jamii01
JF-Expert Member
- Oct 1, 2010
- 1,988
- 1,437
Kuna msichana mmoja aliona maisha kuwa magumu sana, kila alichokuwa akikifanya alikuwa akikiona kushindikana jambo ambalo likaomfanya kukata tamaa. Kila alipokuwa akilitatua tatizo hili, kuna tatizo jingine lilikuwa likiinuka jambo ambalo lilikuwa likimchanganya sana. Hakutaka kuendelea kuishi maisha ya namna hiyo, alichoamua kukifanya ni kumfuata mama yake na kisha kumuelezea matatizo ambayo alikuwa akikutana nayo. Sauti yake tu, ilisikika kama mtu aliyekuwa amekata tamaa na kutokata kuendelea na maisha yake.
Mama yake hakusema kitu, alichokifanya ni kumchukua na kumpeleka jikoni. Akachukua maji na kuyaweka jikoni, yalipocheka, akachukua karoti akaziingiza katika maji yale, akachukua mayai na kuyaingiza katika maji yale na mwisho kuchukua kahawa na kisha kuiingiza katika maji yale bila kusema kitu chochote kile.
Kila kitu kilipokuwa tayari, akayatoa mayai yale katika maji yale na kisha kutoa karoti zile katika maji yale na kisha kumuuliza 'UMEONA NINI?'
"Nimeona karoti, mayai na kahawa" Alijibu.
Alichosema mama yule ni kumtaka binti yake aziguse karoti zile, binti alipozigusa, akagundua kwamba karoti zimekuwa laini sana. Hakuishia hapo, akamtaka ayachukue mayai yale na kutyavunja. Yule binti alipoyavunja, akagundua kwamba yamekuwa magumu tofauti na kipindi ambacho hayakuwa yameingizwa ndani ya maji yale yaliyokuwa yakichemka. Mwanamke yule hakuishia hapo, akamwambia aonje maji yale ambayo yalikuwa yameibgizwa kahawa, alipoyaonja, akayahisi yamebadilika radha na kuwa tamu sana.
"Unamaana gani kufanya haya yote mama?" Msichana yule alimuuliza mama yake ambaye akaanza kumjibu.
"Kabla sijaweka karoti ndani ya maji, zilikuwa ni ngumu sana ila baada ya kuziweka ndani ya maji yanayochemka, zikabadilika na kuwa laini sana. SIkuishia hapo, nilichokifanya ni kuyachukua mayai na kisha kuyaweka ndani ya maji yanayochemka, kilichotokea, mayai yale ambayo yalikuwa laini, yakabadilika na kuwa magumu. Nilipoweka kahawa ndani ya maji, matokeo yake kahawa ile ikabadilisha maji yote. Kumbuka kwamba vitu hivyo vitatu vimepitia katika kitu kimoja, maji yaliyokuwa yakichemka. Hebui niambie binti yangu, wewe ni nani? Karoti, yai au kahawa?"
Wote tunapitia katika matatizo mbalimbali. Hatutakiwi kuwa karoti kwamba tunapopitia humo tunakuwa laini na mwisho kukata tamaa, wote tunatakiwa kuwa kama yai, tunaingia humo kwenye matatizo tukiwa legevu lakini mara tunapoyashinda tunakomaa na kuwa wenye nguvu na wagumu. Ila pamoja na hayo yote, katika kipindi ambacho tunapitia katika matatizo mbalimbali yatupasa kuwa kahawa zaidi, kwa kupitia matatizo yetu basi marafiki zetu wote wanaotuzunguka waweze kubadilika kupitia sisi na hata wakati mwingine kuwabadilisha wale ambao wametufanya sisi kuingia katika matatizo hayo.
HEBU KUWA MUWAZI, UNAPOINGIA KWENYE MATATIZO WEWE HUWA NANI? KAHAWA, YAI AU KAROTI?
KAMA UMEIPENDA, SHARE NA WENGINE WAIONE ILI WAWEZE KUJITAMBUA WAO NI NANI NA KAMA INAWEZEKANA WAWEZE KUBADILIKA.​