Mpauko
R.I.P
- Jan 19, 2019
- 2,323
- 3,353
BINAMU YANGU-01
ROBIN MIHO
0776741545
Ni saa tatu usiku mvua ya wastani ilikuwa ikinyesha taratibu huku upepo ukivuma hapa na pale,nilifumbua macho kivivu na kugundua ya kwamba nilikuwa nimesinzia kochini sebuleni kwangu,nikatupa mkono kujaribu kumpiga mbu aliyekuwa akijipatia shibe mguuni lakini bahati ilikuwa ni yake nikamkosa na kuachia msonyo mdogo huku nikijikuna.
Nikajizoa zoa kuingia chumbani na kujibwaga kitandani,zilipita dakika chache tu kabla simu yangu haijaanza kuita kwa fujo nikafumbua jicho moja na kutupa mkono chini ya mto kuitafuta simu yangu nikaipeleka sikioni bila hata ya kutazama mpigaji ni nani,chezea usingizi wewe!
"Haloo" niliita
"Haloo hujambo mwanangu?"
"Sijambo mama shikamoo"
"Marahaba mwanangu umeshaanza likizo?"
"Ndio mama nineanza jana"
"Oohh mwanangu kesho uje nyumbani mara moja"
"Kuna nini tena mamaaa"
"Baba yako anataka umsindikize nyumbani kwa babu yako maana anaumwa"
"Lini mama?"
"Keshokutwa mwanangu anahitaji kuwahi kumuuguza babu yako na huu uzee wa baba yako hatoweza kuendesha gari hadi Mufindi"
"Sawa mama basi nitakuja kesho"
"Sawa mwanangu uwe na usiku mwema"
"Nanyi pia mama"
Baada ya simu kukatika na usingizi ukawa umeshakata hivyo nikaamua kuanza kupanga nguo zangu kwa ajili ya safari ya ghafla ya Mufindi.
Ni takribani miezi nane tu tangu niajiriwe katika benki ya National Microfinance Bank (NMB) kama meneja mwandamizi hivyo nikahama kwa wazee wangu mtaa wa uhuru na kupanga nyumba ndogo ya vyumba vitatu mtaa wa Mbuyuni.
Baada ya kuridhishwa na maandalizi yangu nikatoka kwenda kutafuta chakula maana nilikuwa mvivu kweli kweli kwenye suala la kupika chakula,nilijizoesha kupikiwa na mpenzi wangu Ezelina ambaye tuliachana baada ya kukorofishana hapa na pale tukaamua tu kusitisha mahusiano ingawaje nilikuwa bado nanpenda lakini glasi ikivunjika hata iunganishwe vipi bado haitoweza kuwa kama ilivyokuwa mwanzo.
Hatimaye siku ya safari ikawadia,tuliamua kuondoka saa nne asubuhi kwa gari ndogo ya baba yangu mzee Maliki aina ya Rav 4 old model nyeupe,niliendesha kwa umakini wa kutosha uliotufikisha Mufindi saa mbili na dakika kadhaa usiku,tulifikia kwa babu na bibi mzaa baba,ingawaje babu hakuwepo,alikuwa hospitalj na tukapanga kwenda kumuona kesho yake.
Nyumba ya babu ilikuwa ni kubwa na yenye vyumba vingi vya kutosha,mimi nilipewa chumba kilichojitegemea kwa nje huku baba yangu Mzee maliki akilala katika vyumba vilivyopo ndani kabisa ya jengo lile kubwa la matofari ya kuchoma,pengine inaweza kuwa nyumba nzuri kuliko nyingi ya nyumba kadhaa za kijiji hiki.
Asubuhi ya siku iliyofuata tulijihimu kwenda hospitali kwani ilikuwa mbali takribani mwendo wa masaa matatu hivi,tuliondoka watu watatu mimi baba na bibi mzaa mama,saa tatu kasoro ilitukuta mbele ya hospitali ya mafinga,hali ya babu haikuwa ya kuridhisha sana ingawaje ilikuwa nafuu ya jana,hadi inatimu saa tisa mchana,baba yangu mzee Maliki aliamua kubaki hospitali na kuniambia nitangulie kijijini pamoja na bibi mzaa mama.
Baada ya kuondoka hospitali masaa mawili tu yalitosha kutufikisha Igowole ambapo bibi aliomba nimuache pale akamsalimu mjomba,ilikuwa ni takribani dk 40 hivi kwa gari kabla ya kuingia kijijini kwetu,baada ya kumwacha sasa nilikanyanga mafuta kuwahi kijijini.
Sijui ni nini kilichonisukuma kuyatupa macho yango pembeni ya barabara alikuwepo binti mmoja mrefu kiasi,maji ya kunde,kifua kidogo na kalio la kutosha kumvutia mwanaume yeyote yule rijali,alikuwa amejitwisha kiroba akitembea kwa haraka kuelekea kule kule nilikokuwa nikielekea.
Nikajikuta nikipunguza mwendo na hatimaye nikasimama na kushusha kioo,nikampungia mkono wa kumwita,mwanzo alisita lakini akasogea dirishani na kunikazia macho kumaanisha alikuwa akinisikiliza.
Ukweli alikuwa ni mzuri sana,midomo minene iliyoumbika vizuri,macho makubwa na uso wa mviringo ulionakshiwa na muonekano wa hurumahuruma hivi,namna gani sasa nilijikuta nikiduwaa kwa sekunde chache huku mapigo ya moyo yakinienda mbio.
"Shikamoo" binti alisalimia baada ya kuona nikiwa nimezubaa.
"Eh.. Marahaba hujambo"
"Sijambo"
"Samahani hivi hospitali ya wilaya iko wapi?"
"Mmh iko hukohuko ulikotoka mbona"
"Eeh ni huku aisee... Inachukua muda gani kufika huko?"
"Ni kama masaa matatu hivi" alijibu huku akikwepesha macho yake baada ya mimi kunkazia sana macho.
"Aaah aise muda umekwenda saa kumi na nusu saizi nitaenda tu kesho!... Unaelekea wapi?" Nikamtupia swali.
"Hapo kihanga"
"Nami naelekea huko ingia nikusogeze mbele kidogo" nilimuona akisita huku akijifikiria na kukuna mikono yake asijue ama akubali au akatae ofa ile,nikashuka na kwenda kumpokea kiroba chake na kukitia kwenye buti,nilibaini ulikuwa ni unga,bila shaka alikuwa akitoka mashineni.
Tukaingia garini na safari ikaanza,nilitembea taratibu huku nikimfikiria binti huyu,sikujua hasa kwanini alinifanya nimfikirie kiasi hiki,mwisho nikavunja ukimya.
"Naitwa Aloyce Jacob Maliki" nikamtupia macho.
"Naitwa Helena Mtavangu"
"Una jina zuri Helena,nami nikijaaliwa mtoto nitamuita Helena"
"Ha ha ha asante bwana"
"Je! Unasoma?"
"Hapana,nimemaliza form six mwaka jana"
"Kwahiyo unaenda chuo sio?"
"Mmmh hapana,matokeo yangu hayakuwa mazuri sana,nitaenda kusomea ufundi cherehani mwezi ujao"
Tayari tulikuwa tumeshafika kijijini,Helena aliomba nimshushe mbali kidogo ingawaje nilibaini ya kwamba aliishi jirani tu na yalipokuwa makazi ya baba na bibi,yaani mwendo wa dakika nne au tano tu kwa mguu,niliwasili nyumbani na kukuta tayari nimeshaandaliwa maji ya kuoga,nilioga na kujivutia jikoni kuota moto maana baridi lilikuwa ni kali kwelikweli,hadi ilipotimu saa nne nikaagana na waliokuwepo jikoni na kwenda kujipumzisha.
Nikiwa kitandani akili yangu ilitawaliwa na picha ya Helena tu,nilimfikiria kwelikweli huku wakati mwingine nikijishitukia na kujiuliza sababu ya kumfikiria kiumbe huyu ni nini hasa? Je nilikuwa nimempenda? Lakini nampendaje mtu nimemuona siku moja? Au namtamani...niliwaza na kuwazua pale kitandani,sikumbuki ni muda gani usingizi ulinipitia nilikuja kugutuka tayari ni saa mbili asubuhi.
ITAENDELEA...