Binafsi sijaridhika na kasi ya kutumbua majipu bila kuyakamua

money bag

JF-Expert Member
Jan 15, 2016
373
298
Hongera sana mh. Rais, kiranja mkuu majaliwa na mawaziri kwa kazi nzuri na kubwa wanaofanya ya kubaini uozo serikalini na mashirika ya umma na kuwasimamisha kazi wakurugenzi na viongozi mara moja.

Jipu ili lipone kabisa lazima likamuliwe litoe ule moyo wa ndani kitendo cha viongozi hawa kushindwa kukamua jipu hakuniridhishi binafsi.

Nilitegemea mkurugezi aliyeisababishia serikali hasara ya mabilioni na ma milioni baada ya kusimamishwa kazi, akamatwe mara moja ashitakiwe afirisiwe mali zake na afungwe gerezani iwe fundisho kwa wengine.

Kitendo cha kumtumbua/kumsimamisha kazi bila kumkamua/kumfirisi na kumfunga jibu halitapona litaendelea kuwepo pale pale sana sana wamepewa likizo ya kwenda kula hayo mabilioni waliyoiba wao na familia zao.

Tunaomba mhe. Rais na mawaziri kamueni basi hayo majipu mliotumbua moyo na usaha wote utoke ndani ya serikali na mashirika ya umma.
 
Back
Top Bottom