Binafsi naona kama mwanadada rapa Dipper Rato amezichanga vibaya karata za kisanii

Mgeni wa Jiji

JF-Expert Member
Jul 27, 2017
8,232
14,280
Wakuu wa sanaa na burudani habari!

Kwa wale wanaofuatilia mziki wa bongo watakuwa sio wageni kwa huyu mwanadada anayejiita Dipper Rato. Binafsi nilimfahamu Dipper zaidi ya miaka 15 iliyopita. Ila ghafla alipotea kwenye game.

Wakati namfahamu Dipper bado alikuwa akitumia jina la Dipper Kivuyo baadae nilimuona akiibukia Vatoloco na akabadilika kiasi akawa sasa Dipper Rato. Ila kisanii bado hakupiga hatua ya kumleta mainstream.

Binafsi niseme zamani nilimuona Dipper kama aliyestahili kumtangulia Roza Ree kwenda mainstream, ila akawa tofauti kabisa, mwanadada Roza Ree alikimbia sana kisanii.

Sasa hivi naona Dipper Rato kama anazidi kujichimbia shimo refu ambalo kamwe hatoweza kutoka ndani yake.

Ili aweze kupenya mainstream, Dipper Rato kaamua kujiingiza au kujifqnanisha na wahalifu (wadudu). Japo wale anaotembea nao na kuwafanya washikaji zake sio wadudu Og, ila kujinasabaisha na wadudu Og ni kosa kubwa kwenye sanaa ya Dipper Rato.

Dipper Rato ameingia kwenye mtikasi ambao kamwe hatoweza kuumudu sababu kwanza yeye sio mdudu Og. Ila wadau muhimu watampuuzia wanamuona kama mhuni mhalifu tu.

Walio karibu na Dipper Rato wamshauri vizuri juu ya kuikuza sanaa yake. Najua kaka zangu John Blass na Defxro Dx mnaweza mshauri mdogo wenu. Atoke hapo alipo maana upepo huo ni kimbunga hatoweza kimudu.
 

Attachments

  • images.jpeg
    images.jpeg
    5.2 KB · Views: 3
Umesema hao sio wadudu og,then means hamna shida yoyote mbona sasa.?

Sema kadem kazuri
 
Umesema hao sio wadudu og,then means hamna shida yoyote mbona sasa.?

Sema kadem kazuri
Shida ipo Mkuu.
Hakutatokea mtu serious akataka kuwekeza kwake. Ni watu wachache wanafahamu kuwa wale sio wadudu bali vijana tu wameamua kupita na upepo wa wadudu.

Hata wale wa Paul bado sio wadudu Og, mdudu Og hana mazoea na serikali, sababu ya mishe zao.
 
Back
Top Bottom