakiwa,pia iweze kuogofya watu wengine wanaotarajia kufanya kosa la aina hii,” alisema.

Kwa upande wake wakili wa mshitakiwa kutoka kampuni ya Ngongi &Advocates ya mjini Dodoma, Godwin Ngongi,aliiomba mahakama hiyo impe adhabu nafuu mteja wake, kwa madai kuwa hilo ni kosa lake la kwanza na amekaa mahabusu gerezani kwa miaka mitano.

Akitoa hukumu hiyo,jaji Mohammed alisema mahakama imezingatia maombolezo ya mshitakiwa kupitia kwa wakili wake,lakini kitendo alichokifanya mshitakiwa hakikubaliki na hivyo mshitakiwa atatumikia jela miaka minne ili iwe funzo kwake.
 
hivi hizi tabia za kulazimisha watoto zetu waolewe kisa unapata mbuzi na ngombe zitakoma lini aisee kuna majitu yana akili za kibwege sana haswa wanaume ndo wananganganiaga na pia haswa waswahili na vijinini tena haswa masikini mfyuuuu
 
Du five yrs kesi nyepesi hivi
ila unaona swa yeye akienda kubakwa na jianaume asilolitaka na madudu yooote yatayomkuta kule vumilie mchewwww kuolewa na lijitu ambalo hulipendi ukiwa na kaumri kidogo plus ndoto hapana aisee kill and god will understand
 
Kama Mshitakiwa Alikuwa AMEKIRI KOSA, Why Amekaa Mahabusu Kwa Miaka Yote Hiyo 5?!!!?? ALAFU Mleta UZI, Jaribu Kufanya Masahihisho Ktk Kichwa Chako Cha Hbr!!! KWA Mtiririko Wa Hbr Hii, ILITAKIWA Useme "ALIYEMUUA" SIO "AMUUA " Kwani Tukio Lenyewe Limeshatendwa Muda Mrefu Na Hukumu Imeshatolewa!!!
 
Kwa upande wake wakili wa mshitakiwa kutoka kampuni ya Ngongi &Advocates ya mjini Dodoma, Godwin Ngongi,aliiomba mahakama hiyo impe adhabu nafuu mteja wake, kwa madai kuwa hilo ni kosa lake la kwanza na amekaa mahabusu gerezani kwa miaka mitano.


Alikuwa vizuri kifedha kiasi cha kutafuta wakili
 
Aisee hiyo adhabu ni kubwa sana, kwanza amekaa mahabusi miaka mitano pili amepoteza mama mzazi, tatu inaonekana hana Ndugu wa maana wa kumsaidia
 
So kama rumnde 5yrs .a adhabu ni 4yrs, so she walks free na anaiday serikali 1yr au inakuwaje?
 
Back
Top Bottom