Binafsi naona kilichomtajirisha Dk Mengi;

Binafsi naona kilichomtajirisha Dk Mengi;

Umkonto

JF-Expert Member
Joined
Dec 27, 2018
Posts
3,369
Reaction score
5,941
1. Kuzifahamu na kuzitumua fursa ambazo wengine hawakuzifahamu. Dk Mengi alianza ujasiriamali katika miaka ya 1980, hapo tayari alishaziona fursa, huku wengine wakiwa wamelala na ujamaa wao. Kuimba nyimbo za chama cha jenga nchi.

2. Kwa kujumlisha akili za kuzaliwa, mazingira maskini ya Tanzania kwa kipindi hicho yalimbeba Dk Mengi. Wanasema, mazingira maskini yana fursa nyingi sana. Sasa, kwa miaka 1980 uchumi wa Tanzania ulikuwa mbovu, vitu muhimu viliadimika. Hapo, mengi alianza kutengeneza na kuuza kalamu.

3. Safari ya kwenda Uskochi kusoma miaka ya 1970 ilikuwa ni exposha kubwa sana kwa Mengi. Kumbuka, kipindi hicho Watanzania wengi walikuwa wamefungwa na fikra za ujamaa, ilikuwa ni kuunga mkono juhudi tu za mwalimu wakati huo. Ulaya iliendelea zamani sana, hivyo mazingira na marafiki wa Ulaya walimuinsipaya sana Mengi.

4. Mwisho kabisa, Dk Mengi alikuwa ana akili ya kuzaliwa ya ujasiriamali, maana wapo Watanzania wengi walienda Ulaya miaka hiyo lakini hawakufanya ujasiriamali zaidi ya kupewa vyeo na Mwalimu.
 
UFUNUO WA YOHANA 14:-13 Nikasikia sauti kutoka mbinguni ikisema, Andika, Heri wafu wafao katika Bwana tangu sasa. Naam, asema Roho, wapate kupumzika baada ya taabu zao; kwa kuwa matendo yao yafuatana nao.
#R.I.P.DR.MENGI
 
Back
Top Bottom